Zanzibar inastahili kuwa na wajumbe wawili tu katika tume ya katiba

Alex manonga

1. ya zanzibar teyari imeundwa ya watanganyika itaundwa lini kama hii ni ya muungano?
2. Ya muungano inahusisa wazenji na watanganyika Je itakayojari haki za watanganyika kama ile ya wazenji ipo wapi?
 
Lazima ifahamike kwamba kama watanganyika tunamambo yetu ambayo tusingependa wazenji waingie kujadili na tutayajadili wapi kama ilvyo kwa wazenji wanamiliki yao:-

1. wanakatiba yao (Yao kama zanzibar kwa maslahi ya wazanzibar tu)
2. wanabunge lao (la wazanzibari tu hakuna mtanganyika)
3. wanaserikali yao ( ya wazanzibari tu hakuna mtanganyika kuingiza walau pua yake)
4. wana viongozi wao (wazanzibari tu hakuna watanganyika kushiriki kuongoza zanzibar)
5.Wana rais wao nk ...............

Popote tuwapo watanganyika lazima wazibari washiriki lakini wanapokuwa wazanzibari watanganyika hawatakiwi , Ni uhusiano gani huu au ushikiano gani? Parastism mode of relation or ............

1. Katika bunge la tanzania wao wamo
2. serikali ya Tanzania wao wamo
3. mahakama za tanzani wao wamo

Ni bora tuwe na serikali tatu

1. serikali ya tanganyika kwa watanganyika na maslahi ya vizazi vyao
2. serikali ya zanzibari kwa wazanzibari na maslahi ya vizazi vyao
3. serikali ya muungano ambayo itakuwa ikiwakilishwa na watanganyika wa tanganyika na wazanzibari wa zanzibar kwa mujibu wa utaratibu na muundo utakaokubalika na pande zote mbili. Sio huu wa sasa wa kijinga na kipuuzi kwa maslahi ya wazanzibar peke yao.

Watanganyika tumechoka kupuuzwa na kunyanyaswa huku mali, ajira na tawala zetu zikiwafaidi wazenji pekee ndani ya muungano.
 
ZANZIBAR ni nchi na itaendelea kuwa nchi. Nani alikwambieni muiue Tanganyika. Mwenye wivu ajinyoge. Mtabaki kulia tu Wadanganyika. Kelele za mlango.........................
 
ZANZIBAR ni nchi na itaendelea kuwa nchi. Nani alikwambieni muiue Tanganyika. Mwenye wivu ajinyoge. Mtabaki kulia tu Wadanganyika. Kelele za mlango.........................

wadanganyika kwa taarifa yako wanaishia(wazee akina kingunge na wale wote wenye umri wake) hiki ni kizazi kingine ni watanganyika-ndo kwanza wanashika madaraka na muda si mrefu utawapokea viongozi na wagunge kutoka zenji waliopewa ajira na watanganyika.

Isitoshe watanganyika ni wapole wapenda amani na siku zote wanapenda kuheshimu jirani zake na kushirikiana nao hususan ninyi wazenji. Lakini kidomodomo chenu kimetuchosha kama huamini miaka michache ijayo utapata majibu.
 
Alex manonga

1. ya zanzibar teyari imeundwa ya watanganyika itaundwa lini kama hii ni ya muungano?
2. Ya muungano inahusisa wazenji na watanganyika Je itakayojari haki za watanganyika kama ile ya wazenji ipo wapi?
Tanganyika ilizikwa 1964 na kuridhiwa na serikali ya muungano inayojumuisha Wazanzibari. Kisheria Wazanzibari wana haki ya kushiriki katiba ya muungano kwa sababu inawahusu. Kwa busara ya kawaida unaweza kusema wengi wanastahili kupewa fursa zaidi lakini kidiplomasia nchi zote zinakuwa na haki sawa katika uamuzi, Tanzania ni matokeo ya uamuzi wa nchi mbili kuungana.
 
