Zanzibar inastahili kuwa na wajumbe wawili tu katika tume ya katiba

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Idadi kubwa ya wazanzibari ni doa kubwa ambalo litasababisha kukataliwa kwa katiba mpya itakayoundwa. Zanzibar ilitakiwa iwe na wawakilishi wawili tu (2) ukizingatia uwiano wa idadi ya watu Tanzania bara na Tanzania visiwani.

Hivi sasa Tanzania bara kuna idadi inayokaribia watu milioni arobaini (40,000,000) wakati Tanzania visiwani ina watu karibia milioni mbili (2,000,000). Ukichanganya idadi ya watu wa Tanzania bara na Zanzibar jumla ni watu milioni arobaini na mbili (42,000,000).

Kwa idadi hii ya watu, uwiano wa idadi ya watu kwa Tanzania visiwani ni asilimia tano tu (5%), wakati Tanzania bara ni asilimia tisini na tano (95%). Asilimia tano ya watu 30 katika tume ni watu wawili, wakati asilimia 95% ya watu 30 ni watu 28. Kwa hiyo Zanzibar ilitakiwa iwe na watu wawili tu katika tume wakati Tanzania bara ilitakiwa iwe na watu 28.

Sasa, siyo sawa Zanzibar kuwa na idadi kubwa ya wajumbe katika tume ya katiba. Maana Wanzabari wanawatungia katiba Tanzania bara wakati Tanzania bara hawakushiriki kutengeneza katiba ya Tanzanaia visiwani.

Upungufu huu ulishaonyeshwa na Msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu machakato wa katiba mpya. Hapa chini ninawasilisha sehemu ya hoja ya kambi rasmi ya upinzani bungeni iliyowasilishwa na Tundu Lisu inayoonyesha kuwa Zanzibari wamepewa madaraka makubwa sana katika kuandaa katiba ya muungano, hasa ilizingatiwa Wanzanibar watashiriki kuamua mambo ya Tanzania bara hata ambayo siyo ya muungano.

''NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR

Mheshimiwa Spika, Muswada unapendekeza kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa ‘mashauriano na makubaliano' na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwa mfano, ibara ya 5 inayohusu kuundwa kwa Tume inamtaka Rais ‘kushauriana na kukubaliana' na Rais wa Zanzibar na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Vile vile, ibara ya 6(1) inayohusu uteuzi wa wajumbe wa Tume; ibara ya 8(1) na (2) inayohusu hadidu za rejea na kuongeza muda wa Tume; na ibara ya 13(2) inayohusu uteuzi wa Katibu wa Tume, zote zinataka kuwepo na makubaliano na Rais wa Zanzibar. Aidha, ibara ya 13(5) inayohusu uteuzi wa watendaji wengine wa Tume inalazimu makubaliano kati ya Waziri na Waziri mwenzake wa Zanzibar ambao nao ni wateuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar.

Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar.

Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana' na Rais wa Zanzibar, "... atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba."

Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya.

Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba!
Mheshimiwa Spika, Mapendekezo haya yanaashiria kuwepo kwa mtazamo ambao chanzo chake ni Makubaliano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ya tarehe 25 Aprili 1964.

Kwa mtazamo huo, Zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kwa hiyo ni lazima sio tu ishirikishwe kwa usawa, bali pia lazima ikubaliane na mabadiliko yoyote ya kikatiba yanayopendekezwa na Muswada.

Kama Profesa Palamagamba Kabudi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alivyosema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika tarehe 12 Novemba 2011: ‘Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.'
Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mtazamo huu sio sahihi.

Kwanza kabisa, Zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa Hati za Muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya Katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu Muungano kama vile Katiba ya Tanzania yamekasimiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa Tanganyika.

Masuala haya ya Muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na Muungano huo!

Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa Muungano bila kwanza kuirudisha Tanganyika kama nchi na bila kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya Muungano!''

Kwanini tusipige kura ya maoni kuhusu muungano???hivi ni kweli Tanganyika na Zanzibar ni sawa??? Mi sijui viongozi wetu wanatupeleka wapi??? Tunahitaji mabadiliko katika nchi yetu,hatuwezi kuona wazanzibar wanabebewa tuu wakati wana nchi yao???
 
Huu muungano una umuhimu gani kwetu sisi watanganyika?Tunanyonywa mno na hao wazenji.Katiba inayoundwa ni ya watanganyika, inawahusu nini hao wazenji?
 
Hapo kuna kinakitu chini ya pazia,haiwezekani na haingii akilini eti nchi yenye watu ml2 iende sawa na nchi ya watu ml40.Z'BAR WANAMAUJANJA KULIKO MAZEZETA TULIOWAPA ZAMANA YA KUTUONGOZA HAPA BARA,bora kuwe na serikari tatu.
 
Mkekuu,

Zanzibar ina watu milioni moja,Tanzania bara milioni 42.

Ndugu mtoa mada ulipaswa ujue kwanza nn madhumuni ya marekebisho ya katiba ya muungano. Baada ya hapo ulipaswa kujua nn muungano wa jamuhuri ya tanzania na baadae ndio uandike thread yako. Elewa kwamba katika marekebisho ya katiba ya muungano na sio tanganyika kama mchangiaji mmoja alivyochangia katika marekebisho hayo kikubwa kunacho angaliwa ni uwakilishi wa maoni kutoka pande zote mbili za muungano yaani zanzibar na tanganyika kwa lugha nyengine tanzania bara na visiwani na wala sio tanzania zanzibar jee ni umuhimu gani ya kuwa na wajumbe sawa hapa tumazungumzia tume iliyohuru itayoshighulikia mchakato mzima wa kupatikana katiba mpya ya muungano na wala sio katiba ya tanganyika wala zanzibar, tume hii majukumu yake yametajwa ndugu mtoa mada tafadhali pitia kwenye rasimu ya tume ya mabadiliko ya muungano. Yatayoamuliwa utakuwa yameamuliwa na ndio utakuwa msimamo wa tume kwa maana fupi huo ndio utaokuwa ndio msimamo wa tanganyika na zanzibar nje ya muungano. Swali liko hapo ingekuwa tume hio wajumbe hawako sawa pande moja wapo ingepiga kelele kuwa idadi ya uwakilishi wake ulikuwa mdogo na ndio ikatokea matokeo hayo sasa wataalamu na serekali zote mbili ile ya visiwani na ile ya muungano vikakubaliana wawe na wajumbe sawa kutoka pande mbili za muungano ili kuondosha migogano ya maamuzi. Ushauri tugekuwa na serikali 3 hili lisingejitokeza na pili kesa lilifanyika pale waasisi wa muungano kuiua tanganyika leo hii wazanzibar wana katiba yao ya watanganyika iko wapi watanganyika wakitaka kubadilisha katiba watabafilisha katiba ya muungano ambayo ndani yake wazanzibar wamo humo. Ndugu watanzania tume sio itayotueleza muskbali ya tanzania yetu bali sisi wenyewe watanzania bara na visiwani ndio tutaokuwa waamuzi wa muungano wetu uweje kwa hio kila tunaloliona kero tuliweke wakati ukifika tulitaje na kwa tume hii iliyoundwa ni tiifu kwani ukiangalia kwa udani wa wakumbe kila mjumbe anamrengo wake kwa hio nawe mwananchi ungana na mrengo wa mjumbe unaemkubali hakika utashida tu
 
Wale watu wa Zanzibar idadi yao ni sawa na Temeke, mchango wao kwenye uchumi wa Taifa (GNP) ni chini ya 2%. Hivyo ndiyo vigezo vingechukuliwa na naunga mkono hoja kwa asilimia 100 kwa vile kinyume chake ni kwamba mstakabali wa watu 42 Milioni unaamuliwa na watu 1.2 Milioni walioko Pemba na Unguja. Huu ni uchuro, bora muungano usiweko kabisa.
 
Tatizo ni kuwa Zanzibar inachukuliwa kama nchi wakati ni sehemu ya muungano. Kwa kuwa Tanganyika siyo nchi vilevile Zanzibar siyo nchi. Hivyo uwakilishi wa tume ulitakiwa kuzingatia uwiano wa watu kwa kila upande wa muungano
 
Ndugu mtoa mada ulipaswa ujue kwanza nn madhumuni ya marekebisho ya katiba ya muungano. Baada ya hapo ulipaswa kujua nn muungano wa jamuhuri ya tanzania na baadae ndio uandike thread yako. Elewa kwamba katika marekebisho ya katiba ya muungano na sio tanganyika kama mchangiaji mmoja alivyochangia katika marekebisho hayo kikubwa kunacho angaliwa ni uwakilishi wa maoni kutoka pande zote mbili za muungano yaani zanzibar na tanganyika kwa lugha nyengine tanzania bara na visiwani na wala sio tanzania zanzibar jee ni umuhimu gani ya kuwa na wajumbe sawa hapa tumazungumzia tume iliyohuru itayoshighulikia mchakato mzima wa kupatikana katiba mpya ya muungano na wala sio katiba ya tanganyika wala zanzibar, tume hii majukumu yake yametajwa ndugu mtoa mada tafadhali pitia kwenye rasimu ya tume ya mabadiliko ya muungano. Yatayoamuliwa utakuwa yameamuliwa na ndio utakuwa msimamo wa tume kwa maana fupi huo ndio utaokuwa ndio msimamo wa tanganyika na zanzibar nje ya muungano. Swali liko hapo ingekuwa tume hio wajumbe hawako sawa pande moja wapo ingepiga kelele kuwa idadi ya uwakilishi wake ulikuwa mdogo na ndio ikatokea matokeo hayo sasa wataalamu na serekali zote mbili ile ya visiwani na ile ya muungano vikakubaliana wawe na wajumbe sawa kutoka pande mbili za muungano ili kuondosha migogano ya maamuzi. Ushauri tugekuwa na serikali 3 hili lisingejitokeza na pili kesa lilifanyika pale waasisi wa muungano kuiua tanganyika leo hii wazanzibar wana katiba yao ya watanganyika iko wapi watanganyika wakitaka kubadilisha katiba watabafilisha katiba ya muungano ambayo ndani yake wazanzibar wamo humo. Ndugu watanzania tume sio itayotueleza muskbali ya tanzania yetu bali sisi wenyewe watanzania bara na visiwani ndio tutaokuwa waamuzi wa muungano wetu uweje kwa hio kila tunaloliona kero tuliweke wakati ukifika tulitaje na kwa tume hii iliyoundwa ni tiifu kwani ukiangalia kwa udani wa wakumbe kila mjumbe anamrengo wake kwa hio nawe mwananchi ungana na mrengo wa mjumbe unaemkubali hakika utashida tu
Watu wawili wanatosha kuwakilisha maoni ya watu milioni mbili, na watu 28 wanatosha kuwakilisha maoni ya watu milioni 40. Kumbuka kwamba tume ya katiba inakusanya maoni pia kwa mambo ambayo siyo ya muungano. Hivyo, Tanzania bara inahitaji kuwa na watu wengi na wachache kwa Zanzibar kwa kufuata uwiano wa idadi ya watu. Si sahihi wazanzibar kuwaamulia watu wa Tanzania bara katiba yao wakati Tanzania bara haikuhusika katika kuandaa katiba ya Zanzibzar
 
Wale watu wa Zanzibar idadi yao ni sawa na Temeke, mchango wao kwenye uchumi wa Taifa (GNP) ni chini ya 2%. Hivyo ndiyo vigezo vingechukuliwa na naunga mkono hoja kwa asilimia 100 kwa vile kinyume chake ni kwamba mstakabali wa watu 42 Milioni unaamuliwa na watu 1.2 Milioni walioko Pemba na Unguja. Huu ni uchuro, bora muungano usiweko kabisa.

Ni uchuro kweli na Katiba itakayotokana na mchakato huo wa katiba ya Tanzania bara kuamiliwa na wazanzibar haiwezi kukubalika kamwe na watu wa Tanzania bara.
 
Mkekuu,

Zanzibar ina watu milioni moja,Tanzania bara milioni 42.

