Zanzibar wabadilisha katiba ya kutowatambua wapinzani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
MABADILIKO Z'BAR: Baraza la Wawakilishi leo lapitisha marekebisho ya katiba yanayomzuia Rais wa Z'bar kushauriana na upinzani wala kuteua wapinzani kuingia ZEC.
=========================

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 11 ya mwaka 1984, ambayo yatatoa nafasi na kumpa uwezo Rais wa Zanzibar, kuchagua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani ambaye kwa sasa hayupo katika baraza hilo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, katika marekebisho hayo vifungu viwili vinahitaji kufanyiwa marekebisho kikiwemo cha 66 kwa kufanya marekebisho na kufuta maneno ya vyama na kiongozi wa upinzani.

Akifafanua katika kifungu hicho, amesema lengo lake ni kutoa nafasi kwa Rais wa Zanzibar kuchagua nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza ambaye kwa sasa hayupo, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia Uchaguzi Mkuu wa marudio mwaka huu, na hivyo kutopata mwakilishi yeyote na hivyo kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Ameongeza kuwa katika mazingira ya sasa katika Baraza la Wawakilishi, hakuna kiongozi katika Baraza hilo pamoja na vyama vilivyopata wingi wa kura, hatua ambayo imemfanya Rais kushindwa kuteua wajumbe wawili katika Baraza la Wawakilishi.

“Katika Baraza la Wawakilishi la sasa Rais ameshindwa kuteua wajumbe wawili katika nafasi kumi ambapo anatakiwa ashauriane na kiongozi wa upinzani ambaye hayupo kwa sasa,” amefafanua na kuongeza kuwa Kifungu cha 77(2) kinafuta neno la upinzani lenye uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi.
 
:D:D:D Si walianza wao kutompa mikono rais wakati wa kusalimiana. Yaani hawataki ushirikiano. Sasa wamejibiwa rasmi.
MABADILIKO Z'BAR: Baraza la Wawakilishi leo lapitisha marekebisho ya katiba yanayomzuia Rais wa Z'bar kushauriana na upinzani wala kuteua wapinzani kuingia ZEC.
unajua wanasahau as if wao ndo wako juu ya viumbe vyote siku watakapokuwa wapinzani wao wataanza kuilalamikia katiba walio ipitisha wao wenyewe.wasubiri kibanano cha UN kinakuja soon kita wanyorosha,
 
unajua wanasahau as if wao ndo wako juu ya viumbe vyote siku watakapokuwa wapinzani wao wataanza kuilalamikia katiba walio ipitisha wao wenyewe.wasubiri kibanano cha UN kinakuja soon kita wanyorosha,

BAVICHA katika ubora wako. Hizo ni ndoto za alinacha. Msije kufanana na hadithi ya fisi na mkono wa binadamu.
 
BAVICHA katika ubora wako. Hizo ni ndoto za alinacha. Msije kufanana na hadithi ya fisi na mkono wa binadamu.
unacho kisema unakijua au unaropoka tu huku ona ile report ya US waliopeleka un wakitaka zanzibar na tz kwa ujumla ichukuliwe hatua?
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom