Zanzibar: Wanaokula hadharani, kuvaa nguo fupi kukiona

Status
Not open for further replies.
Hivi ukiwa umefunga ukaona mwenzako atapiga supu kuku asubuhi asubuhi roho inakutoka na saumu inaisha? Nauliza maana i nilidhani muumini wa kweli aliyefungwa hawezi ingiwa na tamaa hata iweje. Au mnalazimishwa kufunga

Wewe kidogo umehoji kwa busara, kilichopo si kuwatamanisha wanaofunga bali itasaidia kwa malezi ya vijana na watoto wasije kuona kuendelea kula ktk mwezi wa ramadhani ni sawa tu. Hivyo hii inalenga kuwajenga watoto wajue jamii nzima haitegemei kuwaona wakila mchana wa ramadhani.
 
Mwezi wa Ramadhani una heshima maalumu ambayo ni lazima kila mtu auheshimu.
Kwenda zako Mimi mbona sijui nini maana ya mwezi wa Ramadhani? Najilia popote wakati wowote na hakuna sheria inayonibana, msituletee mfumo Islaam hapa Zanzibar kwetu, tena sitaki mtu anipangie mda wa kula wala nini chakula, nikitaka kujilia nguruwe wa kupaka najilia popote na wakati wowote Kum...mae zenu
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imelitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokula hadharani na kuvaa nguofupi wakati huu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alipozungumza na waandishi wa habari jana.

Alisema serikali imeamua kutoa agizo hilo baada ya kujitokeza baadhi ya watu kuonekana wakila mchana hadharani na baadhi ya vijana kuonekana wakiwa wamelewa na kuranda mitaani kinyume na misingi ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha, alisema baadhi ya wanawake wamekuwa wakionekana mitaani wakiwa wamevaa nguo zisizokuwa na heshima.

Waziri Aboud amesema kwamba baadhi ya migahawa na nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitoa huduma mchana katika kipindi cha Mwezi Mtukufu. Waziri Aboud alisema kimsingi wananchi hawazuiwi kula mchana kulingana na imani zao, lakini wanatakiwa kufanya hivyo wakiwa katika maeneo ya faragha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

"Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawataka wale wote wanaojishirikisha na vitendo hivyo waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria pamoja na kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mafundisho yake Mtume Mohammad," alisema.

Aidha, alisema serikali inatarajia wananchi wote Unguja na Pemba watashirikiana kurudisha heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Waziri Aboud amesema serikali imeamua kutoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka Jumuiya moja ya kidini Zanzibar juu ya kuwepo watu wanaokula mchana na kuvaa nguo fupi bila kuzingatia misingi ya mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.
HIVI MAHAKAMA YA KADHI IKIANZISHWA KAMA BAADHI YA WATU WANAVYODAI................ITAKUWAJE...........??? Kuna sheria yoyote kule Zanzibar inayokataza hayo...???? AU ile 'nnji' inatawaliwa KISHARIA..???
 
Wewe kidogo umehoji kwa busara, kilichopo si kuwatamanisha wanaofunga bali itasaidia kwa malezi ya vijana na watoto wasije kuona kuendelea kula ktk mwezi wa ramadhani ni sawa tu. Hivyo hii inalenga kuwajenga watoto wajue jamii nzima haitegemei kuwaona wakila mchana wa ramadhani.
Naomba kutokubaliana na wewe........... UNAPOSEMA JAMII NZIMA UNAMAANISHA HADI WAKRISTU...??? Au ile nchi ni ya kiislamu........... KWANGU NAONA HILI NI TATIZO LA KUINGIZA DINI SERIKALINI...................... WATUELEZA BASI KAMA SERIKALI YAO INA DINI.....
 
Safi sana lazima kuulinda kwa gharama zote mila , desturi na sirka za Mzanzibar.

Hongera sana
 
Naomba kutokubaliana na wewe........... UNAPOSEMA JAMII NZIMA UNAMAANISHA HADI WAKRISTU...??? Au ile nchi ni ya kiislamu........... KWANGU NAONA HILI NI TATIZO LA KUINGIZA DINI SERIKALINI...................... WATUELEZA BASI KAMA SERIKALI YAO INA DINI.....

Kwa Zanzibar ambapo population ni almost 95% waislamu unapozumzia utamaduni lazima dominant group itakuwa ni waislamu, ndio maana sheria kama hizi zipo Zanzibar na si huku bara kwa kuwa hakuna dominant group perse.
 