Baada ya sensa watu hongezeka. Nimeweka kadirio la juu kwa watu wa Zanzibar ili kusiwepo na lawama kuwa idadi yao imepunguzwa.
 
Inaumiza sana kuwa na viongozi ambao hawana upeo mpana wa kufikiri,ndio maana wazenji wanapata jeuri ya kuwafanyia wabara mambo mabaya na kuwaona kama hawana haki,lakini wakija huku bara wanajiona wanahaki na kila kitu,wazenji acheni roho mbaya naamini siku wabara wakicharuka sijui itakuwaje?
 
Hapo kuna kinakitu chini ya pazia,haiwezekani na haingii akilini eti nchi yenye watu ml2 iende sawa na nchi ya watu ml40.Z'BAR WANAMAUJANJA KULIKO MAZEZETA TULIOWAPA ZAMANA YA KUTUONGOZA HAPA BARA,bora kuwe na serikari tatu.

Hapa hakubali mtu. Tume ya namna hii haikubaliki na chochote kitakachoamuliwa na idadi kubwa ya Wanzibar katika tume hakiwezi kukubalika Tanzania bara.
 
Kwanini tusipige kura ya maoni kuhusu muungano???hivi ni kweli Tanganyika na Zanzibar ni sawa??? Mi sijui viongozi wetu wanatupeleka wapi??? Tunahitaji mabadiliko katika nchi yetu,hatuwezi kuona wazanzibar wanabebewa tuu wakati wana nchi yao???

Tatizo la wabunge wetu hawaangalii masilahi ya Tanzania bara. Hapa katiba bado kabisa kwa mwendo huu. Kwa nini Tanzania bara watungiwe katiba na Wanzazibar? Haiwezekani, Tanzania bara inahitaji kujitungia katiba yake yenyewe na siyo vinginevyo.
 
Mtate msitake,
Hiyo ndio tume imeundwa kisheria!
na imepata baraka za kisheria.
Kelele zenu hasitasaidia, tushirikiane kutoa maoni yetu.
 
Huu muungano una umuhimu gani kwetu sisi watanganyika?Tunanyonywa mno na hao wazenji.Katiba inayoundwa ni ya watanganyika, inawahusu nini hao wazenji?

Muungano unaweza kuwa siyo tatizo, lakini kurundika idadi kubwa ya wazanzibar kwenye tume wakati ni wachache sana inafanya katiba isikubalike kabisa kwa watu wa Tanzania bara. Lzima wajumbe wa Zanzibar wapunguzwe kwenye tume ya katiba wabaki wawili ili katiba itakayotungwa iakisi vya kutosha mahitaji ya watu wa Tanzania bara na siyo kuamuliwa na Zanzibar.
 
Dawa ya huu upuuzi ni kuvunja huu muungano, hauna manufaa yoyote kwetu watanganyika, sana sana tunaambulia matusi toka kwa hawa wazenji.
 
Mtate msitake,
Hiyo ndio tume imeundwa kisheria!
na imepata baraka za kisheria.
Kelele zenu hasitasaidia, tushirikiane kutoa maoni yetu.
Nani aliyekwambia sheria ni msahafu? Kama hazifai haziwezi kukubalika. Watanzania bara wanahitaji katiba inayowakilisa maoni yao na siyo kutungiwa katiba na wazanzibar. Kwa nini wazanzibar hawakuwaalika Tanzania bara kutunga katiba yao? Zanzibzr siyo nchi kama ilivyo Tanganyika lazima kuwa na uwiano katika uwakilishi wa tume.
 
Dawa ya huu upuuzi ni kuvunja huu muungano, hauna manufaa yoyote kwetu watanganyika, sana sana tunaambulia matusi toka kwa hawa wazenji.
Kama wakilizimisha kuendelea na mchakato wa katiba bila kupunguza idadi ya Watu wa Tanzania bara hapa ndipo watanzania bara watakaposema enough is enough.
 
Kwanza katiba yetu inawahusu nini? Hii ni katiba ya TANGANYIKA sishauri hata kuwa na mjumbe mmoja wao wana katiba yao, au wao si nchi. Waondolewe wote tujadili katiba yetu
 
Back
Top Bottom