Wanabodi,
Msipokuwa na majibu sahihi ni bora kabisa kukaa kimya kuliko kukisia ama kuleta Ubishi usiokuwa na maana. Chenji ya Rada ni UFISADI mkubwa ulofanyika na hata kama zimegawiwa bara sielewi zimegawiwa vipi kiasi kwamba haya madai yawe na ukweli wowote. Rada ilinunuliwa kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni swala la Kitaifa na tumelipwa kwa jina la mfuko wa Taifa hivyo hata matumizi yake ni ya serikali ya Muungano.
Tatizo linalowakumba Wazanzibar wengi ni pale wanaposikia serikali ya Muungano basi lazima hiyo iwe inazungumzia bara tu, lakini wasichokifahamu ni kwamba Bunge la Taifa Dodoma linawashirikisha Wazanzibar, Utawala wa serikali yetu wamo Wazanzibar kwa manufaa ya pande zote mbili na hata ukitazama Kamati kuu ya chama tawala imejaa Wazanzibar - Huo mseto walounda Zanzibar majuzi unatumika Bara toka mwaka 1964 ktk serikali yetu ya muungano. Matumizi yote yanalipwa na kodi za wananchi wa pande mbili, Bara ikichangia zaidi kwa kila kitu. Sasa iweje fedha hizi zipelekwe ktk serikali ya (mseto) Mapinduzi wakati ni fedha za Muungano?..
Mkandara, hivi kwa mfano ukatokea wizi kwenye mji wa Mkandara, baada ya msako mali ikandulika iko wapi na kurudishwa nyumbani kwa Mkandara, lakini ndani ya huo mji mali ilikuwa ya Juma Mkandara na sio Juma na nduguye aitwaye Abadala. Sasa, Abdallah ana haki ya kupata kiasi cha mali hiyo iliyorudi hata kama huko nyuma hakushiriki kuinunua?
Swali la RADA liliulizwa bungeni na mwanasheria mkuu alifananua. Hata hivyo Rada ilinunuliwa na Jamhuri ya Tanzania (Mkandara) na hasa mtu aliyelipia ni Wizara ya Uchukuzi-Tanzania Bara (Juma Mkandara). Sasa chenji ya wizi imerudi, Abdallah anataka gawio! Wakati huo huo kumbuka ilinunuliwa na mkopo na hivyo mlipaji wa huo mkopo na Tanzania bara (Juma Mkandara). Kama Abdalla atataka gawio, hakuna shida lakini pia awe tayari kuchangia hela za kununua/mkopo.
Hii mambo mseto haibalishi equation.