Safi sana lazima kuulinda kwa gharama zote mila , desturi na sirka za Mzanzibar.

Hongera sana
Amini nakwambia haitazidi hata miaka mitano hamtakuwa tena na habari za kuliomba jeshi la polisi kukamata watu wanaokula mchana katika ramadhan. Nikwambie kitu?

Zamani ni kweli kila kitu kilikuwa kinafungwa, hata sisi tulipokuwa wadogo ilikuwa chakula kinapikwa kimya kimya nyumbani, lakini si sasa! Barubaru pita pale baa ya ccm zenj mida ya mchana mchana kama hujaona watu kama wewe wakila na kunywa na kujisifu kuwa jioni wakirudi nyumbani hamna atakejua kama amekula!

Sa ivi kila kitu kimebadilika, katika huu mwezi zanzibar hupati tena shida ya kunywa bia baridi, kupata msosi na hata ile huduma haramu ya wadada. Kidogo kidogo hamtaiongelea tena habari ya kukamata watu!

Silka zenu mnaziua wenyewe!
 
Nimewasiliana na kile chama cha wauza yule mfugo - CHAWAKITA wanadai hata biashara kipindi hiki imedoda!
 
Kweli tunamchezea MUNGU yaani kweli tujitunze mwezi huuu tu halafu baada ya hapotuendelee kula na kuvaa nguo fupi (uzinzi & Uasherati)?? No haijakaa vizuri, au sijaelewa labda kama sio MUNGU huyu ninae mtumikia
 
kwa hio Zanzibar ni nchi ya Kiislamu? wale waanglikana wa watu na RC maskini weweeeee, sijawahi kuona watu wabinafsi kama hawa, Namshukuru sana MUNGU kuwa mtoto wa Bi Mkubwa...
 
jamani naomba kuuliza? Hivi kwa nini waislamu wanapofunga wanakuwa na masharti mengi sana? je wakristu wanapofunga kwaresima, waislamu huwa wanalazimishwa kula mafichoni? kama ni maadili basi yawepo wakati wote na siyo kipindi cha mfungo tu!
naomba utaratibu wa funga ya kwaresma!masharti kama yapo,mtu ajizuie kwa lipi au matendo yapi na muda gani wa funga?asali vipi?maana yesu alifunga usiku na mchana kwa siku 40!
 
Nguo fupi hazina mpango sema sasa uhuru wa mtu! ngoja niende kuandaa futari kwanza nikirudihapa nitaandika kwa kirefu.
 
Hivi hii sheria ya kutokula hadharani wakati wa Ramadhani iko kwenye ile katiba yetu Chovu? Natamani ningekuwa Zanzibar ningefanya hilo kosa makusudi niangalie wangenishtaki kwa sheria ipi
 
Labda kwa kipindi hiki cha mfungo biashara ya utalii imesimama.... tusiwalaumu zanzbar ni nchi waache waweke sheria zao wanavyojisikia wenyewe kulingana na utamaduni wao...

Niko nawasikia wakina Kibonde hapa, nao wanasema hilo hilo.

Kasheshe mambo kama hayo yasiletwe bara kabisa. Na sababu kubwa ya kuisimamia sheria hio Zenji na Pemba ni uwiano tofauti kati ya wakristu na waislamu.

Waislamu wengi, sababu ni majority, basi ni haki shria kama hiyo kwa kipindi cha mfungo iwepo.

Ila sijui kwanini kuna muungano! Walete referendum tuamue, hasa sie wabara, kwa kweli ni muda muafaka kila nchi iende kivyake sasa, kwani kuna ulazima wa kufuata matakwa ya viongozi wasiokuwepo?
Tanaitaka Tanganyika irudi.
 
nilie4nda Tanga ... wakati wa kufuturu ukifika biashara zimesimama.. jamaa petrol station waligoma kunijazia mafuta eti hadi wamalize kufuturu... hehehehe

“…..Na siku hiyo kipimo kitakuwa kwa haki. Basi watakao kuwa na uzani mzito, hao ndio watakaofanikiwa. Quran 7:8
" Na watakao kuwa na uzani hafifu, basi hao ndio waliozitia khasara nafsi zao kwa sababu ya kuzipinga Ishara Zetu. Quran 7:9
 
Kufunga yatoka moyoni kama unafunga kinafki shetwani ana kazi rahisi sana ya kukuteka, ila mfungo ukkiisha msirudi duniani kwa kasi
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom