Pharaoh
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 843
- 157
FIKA ZANZIBAR UONE RUSHWA POPOTE NA MBAYA ZAIDI INAAMBATANA NA UBABE WA KIJINGA.
Natoa mifano michache tu, Airport kabla hujaingia ndani yupo mlanguni mzee mweupe mvaa kofia kama ustaadh vile, atakuuliza mambo kibao yahusuyo Afya halafu mara atakwambia ukae pembeni karibu na kijikona kwa upande wa kushoto, akikuingiza kwenye kakona hako lazima akutoe chochote la sivyo atakusumbua utakesha airport...
Ukitoka hapo kupewa begi lako lazima unyooshe mkono, mabegi yanajazana na wa kutoa haraka ndio wa kupewa mwanzo wengi mtasaga meno na joto la hapo mpaka mwisho.....
Ukipewa begi hapohapo unavutwa pembeni wa wapakuaji kwa kizingizio cha vitu haramu, hapo ndipo pagumu, watakuingiza kwenye chumba chao na wapo polisi pia, watafungua na kukuvurugia vitu vyote na kuvitoa nje ya mabegi kabla ya kuanza kukuhoji na hapo usije ukanuna umekwisha manake wa njama na polisi wa airport mi nimeshuhudia kijana mwanafunzi wa mzanzibari aliyerudi toka india akilia kama mtoto mimi nilizama mfukoni haraka na sijajifanya najua.
Kabla hujafika mjini toka airport kuna uwezekano wa kuwakutana matrafiki mara 4, andaa bajeti ya kupita.
Ukifika mjini kuna wafanyakazi wa kamisheni ya utalii wakishirikiana na polisi hao wanamtafuta mtu yeyote mjini anaongea au kuongozana na mzungu, watakunyanyasa wewe vibaya ili huyo mzungu akukombowe kwa pesa na wanaanzia dola 500, watakusingizia unafanya kazi ya utembezaji wageni bila kibali (tour guide) hawasikii chochote manake wanakuja wameshanuna na lolote utakalosema watakujibu unanifundisha kazi? hata awe mkeo, girlfriend, business partner, marafiki wa zamani. itaendelea