Zanzibar inastahili kuwa na wajumbe wawili tu katika tume ya katiba

..Zanzibar ....mchango wao kwenye uchumi wa Taifa (GNP) ni chini ya 2%. Hivyo ndiyo vigezo vingechukuliwa.
Na mimi ninakuunga mkono kwa hoja yako hii lakini, ikiwa tutachukua kigezo cha mchango wa eneo la TZ kwenye uchumi wa taifa (GNP), je mikoa ya TZBara inayochangia asilimia kubwa zaidi katika GNP inapaswa kuwa na wajumbe wengi zaidi katika tume? Mikoa hiyo ikia kulalamika tutakimbilia kigezo gani?
 
Mimi naamini kuna siri kubwa ndani ya muungano huu na nijambo la msingi ikiwa mkataba wa muungano wenyewe ukawekwa wazi ili kila Mtanzania auelewe.Najaribu kujiuliza hivi Nyerere na Karume walikuwa hamnazo kuukubali......?? na je ni mambo gani walikubaliana....??? na ilikuwaje wadau wakuu ambao ni wananchi kutoshirikishwa...???
 
Watu wawili wanatosha kuwakilisha maoni ya watu milioni mbili, na watu 28 wanatosha kuwakilisha maoni ya watu milioni 40. Kumbuka kwamba tume ya katiba inakusanya maoni pia kwa mambo ambayo siyo ya muungano. Hivyo, Tanzania bara inahitaji kuwa na watu wengi na wachache kwa Zanzibar kwa kufuata uwiano wa idadi ya watu.

Si sahihi wazanzibar kuwaamulia watu wa Tanzania bara katiba yao wakati Tanzania bara haikuhusika katika kuandaa katiba ya Zanzibzar

Hapo nakuunga mkono mkuu! Basi kama wanasema wanataka idadi sawa ya uwakilishi kwenye tume ya kukusanya maoni ya katiba ya muungano, basi ingeundwa tume nyingine ya kukusanya maoni wa watu wa Tanzania bar, ambapo wao wajumbe wa zenji hawatasemea chochote kuhusu maoni ya tanzania bara kama sisi tulivyokaa kimya kuhusu marekebisho ya katiba ya Tanzania visiwani. Ila sasa tatizo ni kwamba hakuna serikali ya Tanzania bara wala katiba.

Sisi tumechanganywa kwenye muungano wakati wazenji kuna mambo wanajitegemea. Hii sio haki kwetu wa TZ bara! Na sina uhakika na hii tume kama tukisema tunahitaji serikali tatu watakubaliana, coz wajumbe wa TZ visiwani wakipinga basi hatuna letu coz wana mamlaka sawa kwenye tume na wa Tz bara. Hii ni kiini macho tumechezewa watz bara
 
a. Unasumbuliwa na UDINI kama wa mzee Mtei

b. Chadema walienda kumwona JK wakanywa juice wenye akili tukawauliza kitu gani kimebadilika kwenye muswada kabla na baada ya mkutano wenu ikulu? tukaambulia matusi? (walaumu chadema kama utaweza)

c. Zanzibar ni nchi kamili (irrespective of number of people); katiba inayoandikiwa na ya nchi mbili Tanganyika na Zanzibar ...uwiano huo ni halali kwa mujibu wa sheria.

Shiriki katika mchakato wa katiba mpya acha kulalama kama mtoto mdogo poor you
 
vijana_kura_ya_maoni-564x272.jpg
Pata ujumbe: kwa hisani ya Mzalendo.net
Nyie endeleeni kubishana tu wadanganyika, sisi tunafanya action!
 
Haya maajabu,zenji wana bunge lao,wana bendera yao,wana wimbo wao wa taifa wana rais wao.bado wanakatiba yao Na ktk yote hayo Tanganyika hawajatuhusisha kwa lolote.sasa ni vp sisi tuwahusishe ktk ktb yetu,kuwe na katiba ya tanganyika then tuwe ktb ya jmt au sio,,,,ni hayo2.
 
Idadi kubwa ya wazanzibari ni doa kubwa ambalo litasababisha kukataliwa kwa katiba mpya itakayoundwa. Zanzibar ilitakiwa iwe na wawakilishi wawili tu (2) ukizingatia uwiano wa idadi ya watu Tanzania bara na Tanzania visiwani.

Hivi sasa Tanzania bara kuna idadi inayokaribia watu milioni arobaini (40,000,000) wakati Tanzania visiwani ina watu karibia milioni mbili (2,000,000). Ukichanganya idadi ya watu wa Tanzania bara na Zanzibar jumla ni watu milioni arobaini na mbili (42,000,000).

Kwa idadi hii ya watu, uwiano wa idadi ya watu kwa Tanzania visiwani ni asilimia tano tu (5%), wakati Tanzania bara ni asilimia tisini na tano (95%). Asilimia tano ya watu 30 katika tume ni watu wawili, wakati asilimia 95% ya watu 30 ni watu 28. Kwa hiyo Zanzibar ilitakiwa iwe na watu wawili tu katika tume wakati Tanzania bara ilitakiwa iwe na watu 28.

Sasa, siyo sawa Zanzibar kuwa na idadi kubwa ya wajumbe katika tume ya katiba. Maana Wanzabari wanawatungia katiba Tanzania bara wakati Tanzania bara hawakushiriki kutengeneza katiba ya Tanzanaia visiwani.

Upungufu huu ulishaonyeshwa na Msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu machakato wa katiba mpya. Hapa chini ninawasilisha sehemu ya hoja ya kambi rasmi ya upinzani bungeni iliyowasilishwa na Tundu Lisu inayoonyesha kuwa Zanzibari wamepewa madaraka makubwa sana katika kuandaa katiba ya muungano, hasa ilizingatiwa Wanzanibar watashiriki kuamua mambo ya Tanzania bara hata ambayo siyo ya muungano.

‘’NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR

Mheshimiwa Spika, Muswada unapendekeza kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa ‘mashauriano na makubaliano’ na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwa mfano, ibara ya 5 inayohusu kuundwa kwa Tume inamtaka Rais ‘kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Vile vile, ibara ya 6(1) inayohusu uteuzi wa wajumbe wa Tume; ibara ya 8(1) na (2) inayohusu hadidu za rejea na kuongeza muda wa Tume; na ibara ya 13(2) inayohusu uteuzi wa Katibu wa Tume, zote zinataka kuwepo na makubaliano na Rais wa Zanzibar. Aidha, ibara ya 13(5) inayohusu uteuzi wa watendaji wengine wa Tume inalazimu makubaliano kati ya Waziri na Waziri mwenzake wa Zanzibar ambao nao ni wateuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar.


Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar.

Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar, “... atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba.”

Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya.

Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba!
Mheshimiwa Spika, Mapendekezo haya yanaashiria kuwepo kwa mtazamo ambao chanzo chake ni Makubaliano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ya tarehe 25 Aprili 1964.

Kwa mtazamo huo, Zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kwa hiyo ni lazima sio tu ishirikishwe kwa usawa, bali pia lazima ikubaliane na mabadiliko yoyote ya kikatiba yanayopendekezwa na Muswada.

Kama Profesa Palamagamba Kabudi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alivyosema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika tarehe 12 Novemba 2011: ‘Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.’
Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mtazamo huu sio sahihi.

Kwanza kabisa, Zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa Hati za Muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya Katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu Muungano kama vile Katiba ya Tanzania yamekasimiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa Tanganyika.

Masuala haya ya Muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na Muungano huo!

Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa Muungano bila kwanza kuirudisha Tanganyika kama nchi na bila kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya Muungano!’’



kwani ni nani aliyetaka uwepo huu muungano huko nyuma??? na kwa nini watanganyika wanakubali nchi yao ya Tanganyika ife?

MLALAMIKIENI PENGO ANAYESEMA MUUNGANO USICHOKONOLEWE
 
a. Unasumbuliwa na UDINI kama wa mzee Mtei

b. Chadema walienda kumwona JK wakanywa juice wenye akili tukawauliza kitu gani kimebadilika kwenye muswada kabla na baada ya mkutano wenu ikulu? tukaambulia matusi? (walaumu chadema kama utaweza)

c. Zanzibar ni nchi kamili (irrespective of number of people); katiba inayoandikiwa na ya nchi mbili Tanganyika na Zanzibar ...uwiano huo ni halali kwa mujibu wa sheria.

Shiriki katika mchakato wa katiba mpya acha kulalama kama mtoto mdogo poor you

mtei hana udini peke yake na uchaga umemvaa na ndio nyerere akamfukuza haraka kwani hakuweza kuficha makucha yake
 
Wimbo wa Taifa za Zanzibar.

Mungu ametubarikia,
Unguja na Pemba yote.
Sote tunashangiria jamhuri kutuletea,
Mungu ametubarikia unguja na pemba yote
.
 
Binafsi sioni kabisa hii haja ya huu muungano,make ni kama tunalazimisha vile!! Dawa ya haya yote uvunjwe tu,potelea mbali acha wajitegemee na sie tuipate Tanganyika yetu ilio potea!!! Ni cha kushangaza viongoz wetu hawalitambui kabisa hili,ama kuna maslahi binafsi hapo??
 
Sisi wacha tujipange kutoa maoni yetu kuhusu katiba nyie endeleeni kuwaza utumbo wenu na mawazo yenu ya kidini
 
Kwa kweli Wabara tunapelekwa na wazenji, halafu viongozi wetu wanawaogopa, kila watakalosema wazenji it is ok to them, jamani wabara tusikubali upuuzi huu. na katiba siyo mali ya CCM lazima kwanza wabunge wa CCM waelimishwe ili wasiwe na ushabiki ambao haunatija kwa wabara.
 
Kwanza kabisa, Zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa Hati za Muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya Katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu Muungano kama vile Katiba ya Tanzania yamekasimiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa Tanganyika.

Masuala haya ya Muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na Muungano huo!

Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa Muungano bila kwanza kuirudisha Tanganyika kama nchi na bila kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya Muungano!''

Nimeipenda sana hii!!!
 
Kwa kweli Wabara tunapelekwa na wazenji, halafu viongozi wetu wanawaogopa, kila watakalosema wazenji it is ok to them, jamani wabara tusikubali upuuzi huu. na katiba siyo mali ya CCM lazima kwanza wabunge wa CCM waelimishwe ili wasiwe na ushabiki ambao haunatija kwa wabara.
Wabunge wa CCM wanawaza ki-CCM, kifisadi, hawana uchungu na Tanzania. Ila kwa hili hapatoshi kama marekebisho ya tume hayatafanyika haraka.
 
Sisi wacha tujipange kutoa maoni yetu kuhusu katiba nyie endeleeni kuwaza utumbo wenu
Haya ni maoni pia, na ndiyo haya tutakayotoa. Zoezi la kukusanya maoni lisiendelee mpaka idadi ya Wazanzibar kwenye tume ipunguzwe hadi wajumbe wawili tu ili iwiane na idadi ya watu wa pande mbili hizi za muungano.
 
Back
Top Bottom