Zanzibar naona mpaka kieleweke: sasa nafasi za uwakilishi kimataifa(ubalozi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671

kwa kweli tunakoelekea kunatisha, likiisha hili linaibuliwa hili:

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema hakuna uwiano wa kutosha katika nafasi za kazi za utendaji kwenye afisi za kibalozi nje ya nchi kati ya vijana wa Zanzibar na Tanzania bara.

Waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema tatizo hilo ni moja ya kero za muungano zinazoshughulikiwa ili wanzanibari waweze kuajiriwa katika afaisi hizo.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema serikali imeona upo umuhimu kwa nafasi za ajira katika ofisi za kibalozi kuajiriwa kwa usawa kati ya vijana wa Zanzibar na Tanzania bara. Hata hivyo waziri Aboud amesema kuchelewa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya muungano likiwemo suala hilo kunaweza kuwafanya wazanzibari kutokuwa na imani kwa vile hawafaidiki na matunda ya muungano.


source:
HAKUNA UWIANO WA UAJIRI NAFASI ZA KIBALOZI | Mzalendo.net
 
nnachokiona kwa uwazi juu ya hili kuwa huu muungano hasa wazanzibari hawautaki, lkn wanatafuta sababu nyengine. sasa nnajiuliza kwa nn kuzunguka? kinachoogopwa nn ?


si watangaze tu kuwa jamani eeeh, sisi muungano basi, na tupange jinsi ya kutafuta kuuvunja kwa amani.

maana sasa tunapoelekea kunatisha
 
Tanganyika ina idadi ya watu 43 milioni,Zanzibar ina idadi ya watu 1 milioni.Tukitafuta formulae ya usawa idadi ya watu lazima iangaliwe,gharama za uendeshaji nacho ni kigezo muhimu usije kuta Zanzibar mchango wake zero halafu wanalalamikia ajira.
 
Hivi hawa jamaa vipi? Kila kitu wanataka kiwe sawa? Muungano wa wapi huo? USA ni Muungano wa nchi nyingi lakini husikii Jimbo la Texas au Hawaii au Florida wanalalamika hawana mwakilishi nje ya nchi!!!!

Cha msingi ni maslahi ya Taifa haijarishi katoka State ipi. Kweli acha NYERERE aitwe Mtakatifu aliyaona haya zamani sasa yanatimia!!! Nyerere alisema huo ni ulevi tena ulevi wa madaraka!!!

Mimi nawashauri hao wawakilishi hebu wajadili jinsi ya kuwaletea maendeleo wazanzibar!!! Sisi wengine tumeoa na tuna ndugu kule mbona mnataka kutugombanisha na ndugu zetu kwa tamaa zenu za uongozi na ving'ora vya magari!!!!!!
 
unajua huu muundo wa muungano ndio unaosababisha yote haya.


ukweli nchi hizi mbili kuungana ni vichekesho, kwanza eneo, zanzibar eneo lake ni dogo na bara ni kubwa kwa hio inakuwa ngumu hata kugawa mikoa na mengine

pili watu idadi ya huku na kule haziendani, sasa kila jambo linalohusu rasili mali watu mambo huwa mazito.

zanzibar iwe huru, au kuwe na serikali tatu au moja9ambalo wazanzibari hawapendi kulisikia)


hili suali tuwe majasiri kuliamua bila ya kupambana na kutumia nguvu, tuwe tayari kuchukua maamuzi mazito
 
Tatizo letu si muungano wetu ila ni maswala ya muungano kutoka tisa kwenda mambo lukuki - ndio tuongee sasa. Sioni shida kwanini zanzibar ikijieleza kidogo tu tunadhani wanataka kuvunja muungano sio kuboresha?
 
sijsmwelewa anatofautisha tanzania bara na zanzibar au tanganyika na zanzibar. Kama ni tanzania bara na zanzibar hakuna vitu kama hivyo,mama zanzibar aliolewa na baba tanganyika akazaliwa tanzania.

Sasa kisheria kama kuna ambaye haridhiki arudi mezani kwa mazungumzo akitumia nafasi yake kisheria,kama mama anataka kuvunja ndoa ajadiliane na mzazi mwenzake tanganyika walipokutana sisi hatukuwepo.

