Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

mi naona mwende tu sioni faida ya kuwa na nyie midebwedo.lakini naomba niwakumbushe kuwa visiwa vyenu ni moja kati ya visiwa vinavyotarajia kupotea duniani
 
Hata ile gharama ya kuhudumia wabunge toka Znz, Umeme nk itakuwa nafuu kubwa kwa Tanganyika mpya. Kila lakheri wazo hili.

Na wataonekana wamejaa kwenye mitumbwi, wakirudi Unguja na Pemba kwenda kupiga kura ya maoni, kama tuonavyo Sudani Kusini kwa sasa.

South Sudan has set a precedence. Zanzibar, off you go.
 
Kwa hali ilivyo mpaka hivi sasa ni wazi kabisa kuwa Zanzibar ndio huru na Tanganyika ndio iliyomezwa.
Zanzibar, wana Rais wao na Baraza lao la wawakilishi, Tanganyika haina.

Zanzibar wana Bendera yao, Tanganyika haina.

Zanzibar wana wimbo wao wa Taifa, Tanganyika haina.

Zanzibar wana Serikali yao, Tanganyika haina.

Zanzibar wana jina lao, Tanganyika haina.

Nadhani ni wakati muafaka kwa waTanganyika kudai haki zao za msingi. Na si Zanzibar kama wengi wanavyofikiri.
 
watu waliokwenye ndoa utamani kutoa kwa maneno tu lakini mwenzi akisafiri tu wanataka arudi siku hiyo2............wasilete porojo za mitaani!!!
 
Kwa tunaoishi vijijini madongo poromoka uswekeni kisiwani Ukara, Zanzibar inanisaidia nini? Hata wakila kona siwezi kufeel changes kwenye maisha yangu! waende tu!
 
Takribani maoni ya Wazanzibari walio wengi mtandaoni na hapa nyumbani basi huhubiri Zanzibar kujitoa ndani ya Muungano.Suali hili kwa sasa limekuwa ndio uradi wa Wazalendo walio wengi. Kwa ufupi wanataka Zanzibar isimame kama Zanzibar na sio Sehemu au hata tuite nchi iliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hizi ni habari za kiintelijensia ndugu?
 
MMKjj na MaxShimba mmeshafunga mjadala huu. Ni haki yao kama taifa lililowahi kuwa huru kutaka kutoka nje ya muungano. Muungano unatakiwa uwe wa hiari na si shari.

Angalizo: Jeuri na dhihaka inayoonyeshwa na baadhi ya waheshimiwa huku ndani dhidi ya Zanzibar si uungwana. OP hajatia neno lolote zaidi ya kusema kile ambacho yeye binafsi angependelea aone.
 
Mi hapa sintofuata upepo...Zanzibar wanatuhitaji nasi tunawahitaji.
Angalieni Sudani mabepari baada ya kuona south kuna mafuta na north wanapendana na uarabuni wameamua kuchochea vita na kuuza silaa mpaka wamehakikisha kua sudani wamejitenga kwa manufaa yao ya kuwinda resources.
Tuache porojo za mtaani maana hata mwalimu alilaani hili....zbar wakijitenga siku zijazo nchi ya KIATA (knjaro, arusha na tanga) nayo itadai uhuru wake maana pia hawaoni faida ya kua pamoja na mikoa mingine zaidi ya unyonyaji...Kumbuka nyerere walikutana na mangi Meli kwenye kudai uhuru wakati wa Mkoloni UK but just Meli alishindwa kuonyesha ramani ya KIATA so akanyimwa uhuru.
Sasa tukianza kujitenga kwa namna hiyo mwishowe tutatenga nchi nzima !!!!!
 
Duh mbona sie watanganyika tuna jazba utafikiri wote ni Makambalization :- mie naona ni jambo zuri kwa Ndugu zangu wanzanzibari kuwa taifa huru, litarahisisha maendeleo kwa vile visiwa. Sasa hii lugha ya kimakamba inatoka wapi jamani, babu katuambukiza vibaya, hili liinchi likubwa ndio maana wanatudowans, unajua hata hizi kanda zingegeuzwa nchi kaskazini nchi, kusini nchi, pwani nchi, nyanda za juu kusini nchi, kanda ya ziwa nchi nk, tungekua responsible aisee on maendeleo side maana resources zingekua monitored vizuri kuliko hii longolongo ya sasa ya kunufaisha dowans
 
Hili wala si tatizo; kwa vile tunaenda kuzungumzia Katiba Mpya ni vizuri Zanzibar waje na hoja ya kupiga kura ya maoni kama wanataka kubakia kwenye Muungano au watoke. Asilimia 60 ya Wazanzibari wakikubali kutoka basi tunawashika mkono wa kheri na tutawasaidia kulipa madeni yenu na kuwapiga jeki kidogo ili muanzie pazuri.
Dah mzee mwanakijiji hata wewe umebariki hili!!????.
Kweli mnataka tuanze kuitana wazanzibar, wachaga, wanyakyusa, wasukuma n.k ndani ya nchi ambayo baba wa taifa alitumia nguvu na upeo wa juu kutuunganisha na mpaka leo hatujawahi kua na vita au dharau za kikabila!!!???
 
Hapo ndio sikubaliani napo, kwa maana ni bora hata wanaotaka kutoka katika Muungano wakipata Asilimia 50.1 ni bora wapewe....
 
MMKjj na MaxShimba mmeshafunga mjadala huu. Ni haki yao kama taifa lililowahi kuwa huru kutaka kutoka nje ya muungano. Muungano unatakiwa uwe wa hiari na si shari.

Angalizo: Jeuri na dhihaka inayoonyeshwa na baadhi ya waheshimiwa huku ndani dhidi ya Zanzibar si uungwana. OP hajatia neno lolote zaidi ya kusema kile ambacho yeye binafsi angependelea aone.

Kama unafuatilia vizuri Wazanzibari ndio wenye lugha chafu na lugha zilizotolewa humu is just a reaction against them! Remember, action and reaction are equal and opposite! Wabara wanaitwa wakoloni, wanyonyaji (japokuwa sioni hata cha kunyonya toka Zenj), wakandamizaji, nk japokuwa Wazenj wamejaza nafasi ambazo hata sio za Muungano huku Bara na tunafanya nao kazi! Sasa unategemea Wabara watatoa lugha gani ya staha kwa hawa ndugu zetu?
 
Mwiba na wenzake nawafahamu fika ila tujitahidi sio kila bandiko liwe ni mwendelezo wa malumbano. Ukweli ni kwamba muungano huu umejaa malalamiko toka pande zote mbili na ni vyema ukafanyiwa tathmini ya kina kwa manufaa ya wote.
 
Dah mzee mwanakijiji hata wewe umebariki hili!!????.
Kweli mnataka tuanze kuitana wazanzibar, wachaga, wanyakyusa, wasukuma n.k ndani ya nchi ambayo baba wa taifa alitumia nguvu na upeo wa juu kutuunganisha na mpaka leo hatujawahi kua na vita au dharau za kikabila!!!???

mimi ni mtetezi wa Muungano; lakini niinaamini muungano wetu ni kuelekea nchi moja kabisa siyo serikali tatu au nne. Nje ya hapo ni kutengana kabisa ili tubakie kuwa na nchi moja. Hatuwezi kuwa na "nchi ndani ya nchi"..
 
Dah mzee mwanakijiji hata wewe umebariki hili!!????.
Kweli mnataka tuanze kuitana wazanzibar, wachaga, wanyakyusa, wasukuma n.k ndani ya nchi ambayo baba wa taifa alitumia nguvu na upeo wa juu kutuunganisha na mpaka leo hatujawahi kua na vita au dharau za kikabila!!!???

Tatizo ni kuwa Wazanzibar wana malalamiko, bahati mbaya sana hawawezi kueleza kwa ufasaha nini wana nyimwa katika muungano. Wabara ambao ni losers wamekaa kimya kwa muda mrefu, lakini sasa enough is enough, waacheni waamue maana sisi hatuna cha kupoteza.
Ili kuthibitisha haya ninayosema, Nimeweka maswali rahisi hapo juu, humu JF hakuna mzanzibar anayejibu kwa hoja bali ni matusi na kashfa, dalili ya kuishiwa hoja.
Tumechoka kutoa mbeleko, kubeba na kisha aliyebebwa anatoa matusi.
 
It has to be an overwhelming majority not a simple majority.

Kwa jinsi halli ilivyo sasa hivi sidhani kama kura au referendum ni kitu kinchohitajika, kinachihitajika si Zanzibar kujitenga, hiyo ni danganya toto, kinachotakiwa ni Tanganyika kudai uhuru wake kutoka Zanzibar:

Kwa hali ilivyo mpaka hivi sasa ni wazi kabisa kuwa Zanzibar ndio huru na Tanganyika ndio iliyomezwa.

Zanzibar, wana Rais wao, Tanganyika haina.

Zanzibar wana Baraza lao la wawakilishi, Tanganyika haina.

Zanzibar wana Bendera yao, Tanganyika haina.

Zanzibar wana wimbo wao wa Taifa, Tanganyika haina.

Zanzibar wana Serikali yao, Tanganyika haina.

Zanzibar wana jina lao, Tanganyika haina.

Nadhani ni wakati muafaka kwa waTanganyika kudai (Uhuru) haki yao ya msingi kutoka Zanzibar.

Mijitu mingine bwana imekazania, nendeni, ondokeni wakati yenyewe ndio iliyotawaliwa. Inashangaza sana.
 
Hili wala si tatizo; kwa vile tunaenda kuzungumzia Katiba Mpya ni vizuri Zanzibar waje na hoja ya kupiga kura ya maoni kama wanataka kubakia kwenye Muungano au watoke. Asilimia 60 ya Wazanzibari wakikubali kutoka basi tunawashika mkono wa kheri na tutawasaidia kulipa madeni yenu na kuwapiga jeki kidogo ili muanzie pazuri.

sasa na hawa wapemba waliojazana tz bara itakuwaje watafute pasport 2 kama wadosi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom