Zanzibar Kuwa Nchi

nenda ukalime wewe kabwela... tarehe ya muungano inajulikana na kwahiyo sio kitu cha ajabu kama tu waTanganyika wakisema nawao basi muungano huu inawezekana kuvunjwa... ninacho amini mimi ni kuwa waZanzibari wamechoka kuburuzwa... this is the beginning of the end...

Hakuna Mzanzibari aliyeburuzwa, acha kupandikiza mawazo ya chuki kwa hasara ya nchi yetu!
 
Hiyo Serikali ya Tanganyika itatusaidiaje kuondoa umaskini? Tunashabikia vitu ambavyo mwisho wa siku tutajikuta tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele! Zenj wanataka kujikabidhi OIC ili wapewe misaada na Waarabu, Wakoloni wao wa zamani, ndio hiyo move ya kujiita nchi ndani ya nchi!

Sio suala la umasikini, ni suala la kuamua hatima ya nchi yetu. Sina sababu ya kulipa kodi kwa wabunge 80 ambao hawathamini kuwa wao ni sehemu ya muungano,na kisha wakaamua mambo yalio ''nje ya nchi yao'' ndani ya nchi yetu. Hatuwezi kubeba gharama za muungano kwa wenzetu wasioutaka. Mfano Kwanini nilipe umeme bei juu kufidia ule wa bure kwenda zenj. Lakini la muhimu ni kuwa muungano uwe kwa maslahi yetu, kwa mantiki tu 70% ya benefit za muungano zinaenda zenj. Fikiria ajira bara[ 60% znz wanaishi na kufanya shughuli bara],
Watu wa bara approx 40 Million wanafaidika na nini kutoka 900,000 population. !!! je sio kinyume chake!
 
Asante sana kwa hiyo info. Sisi ambao hatukusoma gazeti hilo umetufumbua macho. Kama mambo ndo hayo ni afadhali kuwa na serikali tatu.
 
Zanzibaaaaa!!Nasikitika sana pale nisikiapo kuwa wazanzibar wanatamani muungano ufutike ukweli wote wanaoshabikia niwale walio katika uduni wamawazo na ubinafsi na uchoyo wa madaraka.
Tukisema basi muungano watapata pigo kubwa kiuchumi tofauti nawanavyofikiri ebu jiulize nje ya muungano nifaida gani tunapata??au nimazaogani tunapata kutoka zanzibar kusema tukitoka basi!!Muungano ulikuwa nikiunganishi kwakuwa sisi na wazanzibar tulikuwa na mwingiliano mkubwa wakijadi na mila!!
Lakini inasikitisha wanakuwa navituvidogo kama vya mke mwenza!mara wimbo wataifa wakwetu mara bendera yetu lakini mwisho wasiku wanarudi kulekule!!hivyo kuvunjika muungano nipale watakapo kuwa naushawishi juu yakatiba ya muungano kubadrisha vipengele nasiyo rahisi kwani kila rais aendaye magogoni lazima kuwe na miiko ya utawala hata kama rais ni Bilal,Saif akifika ikulu ya magogoni atakuta kanuni zautawala!!Kuilinda nakuishimu katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania!! Nakuakikisha unaulinda Muungano kwa nguvu zako zote!!! No matter wewe ni nimfuasi wa chama gani!! Nasisi tuna ahidi kuulinda muungano wetu ulio wekwa na wa asisi wetu wapendwa Rais JK.Nyerere na Rais AB.Karume kwa ajili ya manufaa ya waTanganyika na Wazanzibar na kuunda NCHI MOJA TANZANIA ZIDUMU FIKIRA ZA MWENYEKITI:smile-big:
 
Hata kama CUF wanataka kuvunja muungano ni haki yao ya kikatiba ya kuwa na mawazo tofauti... muungano utakufa katika uhai wako( utashuhudia kuvunjika kwake) nchi ngapi ziliungana na kuvunja muungano ? kwanini isiwezekane Tanganyika na kuwa kama zamani? kuna mtu mmoja alisema hapa kuwa tatizo sio kuvunjika muungano bali waTanganyika hawapendelei kulitumia tena hili jina lao...inawezekana ikawa ni kweli...


It will be a treason, wameshafaidi mali zetu nyingi na wanataka waendelee kufaidi nje ya Muungano. Zanzibar tunawabeba ila kelele nyingi. Sasa ni ubabe tu, askari wa huku kule, mkileta nyoo, ni kichapo kwa kwenda mbele! Mtaungana mtake msitake!
 
Nyinyi mlivyoiuwa Tanganyika mlitegemea na waZanzibari watafuata ...ZANZIBAR ipo pale pale na hiyo Tanganyika mtairushida tena kama zamani muda sio mrefu sana...acheni kupoteza muda wenu kuishikilia Zanzibar... kuna mikoa mingi hapa Tanganyika inahitaji kuangaliwa...

Tanganyika ikirudi nasi watu wa Tanga tutadai jamhuri maana mjerumani alipokuja aliikuta Tanga na pori(nyika) akaaita nchi Tanga & Nyika hatimaye Tanganyika.........
 
Sio suala la umasikini, ni suala la kuamua hatima ya nchi yetu. Sina sababu ya kulipa kodi kwa wabunge 80 ambao hawathamini kuwa wao ni sehemu ya muungano,na kisha wakaamua mambo yalio ''nje ya nchi yao'' ndani ya nchi yetu. Hatuwezi kubeba gharama za muungano kwa wenzetu wasioutaka. Mfano Kwanini nilipe umeme bei juu kufidia ule wa bure kwenda zenj. Lakini la muhimu ni kuwa muungano uwe kwa maslahi yetu, kwa mantiki tu 70% ya benefit za muungano zinaenda zenj. Fikiria ajira bara[ 60% znz wanaishi na kufanya shughuli bara],
Watu wa bara approx 40 Million wanafaidika na nini kutoka 900,000 population. !!! je sio kinyume chake!

Sijui kama takwimu ulizotoa ni sahihi au la, lakini ulitegemea Muungano usiwe na maingiliano yoyote ya wananchi wake, sasa huo utakuwa ni Muungano gani? Tukiacha mawazo ya kibaguzi ndio tutajenga nchi yetu!
 
Ndugu zetu wa visiwani hawajielewi, mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni kuwakomboa dhidi ya utawala wa waarabu lakini cha ajabu leo hii wazanzibari hujitukuza na kujiona kama wao ni waarabu kama Tanzania bara tungekuwa na rangi ya kiarabu wangenyamaza kimya, tumewabeba sana lakini hawabebeki, vugu lote hili linatokana na dhana ya kuwa kuna mafuta Zanzibar. Cha msingi Tanganyika na irudi na huo muungano kama hawautaki mpango wao CCM acheni kulazimisha mambo.
 
nenda ukalime wewe kabwela... tarehe ya muungano inajulikana na kwahiyo sio kitu cha ajabu kama tu waTanganyika wakisema nawao basi muungano huu inawezekana kuvunjwa... ninacho amini mimi ni kuwa waZanzibari wamechoka kuburuzwa ....this is the beginning of the end...

Hivi Wazanzibari wanaburuzwa nini jamani. Elimu wengi wameipatia bara UDSM, SUA n.k. hivyo kuwatoa tongo tongo nakuanza sasa kuzungumza. Chakula kwa kiasi kikubwa kinatoka bara (mchele, mahindi, maharage kutoka mikoa ya Mbeya, Morogoro, Shinyanga n.k.). Sasa badala ya kutushukuru kwa kuwasomesha na kuwalisha wao wanajitia ujuaji usio na mantiki.
 
Rasimu ya mabadiliko hayo, niliyaona kwenye kikao fulani cha nchi wafadhili, nikiamini yangewekwa hadharani ili yajadiliwe na Wanzazibari kabla ya kufikishwa Barazani.

Maana ni kuwa Bara iko very much aware kila kinachoendelea Zanzibar, kwanza waliomba bendera, halafu wakaomba wimbo wa taifa, sasa hawajaomba mipaka, bali wametangaza mipaka ili Zanzibar iwe nchi in terms of defined teritory ila usiwe na shaka, hiyo ni mipaka jina tuu, kama ulivyo wimbo wao wa taifa ni wimbo tuu, na bendera yao nayo ni bendera tuu.

Kama wewe nyumbani kwako unaitwa Baba, mwanao akalipenda sana jina la baba, ukakubali naye aitwe baba, akiitwa baba anafurahi, hivi wewe sasa ndio hautakuwa baba?. Wewe utabaki baba wa ukweli na yeye baba jina.

Hivi ndivyo ilivyo status ya Zanzibar, ni nchi jina tuu ila sio dola kwa sababu bado haina vyombo vya ulinzi, vyombo vya dola, Jeshi, Polisi, TISS etc, unless KMKM ndio polisi wao na JKU ndio jeshi lao, them huu utakuwa uhaini 100%.
 
Naona mnatapa tapa tu saivi...alitusumbuwa Nyerere...kweli...kwasababu alikuwa dikteta...basi hata akina Kikwete...na Pinda tumewalea na kuwatawazisha mavi wenyewe...!!!sisi mwendo mdundo..muwe baba...mama...sisi haaooooooo kama Sudan Kusini vile!
 
Naona mnatapa tapa tu saivi...alitusumbuwa Nyerere...kweli...kwasababu alikuwa dikteta...basi hata akina Kikwete...na Pinda tumewalea na kuwatawazisha mavi wenyewe...!!!!
Janius, baada ya kusema mmewatawazisha, ilitosha sio lazima kumalizia kwa maneno mengine hayo ya ******!.
 
Kinachoniishangaza kwa wale wanaoona kuwa Zanzibar inataka kujitutumua kutoka katika katika makucha ya Watanganyika - kutoa hoja zisizo msingi, kwa mfano kusema wazanzibari wanalishwa na kusomeshwa na Tanganyika ni hoja ya kitoto kwani yale ni mashirikiano ambayo yanafanywa na nchi mbali mbali. Ni watanganyika wangapi wamesomeshwa bure na Warusi na Wachina?. Au kuzungumzia wazanzibari kuwepo Tanganyika mbona Watanganyika wako sehemu nyingi tu duniani ikiwemo hapa Zanzibar? Linalotuudhi wazanzibari ni tabia ya Watanganyika kuja Zanzibar na kufanya chokochoko za kisiasa kwa kushirikisha katika matawi ya CCM na baadae kufanya maamuzi kwa maslahi ya Tanganika.Ni kawaida kuona Mbara alofika Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita tu kuwa katibu wa Tawi la CCM au Sheha wa shehia fulanii na baada ya hapo anakaribisha wenzake ili wawe na sauti katika masuala yanayowahusu Wazanzibari. Munadhani hizi maskani zinazoleta chuki visiwani kama vile Kisonge washika dau wakubwa ni kina nani?

Wazanzibari wanapokuja Bara ni kwa ajili ya kutafuta maisha tu na hawajiingizi katika siasa na hata akitaka kufanya hivyo hatoruhusiwa kutokana na mtandao ulowekwa wa kuwapiga vita.Ukimuona Mzanzibari yumo katika siasa za Tanganyika ni katika ngazi ya Kitaifa kwa kupitia katika MUUNGANO.

Yako mengi yanayotukera kwa mfano utasikia nchi ya watu milioni 40 yenye eneo kubwa haiwezi kuilinganisha na watu milioni moja na yenye eneo dogo lakin munasahau kuwa hata inagalikuwa nii mtu mmoja na yenye ukubwa wa maili moja lakini ilikuwa na hadhi ya nchi na tulipoungana hatukukubali kuuza utu wetu kwenu.Sisi Wazanzibari tunaamini tuna haki sawa katika Muungano huu iwe katika kuchangia katika gharama za kuuendesha na katika faida yake.

Kama munaona munaonewa na hamna maslahi na MUUNGANO huu kwa nini hamtoi maoni ya kuurekebisha na kama haiwezekani kuuvunja tu moja kwa moja na mutafute koloni jengine la kutawala.
 
Kwani hapo nyumani ina maana Zanzibar ulikua mkoa? au prezdaa wao alikua
ceremonial president? or mkuu wa mkoa?
 
JOB WELLDONE 100%....
MAREKEBISHO GNU/SUK DONE DONE DONE AT 100%.....Yameshapitishwa Nothing to hide ,Zanzibar ZINDABAAD:becky: Tanganyika imefulia bwa ha ha ha machogo lazima mtajua kama embe ntunda :A S 100: Mkituita vibua muungano umekwisha :confused2:
 
Labda tuzungumzie matatizo yatakayo tupata watanganyika tukivunja muungano, pia faida tutakazo zipata tukivunja vivyo hivyo kwa upande wa Zanzibar. Mimi naona muungano uvunje, ili mtu wa bara akitaka kwenda Zanzibar atafute Visa kabisa, na Mzanzibar naye akitaka kuja huku naye ajiandae kwa masharti ya bara.

Hakuna kubabaishana, wala kulandamiza upande mmoja.
 
Hawawezi kurekebisha Katiba ya Muungano kwa kuifanya Zanzibar NCHI isipokuwa ni lazima wauvunje kwanza MUUNGANO wenyewe na kisha kuanzisha kitu kipya kwa kuafikiana na Bara. Muungano wetu unajieleza wazi kabisa na sijui kama hawa Baraza la Mapinduzi wamefikiria bara itaitwa kitu gani maanake tumekwisha liacha jina la Tanganyika na hawawezi kutulazimisha kurudisha jina hilo pasipo kuuvunja Muungano kwanza.
 
Tutake au mtake, tusitake au msitake, kwa marekebisho hayo Zanzibar imeshajitoa katika muungano. Kwanza wamedefine mipaka ya nchi ya zanzibar, pili yale madaraka aliyokuwa nayo rais wa jamhuri ya muungano kwa zanzibar yameondolewa kwa kiasi kikubwa, Mfano kuteua wakuu wa mikoa ambao kimsingi ndio wawakilishi wa rais wa jamhuri katika mikoa hiyo nk.
Niliwahi kuandika humu kuwa wazanzibar walianza zamani kudai kidogokidogo na kila walivyodai na kukataliwa walitishia kuvunja muungano; kauli hii ikawa silaha yao kubwa ya kupata kila walichohitaji. Katika mambo aliyokuwa anadai Abdu Jumbe, wamebakiza moja tu la sarafu. Nilieleza wazi kuwa sarafu bila kuwa na uchumi imara haisaidii - walipofika hapo wakaanza kudai mafuta nk. JK kwa kutojua ajenda yao ya siri akasema - lisiwape shida, linazungumzika!
sasa wameona wanacheleweshwa, wamepata mwanya, wameutumia.
Lazima tukae tuzungumze, muungano katika hali ya sasa ni usanii - irudi nchi ya tanganyika halafu nchi mbili ziungane kwa makubaliano mapya. Maji yameshamwagika, jaribio la kuyazoa litakumbana na matope pia.
Kutumia nguvu kulazimisha muungano uendelee katika hali ya sasa is unsustainable. Angalia nguvu ndogo ya kosovo - mahakama ya dunia imewatambua kama nchi, angalia eritrea - nguvu kubwa haikuwazuia kujitenga, angalia sudan -nguvu kbwa ya kijeshi ya sudan kaskazini haiazuia kusini kujitenga. Kutumia nguvu ni kukaribisha mauaji kama yale ya yugoslavia!
Nyerere alisema zitafutwe sababu za sasa za kuwa na muungano huu - ikiashiria kuwa zile za zamani zimepitwa na wakati!
Zanzibar siyo watoto wa kushindwa kujua athari na faida za kuvunja/kijuitoa katika muungano - wasing'ang'aniwe vinginevyo itaionekana madai yao kuwa wananyanyaswa ni ya kweli!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom