Zanzibar: Risasi zarindima!

Status
Not open for further replies.
Hadi magamba warudishe nchi kwa wenyewe.

Wala hakuna hoja, mtu mmoja akiukataa utanzania utafanyeje? Hapendi kuwa mtanzania anaruhusiwa kupata uraia wa nchi nyingine kwa hiyo atafute kule Rwanda, au DRC kote kuna uraia wa bwerere??? So kugeuza nchi ni mali yako kwa vile wawe ni ....
 
"naam wacha watupeleke rumande sote tupo tayari, kama baadae itakuja al qaeda au nini hiyo ni juu yetu, halikuhusu"

Kama sote tuko Zanzibar inakuweje halituhusu? Kwa nini wewe uone linakuhusu zaidi? Mifumo ya utawala na demokrasia si ipo, na hatukufurahi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa? Labda tuite umoja wa kizanzibari....kwa nini bado hatutaki amani jamani?
 
Kile kikundi cha UAMSHO kinachodai zanzibar huru kikidai hakitaki muungano sasa hivi kinatawanywa na FFU kwa mabomu ya machozi na risasi baada ya risasi kadhaa kupigwa hewani.

Wapo hapa Kisonge wakitaka kuelekea kituo cha polisi cha MKUNAZINI. Fujo hizi ni baada ya viongozi wao leo kukamatwa baada ya swala ya magharibi na leo walikua na mkutano eneo la Lumumba.

Inaonekana wewe REDIO KIFUA usiwandanganye watu wazima kwenye mtandao huu unawapotezea wakati, Viongozi wote wa Muamsho wako salama na sala ya isha alitusalisha Sheh Mselem na ndio amiri wa Muamsho, ikiwa unataka kuwafurahisha ndugu zako basi usiwaeleze uongo hapa hatupo katika vita vya Iraq na habari za Saidi siaf wa iraq.

Muungano ni hiari tu ,ikiwa upande moja utakataa wewe unaumia nini? niaibu jinchi lenye ardhi kubwa,rasilimali nyingi kungagania Muungano wa kijinchi chenye watu less milion moja Sheme& sad.

MUUNGANO UKIVUNJIKA UNAUMIA NINI WEWE?.ilikuwa laumuhimu udai TANGANYIKA YAKO KWA MAGAMBA NCHI YENYE HISTORIA YA VIKONGWE WENU NA VIZEE WENU WALOPIGANIA UHURU WA HISTORIA YENU.
 
Kwatarifa yako Jumuiya ya Mashehe Uamsho Zanzibar imepata baraka zote kutoka kwa viongozi wao wa Smz, Zanzibar itagombolewa na wazanzibar wenyewe sio vyama vya siasa.
 
Watu wanaona sasa! Aibu yao wao waliolala, na watu wote waseme amen!
 
Wazanzibari walishakataa muungano siku nyingi kwa nini walazimishwe? Waachwe wafanye maamuzi juu ya nchi yao manake ina sifa zote za kuitwa nchi na vilevile muungano ulikuwa baina ya nyerere na karume sasa hawa watu hawapo tena kwa hiyo wana haki ya kudai uhuru wao
 
Wazinzabari wana haki ya kudai aina kile wanachoona ni haki yao nashindwa kuelewa busara ya viongozi wa juu iko wapi?

Lakini muhumi ningeshukuru kupata maoni toka kwa Mzenji73 na abdulahsaf kuhusu wale wabunge toka Zanzibar waliomtukana Mh Lissu bungeni wakati wa mjadala wa bunge la bajeti mwaka jana. Kimsingi alichosema Lissu ndicho watu wa Zanzibar wanadai sasa hivi kwamba wananchi toka pande mbili waachwe waamue kama wanautaka muungano au la. Lakini baadhi ya wabunge toka Zanzibar waliamua kumtukana Lissu. Sasa napata shida kujua nani aliwatuma, na je mawazo yao yanawakilisha hisia/maoni ya wanzanzibari? Na kama jibu ni HAPANA, kwa nini basi hatukusikia watu wa Zanzibar wakikanusha kile wabunge hao walikuwa wanatetea?
 
Last edited by a moderator:
"naam wacha watupeleke rumande sote tupo tayari, kama baadae itakuja al qaeda au nini hiyo ni juu yetu, halikuhusu"
Regardless lakini mpaka watu watakapo hacha hubiri na kuongopea watu kuhusu athari za muungano ambazo si za kweli na kutumia chuki tu dhidi ya watu wengine lazima sheria ichukue mkondo wake.

Wewe unaona wakombozi wengine tunaona ni demagogues tu ambao wanatumia hisia na imani (especially religious one) inayotawala ZNZ kutengeneza chuki, muungano hausiani na chuki dhidi ya wabara wala dini nyingine if anything ni economical development and the impedement associated with it.

Lakini dini ibakie dini tu, na mashee (tena uchwara) wanaohubiri chuki wakileta midomo ni bakora tu na kichapo nothing else because that has nothing to do with political cause or the independence of ZNZ and its development.

Safi sana.
 
Is it M 4 C? Zanzibar ikijitenga Tz inaweza kumeguka na kuzaa nchi nyingi zaidi. Upande wa kusini, magharibi na North.
 
Zanzibar ni koloni la Tanganyika!
yes-nazan hata baadhi ya viongoz wa huku zinjibari wamekuwa planted na wabara-sema kwa kuwa public ya zinjibar ipo kama ilivyo-hawawez liona hili-

kuna wale viongozi wa chama wazee wasiotaka ,kusikia muungano unazungumziwa huku bara,sasa sijui watatoa kauli au watakaa kimya baada ya kusikia habari nzuri kama hizi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom