Inaweza kuzaliwa Zanzibar mpya. Mfano wanaweza kuunda selikari yao ya Muungano wa visiwa vya Pemba na Unguja. Selikari ya Pemba na Selikari ya unguja zikishughulika na mabo yao ya ndani na Selikari ya Muungano ikishughulikia mambo ya Muungano wao.
Pia maridhiano yanaweza kufanyika kwa raia watakaoamua kubaki kwa hiari yao katika sehemu mojawapo zilizokuwa zinaunda muungano uliovunjika. Tutakapoamua kutumia Busara au Jazba kakika kuvunja muungano ndivyo vitakavyoamu yale yatakayotokea siku ya kuvunjika kwa muungano. Montenegro walipiga kura kujitoa kwenye Muungano na Serbia, Serbia kwa shingo upande wakaamua kuwaruhusu lakini hawakuchukua hatua za kuwafukuza wamontenegro waliokuwa wanaishi serbia. Sana sana Serbia ilitafuta njia nyingine ya kuimarisha mahusiano na Montenegro na si kuendeleza uhasama. Hivyo hata kwa Tanganyika na Zanzibar kuna mambo mengi tunaweza kufaidishana baada kama muungano wetu tutauvunja kwa kufuata taratibu zinazotakiwa badala ya kutumia jazba, kujenga uhasama, n.k
Mkuu nakupa hongera kwa mawzo yako ya BUSARA na napenda kukutowa hofu kuwa hakuna mfarakano wowote kati ya Unguja na Pemba na kinachotokea ni kila mmoja kutumia haki yake ya Kidemokrasia.
Mgawanyiko wa kura ni jambo la kawaida chemgelecho Waswahili" Mtu haachi kutia tonge kwenye mdomo akatia puani" Na "Mcheza kwao hutunzzwa"
Ikiwa anaegombea nafasi ya uongozi anawakilisha matakwa yangu basi ni natural nitampigia kura na hicho ndicho kinachofanyika kule Pemba.