Zanzibar/Tanganyika waliunganishwa vipi na nani kuwa nchi moja kabla ya Muungano?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Hili ni swali la kihistoria si la kisiasa. Kwa wale wanaojua ni jinsi gani na ni nani aliyewaunganisha Wazanzibar kuwa nchi moja na kuwapa utambulisho wa utaifa kuwa wao ni Wazanzibari? Swali hili hili linahusu Tanganyika, ni nani aliyewaunganisha na kuwafanya wajitambue kuwa ni "Watanganyika" na kuwa nchi moja na aliwaunganisha vipi?
 
Tanganyika iliunganishwa na wakoloni hapo EU, ndio sababu ya msingi ya kukosekana uzalendo wa kitanganyika.Zanzibar sina uhakika, nadhani ni natural border :thinking:
 
By the way ipo historia ya kisiwa cha Pemba kuunganishwa na Zenj Empire, ndio hadi leo ukaona bado wakati mwengine Unguja inakuwa confused na kuitwa Zanzibar.
 
jina tanganyika lina majibu tofauti kabisa. wakati wa berlin conference, ujerumani alikabidhiwa sehem kubwa ya aridhi yetu akaiita GERMAN EAST AFRICA, IKWA CHINI YA GERMAN EAST AFRICA COMPANY. YALITENGWA MAENEO YA KILIMO NA YA KUCHUKUA VIBARUA. HUU UKAWA MWANZO WA KUIMARIKA KWA MAHUSIANO KATI YA WATU WA PWANI, KASKZANI,KUSINI NA BARA. MAHUSIANO YALIKUWA KWA KIASI KIKUBWA KIPINDI HIKI.

JINA TANGANYIKA MIE NILIWAHI KUJIBU LILITOKANA NA ZIWA TANGANYIKA LILILOKUWA KIGOMA. WENYEJI WALILITAMBUA KAMA "MULI TANGANYIKA"
MWANA JF MMOJA AKASEMA, CHANZO CHA KUPATIKANA TANGANYIKA, NI EXPLOLER MMOJA ALIYEKUWA AKIELEZEA GEOGRAFIA YA ARIDHI HII NA VILIVYOMO. ALIKUWA AKISEMA FROM TANGA TO NYIKA LAND. WABANTU KWA KUTOKUJUA KIDHUNGU AMBALO SI KOSA, WAKAHITIMISHA KWA KUSEMA TANGANYIKA.
WAPAMBANAJI WA KUTAFUTA UHURU, WALIKUTA TAYARI WABANTU WENGI NDANI YA ARIDHI HII WAKIJITAMBUA KAMA WATANGANYIKA.

KWA UPANDE WA ZANZIBAR, SINA FUNUNU JAPOKUWA KWA MJIBU WA HISTORIA YA MWINGILIANO WA WABANTU NA WARABU......................
 
Swali hili hili linahusu Tanganyika, ni nani aliyewaunganisha na kuwafanya wajitambue kuwa ni "Watanganyika" na kuwa nchi moja na aliwaunganisha vipi?

It's more tricky to be answered...ngoja na mie nisikilizie jibu maana JF hapashindikani kitu.
 
Ningependa tutofautishe kati ya nchi,taifa na dola ili tujadili vizuri Tanganyika.league of nations baada ya wajerumani kuangukia pua WW1 waliwapa dhamana ya kutawala eneo(nchi)lilikuwa koloni la wajerumani likijulikana kama german east africa,likijumuisha Tanzania bara kama tunaivyotambua sasa,na eneo la Ruanda-Urundi ambalo ni nchi za Rwanda and Burundi kama zinavyotambulika sasa.Dhamana hiyo ya utawala,ilpelekea waingereza sasa kuwa na dola(state)mpya ambayo haikuwa sovereign,isiyo na madaraka kamili,ikiwa chini ya dola ya uingereza.
na baada ya ya WW2,mandate ya league of nations ikarithiwa na united nations kupitia kwenye trusteeship council ya umoja wa mataifa.kwa hiyo uingereza iliendelea tena kusimamia ardhi,na dola waliyoitengeneza kwa ajili ya utawala,kwa niaba ya umoja wa mataifa.kwa hiyo nchi ya tanganyika ipo tangu duina iumbwe,imeitwa majina tofauti,imekuwa sehemu ya mataifa tofauti,lakini mipaka yake ya sasa na jina hili,imeanza mwaka 1922.
sasa eneo hili(nchi)ambalo waingereza waliendeleza dola mpya ya tanganyika,baada ya ruanda urundi kupewa mandate wabelgiji,nadhani mgao ulizingatia ukaribu na nguvu ya ushawishi,kenya na uganda walikuwepo uingereza,DRC walikuwepo wabelgiji,ingawa wareno walikuwepo msumbiji,ndhani nguvu yao ilikuwa mgogoro.mpaka tunashughulikia uhuru wa dola ya tanganyika,inayomiliki nchi ya tanganyika ya mipaka ya tanzania bara,tulikuwa na mataifa(jamii za watu wenye asili,utamaduni,utawala,lugha,eneo lenye mipaka,mfumo wa usuluhishi na lengo moja)yanakaribia 100.wakati dola ya tanganyika inaingozwa na waingereza,haikuwa nia yao kuunganisha haya mataifa ili liwe taifa moja la tanganyika,waliyaita makabila,kama walivyoitwa wao na warumi,na wakaendelea kupepea muendelezo wa zile tawala za mataifa ya awali,ili mradi tu zinatii amri ya utawala wao,kwa hiyo waka divide and rule,waka hakikisha viongozi wa yale mataifa wanapata privilege na sifa OBE zilkuwa kadhaa,ili dola hii isije kuwa taifa,likawa na nguvu kubwa mpaka ishindikane kutawala.utaona taifa moja kule kilimanjaro ambalo lilikuwa na nguvu,lilianza jitihada zake kudai uhuru wake peke yake.ambayo ni sawa tu.kuna taifa lingine nadhani kule arusha lilifikiria uwezekano huo.vuguvugu la kupatikana uhuru ndio mwanzo wa kuanza kufikria utaifa wa watanganyika,lakini mwanzo mkazo ulikuwa sana kwenye uhuru,kuliko utambulisho wa watu.tulijiona ni kama watu wasiofahamiana wametekwa na jambazi mmoja,basi tushirikiane tumpige kwanza mwizi.lakini siku zilivyokuwa zinazidi kwenda,na watu wa mataifa haya tofauti walivyokuwa wanakutana,kwenye elimu,michezo,biashara na kazi,na nia ya uhuru kuongezeka,nia ya utaifa nayo ikaja.lakini mtu ambaye kwa maoni yangu amechangia sana kwenye kutengeneza taifa la tanganyika ni mwl Nyerere,muono wake ulikuwa kwamba haya mataifa yooote yawe watu wamoja,tujenga taifa moja,tujitengenezee misingi,mwelekeo,hatima kama watu wamoja,kueleka uhuru,na kitambo baada ya uhuru alielekeza nguvu zake nyingi sana,kwenye ujenzi wa taifa,sio kutufanya kuwa ethnically homogeneous,hapana,traits,mtazamo,dhamira,utambulisho,mwelekeo,utamaduni,lugha,desturi...kwa hivyo yeye mchango wake ndio mie naouona mkubwa kuliko watu wengine kwenye kujenga taifa la tanganyika.tarehe ya uhuru ni 9 desemba 1961,lakini hiyo ni tarehe ya dola ya tanganyika kupewa uhuru,jitihada za kuunda taifa la tanganyika,tunaweza kuziweka sambamba na active political mobilization period,miaka ya kati ya hamsini.kujenga taifa ni kazi kubwa sana,inataka consistency time,undertsnading commitment,ambavyo ni haba siku hizi.baada ya muungano,jitihada za ujenzi wataifa zikawa za kujenga taifa tanzania,tukafundishwa uzalendo na kuchanganywa kama karata,tukapelekwa jeshini huko tujuane vizuri,tuwe wamoja.ila sasa tumechoka kuwa taifa tanzania,tunataka kurudi kwenye taifa tanganyika ambalo halipo,kwani hata taifa tanzania halijatengemaa.bado..zanzibar.?
 
Wayuropa wa mwanzo, (sisemi wa kwanza, kwani kuna historia inaonesha kuwa wayuropa walifika visiwa vya Pemba kabla ya Vasco Da Gama kufika Sofala) Wareno walipotuwa Kilwa, walikuta ni mji ambao una nyumba za rangi, wakati Yuropa walikuwa hawajui rangi za nyumba, walikuta nyumba za ghorofa, walikuta sahani na bilauri za udongo "chinaware", wakati wao hawajui chinaware ni nini, walikuta watu wanavaa nguo za hariri na lasi wakati wao hawajui hariri ni nini, Walikuta sarafu za Dhahabu, walikuta dola inayojitawala yenyewe (ukanda mkubwa wa Pwani ya mashariki ya afrika kama si wote), walikuta mabaharia wanaoijuwa bahari kuliko wao. Walikuta Waislaam na Uislaam.

Mwanakijiji, nakushauri pitia Masheikh na watafiti wa KiIslaam uwajuao, watakusaidia sana katika hili. Majina yote hayo, Tanganyika, Zanzibar, Africa yanatokana na lugha ya Kiarabu. Usishangae nikikuambia hata Arusha ni jina la Kiarabu "derived" kutoka Arsh, kama ilivyo Dar Es Salaam na mengine mengi hapa Africa na duniani. Kwani Waarabu wana historia ndefu sana ya kusafiri baharini na nchi kavu. Utashangaa.

Kama kuna mtu mmoja anaweza kukusaidia, ni muandishi na msanii maarufu wa zamani hapo Nairobi, maarufu sana kama Mzee Pembe. Kama una mawasiliano na watu wa Nairobi nnakuasa wakakuulizie haya maswali yako kwake (kama yu hai) ni kisima cha elimu na historia, nyumbani kwake kulikuwa hakuna nafasi kwa vitabu vilivyo sheheni kila pahala. (I met him way back in 1982 in Nairobi).

Na ntapekuwa makabrasha yangu kuona vipi ntaweza kusaidia. Umenikuna kuulizia historia "for a change" ni katika hobby zangu.
 
Back
Top Bottom