JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Watanzania said:Acheni Zanzibar wajitenge ili kanuni ya historia aliyosema Mwalimu Kambarage itimie. Baada ya kujitenga watagundua kumbe siyo wamoja, kuna Wazanzibar na Wapemba. Dhambi ya ubaguzi itaendelea kuwatafuna hadi waone kumbe hata Zanzibar kuna wazanzibara na wanzanzibari. Wazanzibara wakiondolewa Zanzibar, Wazanzibar wataendelea kubaguana hadi mwisho. Wapemba nao itakuwa hivyohivyo, wataona kuna wapemba koko na wapemba weupe. Ubaguzi utaendelea hata wale weupe watajiona si wamoja, kuna wapemba wa Saudia, wapemba wa Oman na wapemba wa kireno. Watanganyika watendelea kuwa wamoja kwa kuwa hawatakuwa wametenda hiyo dhambi ya ubaguzi. Fanyeni haraka wazinzibar na wapemba kujitenga ili kanuni ya historia itimie.
Watanzania,
..mambo yakienda mrama Zanzibar, basi majirani zake wote wataathirika kwa namna moja au nyingine.
..wa-Tanganyika tunapaswa kuomba Zenj iwe na amani na maendeleo.