'Zanzibar Kamwe Haitokua Mwanachama wa FIFA'

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
HATIMAYE Shirikisho la Soka la Kimataifa, (FIFA) limesema kamwe Zanzibar haiwezi kupata uanachama kutoka kwake na inalitambua Shirikisho la Soka Tanzania, TFF pekee.

FIFA imetoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ally Tamim Ferej kutangaza kuwa sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa mwanachama wa FIFA, jambo ambalo limezua mjadala mzito kwa jamii.

Awali, viongozi wa ZFA walitaka kuifikisha kortini TFF na ‘kuiharibia’ kwa FIFA wakidai kunyimwa mambo mengi ya maendeleo ya soka ikiwemo fedha zinazotolewa na shirikisho hilo la kimataifa.

Afisa Maendeleo wa Shirikisho hilo kwa Ukanda wa Kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salam jana kwamba FIFA ni chama mama katika nchi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake.

Mamelodi yuko nchini kwa siku nne kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya soka akifuatana na Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Elimu na Ufundi wa FIFA kutoka Zurich, Uswisi, Jurg Nepfer.

“Nashangaa Tenga (Rais wa TFF, Leodegar) analalamikiwa, hii siyo sahihi. Ukweli ni kwamba kupata uanachama FIFA, ni lazima nchi iwe inajitegemea na kutambulika kwa kila kitu, Zanzibar inapaswa kuwa nje ya Muungano wa Tanzania ndipo inaweza kupatiwa uanachama,” alisema Nepfer.

Alisema Zanzibar inachotakiwa kufanya ni kufanya kazi kwa ushirikiano na TFF ili iweze kufaidika nan misaada ya FIFA.

Alisema FIFA haiwezi kufanya chochote kile kuwapa Zanzibar uanachama kamili na wataendelea kuwa washiriki kupitia TFF.

Source: http://www.nifahamishe.com
 
Hivi mbona nchi zinazounda United Kingdom zina uwanachama wa moja kwa moja wa FIFA!!? Zanzibar si ina Rais wake! Kwanini isipewe! Naomba kuelimishwa hapo kidogo wakuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom