Hiyo kodi wanayolipa TRA ni sehemu tu ya faida wanayoipata kwa kufanya biashara na si vinginevyo. Wanafanya biashara kwa kuwa kuna demand na population kubwa ya kununua bidhaa wanazotengeneza. Bakhresa akiondoka kesho au hata akifilisika bado uhitaji wa maji,ngano,ice cream n.k utabaki pale pale, na tena itakuwa fursa kwa wajasiliamali wengine watanganyika kuanzisha biashara hiyo kuziba pengo na kukidhi hilo hitaji na TRA itapata kodi vilevile. Kwahiyo kumbe ni hao akina Bakhresa wanufaikao zaidi na Tanganyika!!
Mnaweza kufanya walichokifanya akina Bakhressa au unaropoka tu. Nenda Tandale na Temeke kila siku zinaanzishwa bakery mpya na kufa na watanganyika mnajiuliza kwanini zinakufa. Wenzetu wapemba, wahindi wanamaadili mazuri ya pesa sie akina meku, nshomile tukipata faida tunataka matawi ya juu unakuta baada ya miaka mitatu hakuna tena biashara. Tuonyeshe kwanza tunaweza badala ya kuwa tunaropoka kufurahisha kijiwe.