Baada ya kusoma nakala ndefu hii, sinabudi kusema kuwa , ni kweli kuwa huu muungano haufahamiki. Nasikitika kuwa mwandishi amechukulia kuwadharau wazanzibari kwa kuwa kijinchi chao hakina mpango wowote kwa kuwa ni padogo halafu pia population yake ni ndogo sana. Mimi nashindwa kumuelewa sababu inaonekana wazi kuwa ni limbukeni wa mambo.
Senegal na gambia walitaka kuunganisha nchi zao. Nenda kwenye ramani ya dunia uione senegal na gambia ziko vipi. Na katika makubaliano yao waliitisha referendum na kupeana miaka mitano wananchi wao kuamua. Wagambia walikataa. Mbona haikuwa noma. Singapore na Malaysia pia walikuwa na muungano na nchi zote hizi angalia maeneo yao. Leo imekuwa kioja Zanzibar?????.
Sisi wazanzibari tumeungana na Tanganyika, ziko wapi nakala za muungano?. Ziko wapi sheria zilizofuatwa kuunganisha nchi?. Leo Mh. Kikwete kuitisha katiba mpya ni katika kutaka kuhalalisha muungano lakini kama ulivojijibu mwenyewe, itapigwa na chini sababu wazanzibari hawatakai tena kutawaliwa.
Kejeli zenu na dharau juu ya wazanzibari munazionyesha kila wakati munaposhika kalamu mukiandika. Mimi nawaombea CHADEMA mushinde kura muuvunje muungano tukae kwa kuheshimiana na sio kuburuzana na kudharauliana. Sisi tumechoshwa na muungano bandia. Muungano FEKI.
 
Manonga na wenye mtazamo wako

Ungekuwa jaji unasemaje kuhusu muundo wa serikali za nchi mbili kuzaa serikali moja kwa nchi zote mbili huku moja ikibakiwa naserikali yake ndani kwa ndani?


katika muundo huo unadhani maslahi ya muungano yaliwekwa kuilinda zanzibar kwa hofu iliyofichika au ilizingatia demokrasi huru kwa maana ya usawa kimuundo ? (serikali tatu)

kuzikwa kwa tanganyika kulitokana na mtazamo chanya wa mwal nyelele na A. Aman Karume, kwa bahati mbaya viongozi vilaza wa wakati huu hasa wazanzibar wamekosa staha, wamekuwa wabinafsi, wakitaka kila kitu kutoka T bara, wenyekupayuka na wasio na subira.

Ni kutokana na vurugu hizi nadhani kulikuwa na makosa ya kimuundo wa muungano. Watanganyika tunahaki kujadili baadhi ya mambo yetu bila ya kuigiliwa au uwepo wa wazanzibari. Bali tushirikishane kwenye yale mambo yanayohusu muungano pekee.

Sio sahihi pale zito akihoji huduma kwa wapiga kura wake wanzibar wakishiriki lakini mbunge wa bububu au mkanyageni anapohoji katika bunge la wawakilishi zito, mnyika au zambi hawapo, hakuna mantiki hapa.

Na hili la uwakilishi wa 50% kwa 50% linatoka wapi? kisheria, kibiashara na kimahesabu ukichangia mtaji kwa 20% na mwezio 80% ni wazi gawio la faida litafuata utaratibu huo huo wa 20% kwa 80% sio 50-50. sasa ya watu mil 1.5 na watu mil 40 uwakilish wa 50-50 unatoka wapi ilhali huko zenji hapakuwa walau na uwakilishi wa at least 1% kutoka T bara?

Hapa ndipo wanasisa wetu au wanadiplomasia wanapaswa kurejea darasani kujifunza upya, na muungano kwa kasoro hizi ndo unakufa ni sualana muda tu. Tutachangia sana kwa ushabiki lakini ukweli utabakia kuwa muundo wa muungano ni mbovu hakubaliki.
 
Kwanza kwanini wameshilikishwa ile hali washasema hawataki muungano.Umefika wakati wa Tanganyika kuwa na serikali yake.
 
Mimi moni yangu ni kuwa huu Muungano ufe. Hauna tija tena. Uzuri ni kuwa wa-Zanzibar na wa-Tanganyika wote hawautaki tena Muungano huo. Watetezi wa Muungano huo ni viongozi ambao wanajinufaisha na raslimali za Tanganyika.

Sheria haina nguvu kuliko uhalisia. Sheria ya Muungano haiwezi kuwa nzuri kwa kulinda dhulma na ufisadi wa kundi dogo la watu katika jamhuri. Nchi ya watu 900,000 na nchi yenye watu 43,0000,0000 haziwezi kuwakilishwa na idadi sawa kwenye Tume ya Katiba. Kwanini idadi ya wajumbe iwe sawa? Mbona idadi ya raia wa nchi hizo mbili haziko sawa? Mbona idadi ya wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano hailingani na ile ya Tanganyika?

Kikwete akituburuza patachimbika...hata sisi wanajeshi tutaingilia kati kusawazisha mambo...tunafuatilia kwa makini sana mambo yote
 
Back
Top Bottom