Asiongee na watoto kwanza wamepumzika sasa hivi ili wakue,naona mama ameanza kutembea na wanaume tofauti tofauti ili kumchanganya baba ila naona baba kwa sababu ya busara anatulia kama haoni,mama ngarama zote ni za baba hana lolote zaidi ya kupiga hina na kukaa barani na kupiga soga.

Ushauri kwa mama hata hao wanaomdanganya tayari wameshaona jinsi alivyokuwa hana msimamo,atulie aendelee kula ugali wababa.
 
Tatizo letu si muungano wetu ila ni maswala ya muungano kutoka tisa kwenda mambo lukuki - ndio tuongee sasa. Sioni shida kwanini zanzibar ikijieleza kidogo tu tunadhani wanataka kuvunja muungano sio kuboresha?
Mutajuwa wenyewe siye tushachoka na hizi ngonjera zenu za kila siku kuhusiana na muungano....maana ccm na cuf ni baba mmoja
mama mmoja (wameungana) sasa musichokaa chini na kuzungumza ni kitu gani? mara Jussa,mara Sitta,mara Shamuhuna,mara
Tibaijuka' aaaah? tumewachoka jamani! hatuli tukalala kwa amani kisa nyie Wakojani na Wakwere? kwenden zen huko.....
 
hawa zanzibar wanakuja kuisoma tanganyika vyema-ngoja aingie kiongozi mwenye kufanya maamuzi magumu,ndo watajua,
kila siku wanaleta usumbufu
 
Mh;kwa kweli inatisha!!!!
Zanzibar kila siku tunawaasa mtoke tu kwa amani;hizi chokochoko za nini?
 
tanganyika ina idadi ya watu 43 milioni,zanzibar ina idadi ya watu 1 milioni.tukitafuta formulae ya usawa idadi ya watu lazima iangaliwe,gharama za uendeshaji nacho ni kigezo muhimu usije kuta zanzibar mchango wake zero halafu wanalalamikia ajira.


wee, hapa kuna muungano baina ya nchi mbili tanganyika na zanzibar! Hapa pana zungumziwa haki sawa ktk muungano huo! Hapazungumziwi muungano wa "population" au idadi ya watu bali ni muungano baina ya nchi na nchi!
Zanzibar nchi maskini hata kama wangeungana na nchi tajiri na kubwa kama nigeria suala ni mgawanyo sawa baina yao! Sas vigezo vyako hivi vya kudai tanganyika milioni 43 na zanzibar m.1, na uchangiaji wa pato la nchi wewe umevitoa wapi? Au viko ktk mkataba wa muungano?

Kwani wakati mnaungana nao hamkujua zanzibar ina watu milioni 1? Hakuna kitu kinachoniuma kama unafiki na uhasidi!!!
 
kuficha donda dungu -- ndugu zangu. Zanzibar endeleeni kudai haki zenu zote sisi watanganyika tunawapa support.
 
Sijui kuna siri gani hadi viongozi wa tanganyika waendelee kuwaoa hawa jamaa. vunja muungano wamalizane wenyewe kwa wenyewe
 
Do we really need Zanzibaris? They need us

What is their contribution towards the cost of running the union affairs? They contribute nothing. They deserve nothing.

We should demand that contribution towards the costs associated with our union should be 50/50

Let them break away and leave us in peace. they are together only because of the union. once the union is not there they will be like Somalia
 
Ajira sio suala la Muungano. Muhimu ni hizi ajira za KITANZANIA kuwekwa wazi. JMK hailindi na kuitetea KATIBA ya JMT
 
Waangalie pia na huku kungine:
-JWTZ tuwe nusu kwa nusu.
-Police, UwT tuwe nusu kwa nusu.
-BUNGE nalo wavunje BLW kisha tuwe nusu kwa nusu.
Kwa namna hii na mwendo huu kila MZANZIBARI atakuwa kwenye AJIRA.
 
Ntaka nijue:
  1. je zanzibar inagharimia nini kwenye hizi balozi zetu?
  2. ikiwa itakuwa huru itamudu yenyewe kuwa na hizi balozi?
 
Back
Top Bottom