Zanzibar: Wawakilishi nao posho, mishahara juu!

2mbaku

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
316
67
Wakati sakata la kuongezwa posho za wabunge likiwa bado linafukuta Tanzania bara, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) wameongezewa posho na mshahara na kuanza kupokea kwa mwezi Sh. Milioni 4.3 kuanzia Oktoba mwaka huu. imefahamika.

Kabla ya marekebisho yalioanza kutekelezwa mwezi Oktoba Wawakilishi walikuwa wakipata mashahara na posho mbali mbali jumla ya Sh Milioni 3.3 kwa mwezi. Kiwango cha chini cha mshahara Zanzibar kwa mfanyakazi wa Serikali ni 125,000 kwa mwezi.

Ongezeko hilo la Shilingi Milioni moja la mshahara na posho mbalimbali limekuja siku chache baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza posho za wabunge kutoka Sh. 70,000 kwa siku hadi 200,000 na kusababisha manung’uniko makali kutoka kwa jamii.

Julai mwaka huu wajumbe hao wa Baraza la Wawakilkishi walitishia kugoma kuchangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi wakitaka serikali kuzingatia marekebisho ya maslahi yao. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed, alithibbitisha ongezeko la mishahara ya Wawakilishi kwa asilimia 200.

Alisema ongezeko hilo litasaidia Wawakilishi kumudu gharama za maisha zilizoogezeka na kuwatia motisha kufanyakazi kwa bidii chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alisema marekebisho hayo yamekwenda sambamba na marekebisho ya wafanyakazi wote katika sekta ya umma Zanzibar kwa madhumuni ya kusadia kumudu maisha yao.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), Mohammed Mwinyi Khamis alisema kiwango hicho cha nyongeza ni kikubwa ikilinganishwa na kima cha chini cha mfanyakzi wa kawaida.

Mwinyi alisema kwamba katika tathmini yao walipendekeza watumishi wa umma walipwe mshahara wa kima cha chini Sh 234,000 na wafanyakzi katika sekta binafsi walipendekeza Sh 174,000 kwa mwezi.

Hata hivyo, alisema wafanyakazi katika sekta binafsi wameendelea kulipwa kima cha chini Sh 70,000 na watumishi wa umma 125,000 licha ya kupanda kwa gharama za maisha kuazia Januari mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Alisema marekebisho hayo yamekwenda sambamba na marekebisho ya wafanyakazi wote katika sekta ya umma Zanzibar kwa madhumuni ya kusadia kumudu maisha yao.
Bora hawa wana akili kidogo!
 
yaheeee,bora yenu nyie ati mwapandisha kwa wafanyakazi wote huku bara yaheeee ugumu wa maisha uko kwa wabunge tu.
 
Posho ni wimbo unaokubalika na CCM nafsi za wabunge wetu zimeshatekwa na pesa; hoja zinazokubalika ni za kutetea maslahi yao

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom