Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

Hili wala si tatizo; kwa vile tunaenda kuzungumzia Katiba Mpya ni vizuri Zanzibar waje na hoja ya kupiga kura ya maoni kama wanataka kubakia kwenye Muungano au watoke. Asilimia 60 ya Wazanzibari wakikubali kutoka basi tunawashika mkono wa kheri na tutawasaidia kulipa madeni yenu na kuwapiga jeki kidogo ili muanzie pazuri.

A rational thinking!, Ila Mkuu uamuzi wa Zanzibar kujitoa katika muungano si wa Wananchi pekee, hata asilimia 101 wakitaka kujitoa haitawezekana hata kidogo!
 
Sio mimi nikajifunze historia ya Zanzibar, wewe ukajifunze historia au hukubali kuwa Zanzibar ndio Taifa lililokuwa linatawala hii himaya yote ya pwani ya Afrika Mashariki mpaka Kongo? Au huamini kuwa machafuko Zanzibar yalianzishwa na Nyerere? Au huamini kuwa Tanganyika ndio iliomezwa na Zanzibar? Niambie ni nini katika hivyo huamini nikupe ushahidi wa kitaalam kabisa nawe utowe wako halafu tuendelee, nakuhakikishia huna.

Hii red si kweli-
 Kilwa Kisiwani :: the oldest city in east african history
 
kwa maoni yangu suala la muungano linatakiwa kutolewa somo kwani hata mimi binafsi sijui umuhimu wa muungano zaidi ya kuona unatumika kisiasa kwa kuwakandamiza wazanzibar kufikia malengo yao,navyojua ni kwamba hata marais wa zanzibar ambao wamepatikana nikiwa na mawazo kamili hawajawai kupatikana kwa mapenzi ya wazanzibar achilia mbali walivyorundikana kwenye bunge la muungano mpaka wanatufanyia maamuzi watanganyika!

Serikali inatakiwa kuelewa kuwa mawazo watu ya mwaka 1964 mpaka sasa yamebadilika mno kwa sasa ni lazima elimu ya muungano itolewe tena si kwa kulazimishwa kisha kura ya maoni ipigwe kwa pande zote ili kufikia malengo ambayo ni kama tunauhitaji muungano au la,tofauti na hapo tutakuwa tunajidanganya!,mambo ya kuburuzana yamepitwa na wakati,bado kuna maswali mengi ya kujiuliza je tumeingiaje kwenye shirikisho la afrika mashariki?tutafaidikaje?kama ni faida ni kwa muda gani?na muda ukiisha au hizo faida kukoma tutatokaje?
 
Ndiba unachosema ni kweli kabisa mkuu. Nadhani iko agenda iliyojificha maana ukiangalia the way issue ya muungano inavyobebwa mara nyingi unashindwa kuelewa kuna nini nyuma ya pazia.

Ni kweli wazanzibar wamekuwa kama ndugu zetu na kwa kweli wakati wote tumejisikia hivyo. Lakini kama wao wanaona ni wakati muafaka kujiweka pembeni na kujitenga na bara hili ni jambo jema na haki yao ya msingi. Zanzibar ilikuwepo muda mwingi nje ya muungano na sasa kama wanaona mahitaji waliyonayo ni kukaa nje ya Muungano that is fine also

Kwangu mimi nawaona kama mtoto wa kiume anaejiona mbele ya wazazi ya kuwa amekuwa na sasa anaweza kujitegemea.

Kwa uamuzi kama huu, kama wanzibar wenyewe watajitokeza na kutaka kuwa pembeni ya Muungano inawezekana pia maana hata Katiba yao naamini sio jambo lililokuwa lenye kupendwa machoni mwa watawala wa CCM. Ila hatimaye maamuzi yao yalilazimisha

So wakiamua na kupaza sauti hakuna mtu ndani ya CCM au popote anaeweza kuwazuia.

Hatima iko mikononi mwenu wazanzibar, ule wakati wa kulalamika kunyonywa na bara huku bado mmeng'ang'ania ndoa inayowanyonya umepita, kama mnaona vema kujitenga na bara, okay

Hofu kubwa ya mataifa ya Magharibi ni kuwa kama Zanzibar itajitenga isije ikageuka kuwa kituo cha ugaidi, hii ni hofu ambayo imekuwepo kwa siku nyingi. Mataifa ya Magharibi kila mara yamekuwa yakiisaidia serikali ya mwungano kwa sharti la kuhakikisha Zanzibar haijitengi. Kama mataifa ya Magharibi yataridhika kuwa Zanzibar, hata kama ikijitenga haitafanywa kuwa nyumba ya magaidi, mahitaji ya Zanzibar kujitenga hayatakuwa na kizuizi chochote kutoka kwa CCM, vinginevyo wafanye kazi ya ziada kufanikisha hilo. Hakuna mwenye uhakika wa utengamano kati ya Waunguja na Wapemba mpaka sasa.
 
Kilwa Kisiwani ni the oldest city in East Africa or could be termed one of the oldest cities in the modern world. No doubt about that, hata msafara wa Vasco Dagama ulifikiri kuwa hiyo ndio india waliokuwa wakiitafuta.
Zenj Empire, kama umewahi kuisikia, ilitawala hapo mpaka Sofala. Lakini sidhani kama hili ni muhimu, muhimu ni hili:

Zanzibar ni nchi yenye serikali yake na kila kitu chake ki nchi, hata jina. On the other side, huku kwetu bara. Hatuna.

Hatuna Serikali yetu, hatuna , hatuna, hatuna.

Nadhani ni huku kwetu ndio wa kudai Uhuru kutoka kwa Zanzibar, ndio iliyotumeza na si Wazanzibar kutaka kujitenga. Sisi tupo ndani ya Muungano ambao uliimeza nchi moja ya zilizoungana na kuipotezea uTaifa wake. Si kwa waZanzibari kutaka kujitenga au la, ni sisi wakutafuta Uhuru wetu wa Tanganyika. Kwa sasa hatuna, kwa sasa tuna Tanzania ambayo ni nchi iliyozaliwa baada ya kuungana Zanzibar na Tanganyika, sasa vipi leo wenzetu wawe na kila kitu chao ilhali sisi hatuna hata bendera yetu? Kama si kutawaliwa huku ni nini?
 
Takribani maoni ya Wazanzibari walio wengi mtandaoni na hapa nyumbani basi huhubiri Zanzibar kujitoa ndani ya Muungano.Suali hili kwa sasa limekuwa ndio uradi wa Wazalendo walio wengi. Kwa ufupi wanataka Zanzibar isimame kama Zanzibar na sio Sehemu au hata tuite nchi iliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Fanyeni fasta, mnatunyonya tu wavivu wakubwa nyie!!!!!!!!!!!!
 
Kilwa Kisiwani ni the oldest city in East Africa or could be termed one of the oldest cities in the modern world. No doubt about that, hata msafara wa Vasco Dagama ulifikiri kuwa hiyo ndio india waliokuwa wakiitafuta.
Zenj Empire, kama umewahi kuisikia, ilitawala hapo mpaka Sofala. Lakini sidhani kama hili ni muhimu, muhimu ni hili:

Zanzibar ni nchi yenye serikali yake na kila kitu chake ki nchi, hata jina. On the other side, huku kwetu bara. Hatuna.

Hatuna Serikali yetu, hatuna , hatuna, hatuna.

Nadhani ni huku kwetu ndio wa kudai Uhuru kutoka kwa Zanzibar, ndio iliyotumeza na si Wazanzibar kutaka kujitenga. Sisi tupo ndani ya Muungano ambao uliimeza nchi moja ya zilizoungana na kupoiteza uTaifa wake. Si kwa waZanzibari kutaka kujitenga au la, ni sisi wakutafuta Uhuru wetu wa Tanganyika. Kwa sasa hatuna, kwa sasa tuna Tanzania ambayo ni nchi iliyozaliwa baada ya kuungana Zanzibar na Tanganyika, sasa vipi leo wenzetu wawe na kila kitu chao ilhali sisi hatuna hata bendera yetu? Kama si kutawaliwa huku ni nini?

Hee! we nawe wa wapi? Au ndio ushaukana?
 
Kuanzia sura,majina,rangi,utamaduni na hata kuzungumza kiswahili hatufanani, hata mzanzibar awe mweusi na mtanganyika awe mweusi basi utaweza kuwatafautisha hili begi na hili sanduku. Sasa ni kwa nini watanganyika wasiweze kungana na nchi zilizopakana na wao? Na jengine ni kwa nini watanganyika mumengagania sana muungano muungano kwani lazima wazanzibar waungane na nyiyi ? Musijidanganye muungano unaishi zanzibar kutokana na vibaraka wa ccm/smz ikiondoka leo ccm madarakani basi muungano bye bye wazanzibar muungano tunaoona kama maradhi yakuambukiza ibola na tuko tayari kuwashia kila kitu huko bara lakini turudishe hadhi ya nchi yetu. Mungu ibariki zanzibar na uwashe watanganyika na tanzania walio kataa kwao tanganyika.
 
Attachments

  • tanz300dpi.jpg
    tanz300dpi.jpg
    33.7 KB · Views: 27
hata mi nauchukia sana uo mungano wa ki ccm, tuna ihitaji tanganyika yetu irudi. Bora waende kwa amani.

Waende au sisi tupate Uhuru wetu kwanza? Kuondoka kwa Zanzibar hakutegemei Zanzibar, kunategemea sisi lini tutakuwa huru?
 
wakijitenga tu mimi nipo kariakoo, maduka kumi yatakuwa yangu na yule Mpemba aliyenunua kanisa la Mama Rwakatale nitawagawia wachaga
 
wakijitenga tu mimi nipo kariakoo, maduka kumi yatakuwa yangu na yule Mpemba aliyenunua kanisa la Mama Rwakatale nitawagawia wachaga

Kwani kinachokushinda sasa kuwa na maduka kumi Kariakoo ni nini? si juhudi zako tu? Hao waliokuwa nayo si wamefanya jitihada zao ndio wakayapata? anza na wewe, usingoje vya kupewa.
 
Tutawalilia kwa lipi? fafanua vizuri

Mallaba,

Fanya utafiti kidogo utaona, Wazanzibari ndio wafanya biashara wakubwa Tanganyika, Bakhressa, Zakaria, SSB wote hawa ni either wapemba au waunguja na ni walipa kodi wakubwa TRA sasa wakisema wanaondoka sijui hiyo Tanzania tunayojisifu nayo itatoka wapi. Pili tuje katika utendaji tuna mawaziri wengi wazanzibari na pia kumbuka zanzibar bado inatudai deni la fedha iliyotukopesha wakati tunaunda muungano kutokana na mauzo yake ya karafuu. Hata bado kuna mashamba na biashara mikoani zinaendeshwa na wazanzibar, property nyingi Dar, Arusha, Kilimanjaro na Mbeya wazanzibari wanamiliki imagine the spillover effect yake katika uchumi wa nchi hii?? Nyerere aliyumba tulivyo nationalize our economy sasa sijui sasa hivi akija JK atayumba vp ndio maana nasema tutawalilia
 
mkuu....usipotoshe... TBL , TCC, VODACOM.... Precision air (Shirima)... Akiba Commercial Bank ..,goldmines, diamonds mines migodi na viwanda vingine vingi... hawa si wafanyabiashara.. wanacheza na hawalipi kodi....?..... kuwa makini
 
Mkuu,

Kaulize TRA who is no 1 Tax payer utaambiwa ni Bakhressa kaka. Yeye na TBL wanabadilishana nafasi tu kila mwaka. Hili nina uhakika nalo. Hao wengine vidagaa tu. Cheki vizuri records kaka.
 
Mkuu,

Kaulize TRA who is no 1 Tax payer utaambiwa ni Bakhressa kaka. Yeye na TBL wanabadilishana nafasi tu kila mwaka. Hili nina uhakika nalo. Hao wengine vidagaa tu. Cheki vizuri records kaka.

mkuu...bidhaa za bakhresa zinanunuliwa sana na nani yaani...market.. na ipo wapi.?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom