Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Katika kile kinachoonekana kuumwa na utaifa wao na shauku ya kujitegemea yenyewe nchi ya zanzibar ipo mbioni kuukwaa uwanachama wa shirikisho la vyama vya mpira wa miguu duniani (FIFA).
Hatua hiyo imekuja baada ya ujumbe mzito kutoka serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar,ukiongozwa na Naibu waziri kiongozi Mh. Ali Juma Shamhuna, kukutana na rais wa shirikisho hilo Bw. Seppt Blatter kama inavyoonekana pichani hapo chini.
Zanzibar, ikiwa ni moja ya nchi inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeshapata baraka zote kutoka kwa mshirika mwenzake katika Jamhuri hiyo, Tanganyika na FIFA haina kikwazo na hilo. Hatua hii ya Zanzibar iwapo itafanikiwa itakuwa mafanikio makubwa kwa Zanzibar kufunguwa milango ya kujitegemea na kujitangaza kimataifa.
Taarifa kutoka Zanzibar zinasema, wananchi wengi wamefurahishwa na kuunga mkono kwa dhati juhudi hizo za SMZ na kuahidi kuiunga mkono hadi mafanikio yapatikane.
Kwa mda mrefu Zanzibar imekuwa ikipigana kufa na kupona bila ya kukata tamaa kutafuta uwanachama wa shirikisho hilo ili iweze kuendeleza mchezo huo unaopendwa visiwani katika ngazi ya kimataifa.
Pichani Rais wa chama cha soka cha Zanzibar(ZFA) Bw. Ali Ferej Tamim kushoto, Naibu waziri kiongozi wa SMZ Bw. Ali Juma Shamhuna na Bw. Septt Blatter, rais wa FIFA, wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya mazungumzo ya kufanikisha mpango wa Zanzibar kuwa mwanachama wa shirikisho hilo mjini Zurich.