Zanzibar kutumia Sh. bilioni 445 bajeti ijayo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Mwinyi%20makame%20Z%289%29.jpg


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, (SMZ) imetangaza mwelekeo wa bajeti ya mwaka wa Fedha 2010/11 ambapo inatarajia kutumia Sh. bilioni 444.6 katika mwaka ujao wa Fedha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema kiwango hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika katika utekelezaji wa kazi za kawaida na mpango wa maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Aidha, alisema bajeti hiyo imelenga kumkomboa mwananchi kwa kuimarisha kilimo cha kisasa, makazi bora pamoja na kuimarisha huduma za kijamii kwa wananchi.

Alisema Serikali inatarajia kutumia Sh. bilioni 193.4 kwa kazi za kawaida na Sh. bilioni 251.2 kwa ajili ya utekelezaji mpango wa maendeleo wa Serikali.

Sh. bilioni 211.7 zinatarajiwa kupatikana kupitia misaada ya wahisani wakati Sh. bilioni 39.4 zitatokana na mapato ya ndani.

Hata hivyo alisema katika mwaka ujao wa Fedha Serikali inatarajia kutumia Sh. bilioni 82.4 kwa ajili ya malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma.

Aidha alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali inatarajia kukusanya mapato ya ndani ya Sh. bilioni 171.6 wakati Sh. bilioni 266.9 zinatarajiwa kupatikana kupitia misaada ya wahisani.


CHANZO: NIPASHE
 
Hebu wadau tuanzie hapo. Hii inashangaza kweli. Kati ya hizo mia 4, mia 2 zinatoka kwa wahisani. Inakuwaje nguvu za kimamlake watake ziwe sawa? Wajuzi tuwekeeni takwimu na data hapo ili twende sawa
 
Hebu wadau tuanzie hapo. Hii inashangaza kweli. Kati ya hizo mia 4, mia 2 zinatoka kwa wahisani. Inakuwaje nguvu za kimamlake watake ziwe sawa? Wajuzi tuwekeeni takwimu na data hapo ili twende sawa

Kuanzia hapo wapi? unaposhangaa wewe? twende sawa kutoka wapi kwenda wapi?
 
Back
Top Bottom