Zanzibar ilipata UHURU mwaka 1963, kwa nini ukweli huu unafichwa?

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
472
Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa Mji Mkongwe mapema mwaka 1963. Kipindi ilipopandishwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, huku kukiadhimishwa uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.

Na Taifa la Zanzibar lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa, mwaka huo 1963.

Je ni kwa nini hatusherehekei uhuru wa Zanzibar 12/Dec/1963 na dadala yake tunasherehekea mapinduzi ya mwaka 1964?
 
...Kipindi ilipopandishwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, huku kukiadhimishwa uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.
Samahani naomba kuuliza, hiyo bendera ndio kama ile iliyotumika kwenye mkutano wa CUF pale Manzese juzi?
 
Ili mradi Maalim na Jussa wamo ndani ya serikali hii tarehe lazima itarudishwa na kutambuliwa. Nchi ipo, bendera ipo, wimbo wa taifa upo, tarehe ya uhuru itakosekanaje? Nawahurumia sana akina "Mapinduzi Daima". Amani Karume kairudisha nchi ujombani kwa kuwa yeye hakuwa mtoto halisi wa Abeid.
 
Mkuu sijakupata kabisa. tafadhali,, Amani Karume hakuwa............?
 
Samahani naomba kuuliza, hiyo bendera ndio kama ile iliyotumika kwenye mkutano wa CUF pale Manzese juzi?

Hii hapa

tz-zan63.gif

On 10 December 1963, the Zanzibar Protectorate was granted independence as the Sultanate of Zanzibar by the British. The flag adopted was red with a green disc upon which were two yellow cloves. (Possibly because the flag was short-lived, variations exist on the design of the cloves.) The Sultanate, and its flag, didn't last long. On 12 January 1964 there was a violent Marxist/Africanist coup which resulted in the deaths or explusion of an estimated one in five of the Arab population.
 
Yes, Zanzibar walipata uhuru 1963 lakini ulikuwa uhuru-bandia. Uhuru wa remote control uliojaa makucha ya mkoloni yule yule waliyekuwa wanamfukuza na ndio maana kukawepo na Mapinduzi. Mapinduzi maana yake unapindua kile usichokubaliana nacho.

Bado nasubiri kwa hamu kumsikia Maalim Seif akiongea kuhusu uhuru wa 1963 na Mapinduzi ya 1964. Hapa ndio kuna siri kubwa kuhusu CUF ya mtandao ya Maalim Seif.
 
Walioupata huo 'uhuru' wamezuiwa na mtu yeyote kuusherekea?! Mi nadhani kama kuna walioupata lazima tu wanausherekea, labda tu msiohusika hampewi mialiko!!
 
Mkuu sijakupata kabisa. tafadhali,, Amani Karume hakuwa............?
Hakuwa mtoto wa Abeid Amani Karume na kwa kweli anafanana zaidi na akina Diria. Ndio maana Commando na Wazanzibar wengi hawakumtaka kabisa awe Rais. Madhara yake tumeyaona. Ngoja akina HU na MH watakuja na data kamili.
 
Huyu mtoa mada hivi anajua hata South Africa ilipata uhuru wake karne iliyopita lakini uhuru unaosherehekewa ni ule wa mwaka 1994...:A S-coffee:
 
Yes, Zanzibar walipata uhuru 1963 lakini ulikuwa uhuru-bandia. Uhuru wa remote control uliojaa makucha ya mkoloni yule yule waliyekuwa wanamfukuza na ndio maana kukawepo na Mapinduzi. Mapinduzi maana yake unapindua kile usichokubaliana nacho.

Bado nasubiri kwa hamu kumsikia Maalim Seif akiongea kuhusu uhuru wa 1963 na Mapinduzi ya 1964. Hapa ndio kuna siri kubwa kuhusu CUF ya mtandao ya Maalim Seif.
Haukuwa uhuru bandia. Commonwealth, UN waliutambua. Lengo hasa la Maalim, Jussa ni kuirudisha Zanzibar huko. Wako wengi ndani na nje ya Zanzibar kama akina Barubaru wetu humu. Hii SUK ni "transition" tu.
 
Sr.
Uhuru ni hali ambayo kwayo wenyeji wa Taifa, Nchi ausehemu yake wana madaraka ya kujichagulia dira na viongozi wawatakao, uwezo wakuwaondoa kwa mujibu wa sheria zilizo pitishwa na vyombo halali vya kitaifa; nakwa hiyo kuwa na sovereignty juu ya Taifa au nchi yao na mstakali wake. Uhuruni tofauti na mapinduzi, kwani mapinduzi yanauondosha utawala ulopo kwa nguvuau amani; ingawa aidha mapinduzi yanaweza kuleta uhuru kutegemea mfumo, dira nauongozi uliopinduliwa. Lakini mapinduzi yanaweza kuwa na dhaira ya kuletauwiano katika kushiriki katika usimamizi wa utawala, kugawana mali n.k.Mapinduzi ya Urusi yalilenga hili, lakini vita vya mapinduzi vya Marekanivililenga kuleta uhuru. Kuhusu Zanzibar inategemea mtazamo wako; Uhuru chini ya himaya ya Sultani uliwakilisha maono ya kitaifa au la?
 
Yes, Zanzibar walipata uhuru 1963 lakini ulikuwa uhuru-bandia. Uhuru wa remote control uliojaa makucha ya mkoloni yule yule waliyekuwa wanamfukuza na ndio maana kukawepo na Mapinduzi. Mapinduzi maana yake unapindua kile usichokubaliana nacho.

Bado nasubiri kwa hamu kumsikia Maalim Seif akiongea kuhusu uhuru wa 1963 na Mapinduzi ya 1964. Hapa ndio kuna siri kubwa kuhusu CUF ya mtandao ya Maalim Seif.

Mkuu kama ulikuwa uhuru bandia, sasa ile hotuba ya Waziri Mkuu wa Zanzibar na kuezeka bendera ya Zanzibar pale UN ilikuwa nini, maigizo pia?..
 
Mkuu kama ulikuwa uhuru bandia, sasa ile hotuba ya Waziri Mkuu wa Zanzibar na kuezeka bendera ya Zanzibar pale UN ilikuwa nini, maigizo pia?..
Ndivyo tulivyofundishwa shuleni Sr. Magdalena ili kuyakubali na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya 12/01/1964. Vunjeni Muungano muone kitakachotokea ambacho Mwalimu alikisema pale Kilimanjaro Hotel. Halafu eti RA anawaandaa ENL/AAAK au AAAK/ENL kuchukua serikali ya Muungano 2015! Bila shaka ulimsikia Maalim Seif na kauli yake tata ya kupokezana Urais wa Muungano tu.
 
katika nchi ambayo historia yake imeharibika na jamii imepotoshwa vya kutoshwa ni zanzibar
kuna mambo mengi ambayo yamefichwa kuhusu harakati za uhuru na mambo mengine
watu kama kina JOHN OKELO na hawapo kwenye vitabu vinavyotumika mashuleni na kufanya wasifahamike,huku vitabu vilivyopo vikitoa uongo kuwa karume ndie aliefanya mapindunzi,huku ni kudanganya watu.Nadhani tulifanya mistake sana ya kufanya muungano na hawa zanzibar ndio maana hata muungano wenyewe umekuwa kitendawili
 
Back
Top Bottom