Zanzibar Kumekucha

for your information karume alikuwa hautaki muungano kwa sababu alikuja kugundua kapigwa mchanga wa macho na nyerere..by the way hata mimi nataka muungano uvunjike hauna maana yoyote

Si kweli kwamba Karume hakupenda Muungano, Nyerere alipomuuliza Karume kama anataka waunganishe nchi au la akasema "niko tayari hata sasa!" Ndio maana hakujitoa kwenye huo Muungano na alikubali kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kwa muda wote alipokuwa hai! Tatizo la baadhi ya Wazenj wachukia Muungano na wabaguzi wanafikiri kwamba bila Muungano wataendelea sana na eti watakuwa "Dubai ya Afrika Mashariki!" Sijui ndoto hii itatimizwa kwa rasilimali zipi!
 
Muungano ukivunjika who is a looser?? wapemba wananunua mashamba Mbagala na Mkuranga kama vile wapo wete, Maduka ya kariakoo ni wapemba watupu, wachuuzi wa mchele pale Tandika ni wapemba, nenda shy wanunuzi wa mchele ni hao hao. Kwa upande mwingine, mtu wa bara ukiweka hata kioski cha soda zanzibar hakuna atakayenunua, achilia mbali ardhi ambayo hauwezi kupewa labda unywe kikombe cha babu. Jamaa hawaangalii mbali, wazanziba/pemba ni wakuzaliana sana, familia moja watoto sita, nane mpaka kumi, suala la global warming hawalioni kwao, ukubwa wa kisiwa chao unapungua siku hadi siku, sasa kisiwa kikimezwa watakwenda wapi?

Kwa maoni yangu binafsi, mbali na udungu tunaoutaka hasa watu wa bara kwa kifupi wao ndio wanaotunyonya tena kama kupe. Tumewapendelea sana sasa inaonekana tunajikomba ACHA WAVUNJE MUUNGANO WAO WENYEWE LITAKALOWATOKEA WAWE TAYARI KULIMEZA.
Kijana inaonesha upeo wako mdogo,hujui kuwa sababu ya kuwafanya wazanzibar kukimbia zanzibar ni properganda ya nyerere,walichofanya zanzibar kufitinisha kisiasa na kiukabila upemba na unguja,pia wakatumia nguvu za dola kuwapiga wananchi na hasa wafanya biashara ili wakimbie zanzbar na badala yake waje tanganyika,na azimia la kuja tanganyika waje kufanya biashara,pia waje kuchanganya damu eti tuwe watanzania.

Zaidi ya hayo aliyofanya nyerere,kutukomoa kimaisha,kuikandamiza zanzbar kiuchumi,unajua kuwa kabla ya muungano zanzbar ilikuwa na uchumi mzuri kuliko tanganyika ? Walichofanya nyerere aliiondolea zanzbar kiti cha umoja wa mataifa na account ya zanzibar huko ughaibuni katika bank kuu ya dunia kuzichukua na kuzitia katika mfuko wamuungano,tena zilikuwa pesa za kigani unajua hilo ?

Sisi kuishi tanganyika tulilazimika kwa sababu tunapokua zanzbar muungano unatuharasi sana ili tu move on huku bara ili muungano udumu,lakini wapi,asimilia ya wazanzibari walioko bara ni 1,asilimia99 ipo zanzibar hata tukuivunja hatuna hasara,hayo mashamba sio kitu kwetu,pia kuzaa watoto 9 ni majaaliwa kama hufahamu.

Sisi population yetu ni ndogo sana inaturuhusu tuzae hata 20 kila mtu,bado tunahitajiana,kwa hiyo kuwa respect,au unahasira na wazanzibari kakuchukulia dada yako,hehe pole kijana. ila kuwa be care free maneno ya kingwendu ajije akakubaka.
 
Nina imani hakuna mzanzibari yeyote asiyetaka muungano,kama yupo ni kwa maslahi yake mwenyewe na familia yake.vilevile naamini kabisa kuwa idadi ya wazanzibari waliohamia bara ni wengi kuliko walio zanzibar na kwa kuzaana hao wanajua,naamini kabisa kuwa wengi wa walioko zanzibar wanatamani kuhamia bara hapo wakipata nafasi tena jumla na familia zao.Naamini kabisa kuwa mahitaji muhimu hasa chakula,umeme wanategemea bara kwa 90% na hilo halitaepukika kwa miaka mingi ijayo.ANGALIZO:Hata ikipigwa kura ya maoni leo hakuna mzanzibari atakaye thubutu kusema NO TO MUUNGANO wachache wataweza.Lakini hata ardhi ipasuke haitawezekana kwa faida wanazopata katika huu muungano.ZIPO NYINGINE NYINGI ZA KISIASA AMBAZO MNAZIJUA NA NYINGINE ZA UPENDELEO MAALUM NYINGI SANA HADI ZINATUKERA WABARA lakini kwa faida yao tunanyamaza kuepuka malumbano.:bored::bored::bored:
 
Hamtokaa salama!! luv this one please watch it all! its' amazing stuff!!



huyu mzee hana mpya ...alikua dikteta na amecha wafuasi wake hapa ambao bado wana muabudu....Kama si huyu mzee Tanganyika ingekua mbali sana. Hebu tuangalieni Tanzania ni nchi ya ngapi kwa umasikini duniani pamoja na rasilimali zote zilizopo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom