Zanzibar huchangia TRA 1.4% lakini hugawiwa 4.5% ya mapato ya Muungano!!

Suluhu ya hili jambo ni serikali tatu tu! Hapo kitaeleweka nani anachangia nini kwenye muungano na kwa uwiano gani. Tofauti na hapo, muungano utalalamikiwa kila siku.

serikali tatu za nini?kama itakuwa si kushibisha watu tu
kila nchi inatakiwa ishike utaratibu wake,muungano ufe
 
Sishangai watanganyika kusema mnadhulimiwa na z'bar kwani huko kwenu kila sehemu baa kwa hivyo wengi wenu walevi kama siwote ndomana unazungumza vitu msivyovijua fatilieni mambo muujuwe ukweli kama z'bar inaadhulumiwa umeme znz unanunua tena mabilioni ya pesa kwa mwezi aminini nyie watanganyika 90% wazanzibar wahawautaki muungano kwani hauna faida kwa znz. Mungu ibariki z'bar
 
Suala la msingi kujiuliza hapa.

Kwanini Tanganyika mnapokwenda kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo yenu kama waTanganyika kwanini mnakopa kwa jina la Tanzania? Ina maana hamujui kuwa deni hili lina reflect hata kwa Znz pia.
Kwanini msikope kwa jina lenu Tanganyika?

hata kama tunakopa kwa kuwa-include wanzazibar,tuna haki ya kutumia hizo hela sisi watanganyika
maana gdp ya zanzibar ni sawa na wizara moja hapa tanganyika,so kamwe madeni hamtaweza kulipa,ndio maana hata kama mnataka mgao,itakuwa mnatuibia,hamna mnchachochangia cha maana then mnataka pasu kwa pasu,nyie bila tanganyika hamuez kujiendesha

soma hii uone kama uchumi wenu umekuwa mara nne(4)ili ujiulize hali yenu ilikuwaje kabla ya hapo na compare uchumi wenu uliokuwa na mchango wenu kwenye serikali ya muungano uone ni hasara kiasi gani mnatupa

Tanzania: Zanzibar Economy Grows Four Times
6 March 2010
Zanzibar economy has expanded over four times under President Amani Abeid Karume, with the generation of wealth increasing from Sh189.5 billion eight years ago to nearly Sh739 billion, The Citizen can report.

However, official figures obtained by this paper show, that despite the impressive gross domestic (GDP) performance, a majority of the Islanders are still poor, with 16 per cent of the rural dwellers living below the food poverty line.
more information

allAfrica.com: Tanzania: Zanzibar Economy Grows Four Times

Sishangai watanganyika kusema mnadhulimiwa na z'bar kwani huko kwenu kila sehemu baa kwa hivyo wengi wenu walevi kama siwote ndomana unazungumza vitu msivyovijua fatilieni mambo muujuwe ukweli kama z'bar inaadhulumiwa umeme znz unanunua tena mabilioni ya pesa kwa mwezi aminini nyie watanganyika 90% wazanzibar wahawautaki muungano kwani hauna faida kwa znz. Mungu ibariki z'bar
kama huna uhakika ni bora uklae kimya,deni hamtaki kulipa mnaleta mambo yasiyohusika,
siku mambo yakivurugika tukizima switch huku wachache sana wenye majenereta kutoka dubai,oman n.k ndo watakao kuwa na umeme
 
MZIGO HUU TULIOBEBESHWA WA KUWABEBA WANZANZIBAR WOTE KAMA WATOTO WADOGO NI MATESO SANA KWETU.
nadhani inahitajika support ya cia ili tuweze kuuvunja huu muungano,maana viongozi ni waoga,
huu muungano umekuwa gunia la misumari na kila siku wanaturudishwa nyuma tuu,

ZANZIBAR NA MUUNGANO Mwanzoni na katikati ya karne ya
kumi na tisa Zanzibar ilikuwa nchi
kamili,ilikuwa ikijitegemea kwa hali na
mali,na kwa wakati mmoja Zanzibar
ilikuwa ndio nchi yenye nguvu katika
Afrika Mashariki nzima.Zanzibar ya wakati huo ilikuwa haina deni,ilikuwa
ina pesa yake,bendera yake na
maamuzi kamili juu ya suala ya
nchi.Hakuna aliekuwa akituingilia
katika mambo yetu ya nje,maamuzi
yetu yalikuwa yakituhusu wenyewe,na tulikuwa tukinufaika
kwa yale tuliyokuwa
tukiyaamua.Baada ya muungano nchi
ya Zanzibar ilitoweka katika ramani ya
ulimwengu na kupoteza kiti chake
katika Umoja wa Mataifa.leo hii Zanzibar inajulikana na watu
wachache duniani,wengi wanaoishi
nchi za nje watakubaliana na sisi
kuwa Zanzibar haijulikani,na hii yote
imetokana na kumezwa na Muungano
usiokuwa na kichwa wala miguu,bila ya shaka Muungano kati ya bara na
visiwani umeinufaisha Tanzania Bara
kuliko visiwani kwa kila hali,yote
tunayaona haya katika kila nyanja
kutoka kwenye matibabu,elimu na
uchumi.Tunakumbuka Zanzibar ya zamani ilivyokuwa,tulikuwa tunalala
milango nje bila ya kuhofia majambazi
na wizi wenye kutumia
silaha,tunakumbuka kila mzanzibari
alikuwa akimjuwa jirani na
tukisaidiana kwa kila hali na mali.leo hii Zanzibar imekuwa haina maana
pesa mbili,wizi unyanganyi,ubakaji,na
wageni wa kila aina
tusiowajuwa,hatukatai kuwa na
wageni kutoka Bara wao ni ndugu
zetu na wenzetu lakini lazima kuwe na vitambulisho tujue kuwa hawa sio
watu kutoka Malawi au nchi
nyengine,sasa hivi ukijuwa kiswahili
tu basi hiyo ndio pasi yako ya
kuingilia Zanzibar.Tunajuwa fika kuwa
CCM haikufanikiwa kuweka Muungano sawa wala haikujaribu
kwa sababu wengi ya hao viongozi ni
kuwa wana mambo yao
yanawaendea.Chama cha CUF kabla ya
kuingia madarakani kulikuwa na
kelele nyingi kuhusu muungano,je leo hii kelele zile ziko wapi?Mbona
hatusikii chama cha wananchi CUF
kudai haki zetu bungeni?Jambo la
msingi kuwa viongozi wa CCM na CUF
wawe kitu kimoja na kutuwakilisha
sisi bungeni,tunataka haki zetu,tunataka heshima yetu
irudi,tunataka tuwe na mamlaka yetu
wenyewe na tuwe na uwezo wa
kuamua mambo yetu wenyewe ndani
na nje ya nchi.Tunataka raisi wetu
atambulike,tunataka uhusiano wa Zanzibar na nchi nyengine uimarike
kwa jina la Zanzibar,tunataka bendera
yetu na tunataka misaada ije kwa jina
la Zanzibar na sio Tanzania ambapo
tunaishia mikono mitupu.Tunataka
tuwe na timu yetu wenyewe ya mpira itakayoshirika makombe yote ya
kimataifa.Hatusemi tuvunje muungano
lakini tunataka marekebisho ili na sisi
tutambulike duniani kuwa Zanzibar
ipo na bado inadumu.Mungu ibariki
Zanzibar.Mungu Ibariki Afrika
 
zanzibar na muungano mwanzoni na katikati ya karne ya
kumi na tisa zanzibar ilikuwa nchi
kamili,ilikuwa ikijitegemea kwa hali na
mali,na kwa wakati mmoja zanzibar
ilikuwa ndio nchi yenye nguvu katika
afrika mashariki nzima.zanzibar ya wakati huo ilikuwa haina deni,ilikuwa
ina pesa yake,bendera yake na
maamuzi kamili juu ya suala ya
nchi.hakuna aliekuwa akituingilia
katika mambo yetu ya nje,maamuzi
yetu yalikuwa yakituhusu wenyewe,na tulikuwa tukinufaika
kwa yale tuliyokuwa
tukiyaamua.baada ya muungano nchi
ya zanzibar ilitoweka katika ramani ya
ulimwengu na kupoteza kiti chake
katika umoja wa mataifa.leo hii zanzibar inajulikana na watu
wachache duniani,wengi wanaoishi
nchi za nje watakubaliana na sisi
kuwa zanzibar haijulikani,na hii yote
imetokana na kumezwa na muungano
usiokuwa na kichwa wala miguu,bila ya shaka muungano kati ya bara na
visiwani umeinufaisha tanzania bara
kuliko visiwani kwa kila hali,yote
tunayaona haya katika kila nyanja
kutoka kwenye matibabu,elimu na
uchumi.tunakumbuka zanzibar ya zamani ilivyokuwa,tulikuwa tunalala
milango nje bila ya kuhofia majambazi
na wizi wenye kutumia
silaha,tunakumbuka kila mzanzibari
alikuwa akimjuwa jirani na
tukisaidiana kwa kila hali na mali.leo hii zanzibar imekuwa haina maana
pesa mbili,wizi unyanganyi,ubakaji,na
wageni wa kila aina
tusiowajuwa,hatukatai kuwa na
wageni kutoka bara wao ni ndugu
zetu na wenzetu lakini lazima kuwe na vitambulisho tujue kuwa hawa sio
watu kutoka malawi au nchi
nyengine,sasa hivi ukijuwa kiswahili
tu basi hiyo ndio pasi yako ya
kuingilia zanzibar.tunajuwa fika kuwa
ccm haikufanikiwa kuweka muungano sawa wala haikujaribu
kwa sababu wengi ya hao viongozi ni
kuwa wana mambo yao
yanawaendea.chama cha cuf kabla ya
kuingia madarakani kulikuwa na
kelele nyingi kuhusu muungano,je leo hii kelele zile ziko wapi?mbona
hatusikii chama cha wananchi cuf
kudai haki zetu bungeni?jambo la
msingi kuwa viongozi wa ccm na cuf
wawe kitu kimoja na kutuwakilisha
sisi bungeni,tunataka haki zetu,tunataka heshima yetu
irudi,tunataka tuwe na mamlaka yetu
wenyewe na tuwe na uwezo wa
kuamua mambo yetu wenyewe ndani
na nje ya nchi.tunataka raisi wetu
atambulike,tunataka uhusiano wa zanzibar na nchi nyengine uimarike
kwa jina la zanzibar,tunataka bendera
yetu na tunataka misaada ije kwa jina
la zanzibar na sio tanzania ambapo
tunaishia mikono mitupu.tunataka
tuwe na timu yetu wenyewe ya mpira itakayoshirika makombe yote ya
kimataifa.hatusemi tuvunje muungano
lakini tunataka marekebisho ili na sisi
tutambulike duniani kuwa zanzibar
ipo na bado inadumu.mungu ibariki
zanzibar.mungu ibariki afrika

naona umesahau kuwajumuisha waarabu kwenye hii historia yako
wao ndio waliokuwa wakiiendesha zanzibar-baada ya wao kuuliwa,zenji ikarudi to its roots
 
Kafanye utafiti ndipo uje na hoja za maana, yaonekana umekurupuka. 4.5% wanayo pata Znz sio kwamba inatokana tu mapato ya TRA , bali pia inajumuisha misaada ya kimaendeleo inayotolewa kwa Tanzania

Hata na wewe hujafanya utafiti angalau yeye ana utafiti kidogo wenye mantiki, kwani huo mgao unaotokana na makusanyo ya tra wanapata % ngapi? Kwani ruzuku ya umeme wanayopata ni mambo ya muungano? inamsaidia nani? Kama serikali ya muungano inaweza kutoa ruzuku ya umeme zanzibar kwanini wasitoe ruzuku hiyo kwa watu wa Bara?
 
naona umesahau kuwajumuisha waarabu kwenye hii historia yako
wao ndio waliokuwa wakiiendesha zanzibar-baada ya wao kuuliwa,zenji ikarudi to its roots

Historia ya waarabu katika kuitawala Zanzibar imepotoshwa sana. Lakini kwa watu kama nyinyi ambao mumeshalishwa kasumba siku nyingi hamuamini! By the way Vijana wa sasa wa Kizanzibari tunaanza kuufahamu ukweli wa historia za tawala mbali mbali pamoja na upotoshwaji uliofanywa dhidi ya Waarabu!
 
Mchungaji vipi siku hizi, naona unakurupuka sana. au ndio foleni za Dar inakubidi uwahi kazini.

Tanganyika ndio mzigo mzito kwa znz kwani madeni au mikopo yote wakopa kwa jina la Tanzania, na hivyo kuwaingiza madeni ZNZ katika kuyalipa.

I love Zanzibarians ladies, they are good on bed! Otherwise ningeshauri tuvunje muungano ....
 
Historia ya waarabu katika kuitawala Zanzibar imepotoshwa sana. Lakini kwa watu kama nyinyi ambao mumeshalishwa kasumba siku nyingi hamuamini! By the way Vijana wa sasa wa Kizanzibari tunaanza kuufahamu ukweli wa historia za tawala mbali mbali pamoja na upotoshwaji uliofanywa dhidi ya Waarabu!

Waarabu hawa hawa au wengine unaowaongelea? Maana wale walikuwa wafanya biashara ya binadamu wenzao! Mtu mweusi alikuwa takataka na walichokiacha nyuma pamoja na ukweli kuwa wao ndo walianza kufika sehemu nyingi za nchi yetu ni urithi usiorithika. Fanya tafiti vizuri uone! Tuongee mambo kwa kubalance sio kusema tu kwa sababu tuna key boards au midomo!
 
Mchungaji vipi siku hizi, naona unakurupuka sana. au ndio foleni za Dar inakubidi uwahi kazini.

Tanganyika ndio mzigo mzito kwa znz kwani madeni au mikopo yote wakopa kwa jina la Tanzania, na hivyo kuwaingiza madeni ZNZ katika kuyalipa.

Mbona sijana mahali umejibu hoja? Je ni sawa uchangie sh 1 katika 10 halafu udai sh 5?
Ardhi ni suala la muungano? Pesa za wabunge wa Zbar zinalipwa na Mzanzibar? Mishahara inayopelekwa kutoa TRA ina deni ? Umeme unaotolewa kama sadaka mzanzibar anachangia nini? Deni la umeme lililosamehewa kwa umeme wa bure mzbar amelipa?

Hata siku moja hutasikia mzbar akisema tuvunje muungano, utasikia tuboreshe. Unajua ni kwanini.
 
halafu cha ajabu pamoja na kubebwa kote bado wanasema wanadhulumiwa!

Ajabu ya hao wanao dai kubeba bado tu wanang'ang'ania "mzigo". Zanzibar hawana haja ya kubebwa na nyinyi ,wenyewe hamna mbele wala nyuma. Acheni unafiki wa kujifanya wahsani.
 
Mbona sijana mahali umejibu hoja? Je ni sawa uchangie sh 1 katika 10 halafu udai sh 5?
Ardhi ni suala la muungano? Pesa za wabunge wa Zbar zinalipwa na Mzanzibar? Mishahara inayopelekwa kutoa TRA ina deni ? Umeme unaotolewa kama sadaka mzanzibar anachangia nini? Deni la umeme lililosamehewa kwa umeme wa bure mzbar amelipa?

Hata siku moja hutasikia mzbar akisema tuvunje muungano, utasikia tuboreshe. Unajua ni kwanini.

Kama kwaida yako unafiki ndio zaidi. Muungano mnao ung'ang'ania nyinyi na CCM. Sasa utaanza na nyimbo "baba wa taifa wee" baba wa taifa.
 
Zanzibar ni Koloni letu na kamwe hatuwezi kuliachia, Tutaendelea kuitawala Zanzibara hata ikibidi Kimabavu
Kwanza jifunze kutawala tumbo lako...Baadae ulete hizo pumba hapa...MmKOLONİ UNA NJAA KAMA FİSİ.
 
@JK

a. Tanganyika wanachukua mshiko wa mashirika yote yaliyoko katika muungano bila kuwagawia wazenj (angalia mashirika yote yaliyoko chini ya mambo ya muungano.

b. Walipobinafsisha hayo mashirika mshiko wote ulibebwa na watanganyika na wazenj hawakupata mshiko wao..

c. Ajira nyingi katika mashirika ya muungano wanachukua watanganyika hivyo kuwanyima fursa wazenj ...

b. Biashara ya nje watanganyika wanafuta bila kufanya mgawo accordingly..list can go on..

sijui kama tuta maintain ukoloni wa aina hii, of course wakija kudai uhuru wao kwa njia za ajabu msishangae. na kulalama aisee..

Topical,

..yako mashirika kama Posta na Simu ambayo kama yalibinafsishwa ZNZ ilipaswa kupewa stahiki yake. Shirika la Posta na Simu lilikuwa chini ya EAC iliyovunjika mwaka 1977. kwa upande mwingine sidhani kama ZNZ ilishiriki ktk kutaifisha/kuanzisha National Bank of Commerce[NBC] kwa hiyo haistahiki hisa zozote zile kutokana na mauzo ya shirika hilo.

..kuhusu suala la ajira, si kweli kwamba waZNZ wananyimwa nafasi. Ieleweke kwamba ajira ktk mashirika ya umma, yaliyo ya muungano na yasiyo ya muungano, ziko wazi kwa Mtanzania yeyote yule. Majuzi kulikuwa na malalamiko ktk baraza la wawakilishi kwamba lecturers toka Zanzibar University wanaacha kazi na kukimbilia Univ of Dodoma. Huo ni ushahidi kwamba waZNZ wenye qualifications wanapata kazi bila matatizo ktk taasisi za muungano.

..Kuna special case kama hiyo ya wakili wa mahakamu kuu ya znz vs wakili wa mahakama kuu ya Tanzania[Tanganyika] ambayo inatakiwa ifanyiwe kazi, lakini sidhani kama ni tatizo kubwa.

..Kwa mtizamo wangu,i mwandishi anataka waZNZ watengewe "QUOTA" au idadi maalum ya ajira ktk mashirika hayo. Anajua likifanyika hilo basi waZNZ wanaweza kupata nafasi nyingi wasizostahili kama ilivyofanyika kwa nafasi za wabunge.

..Kuna maelfu ya waZNZ wapo kila kona ya Tanganyika wakifanya shughuli halali za kuwapatia kipato, ni jambo la ajabu kidogo kudai kwamba waZNZ wanabanwa au hawanufaiki na muungano huu.

..Kuhusu fursa za biashara za nje, na masuala kama Free Port, Off-Shore companies, etc kinachopaswa ni kuangalia maslahi ya pande zote mbili za muungano wetu. Kwa mfano, kuna kipindi ZNZ ilitaka watoze ushuru mdogo sana kwa bidhaa zinazoteremshwa bandarini ZNZ halafu bidhaa hizo ziingizwe Tanganyika bila kulipiwa tofauti ya ushuru. Huo ndiyo umekuwa mgogoro mkubwa kati ya ZNZ na TRA.

..kuna ripoti inayoelekza kwamba misamaha ya kodi inayotolewa ZNZ ni 46% ya kinachokusanywa huko, wakati kwa TGK ni 23--24% ya tunachokusanya. Zaidi ya hayo, waZNZ hugoma kulipia huduma za mashirika ya Tanganyika kama Tanesco, na zaidi wanataka wapewe gawio kubwa zaidi kutoka kasma ya Muungano[tanganyika]. Katika mazingira hayo ni nani anayemnyonya mwenzake??!!

..mimi naomba niwape changamoto ndugu zetu wa ZNZ, na hapa nitaomba nitumie maneno ya aliyekuwa Rais wa Marekani JF Kennedy. ASK NOT WHAT THE UNION CAN DO FOR YOU, BUT WHAT YOU CAN DO FOR OUR UNION.
 
Historia ya waarabu katika kuitawala Zanzibar imepotoshwa sana. Lakini kwa watu kama nyinyi ambao mumeshalishwa kasumba siku nyingi hamuamini! By the way Vijana wa sasa wa Kizanzibari tunaanza kuufahamu ukweli wa historia za tawala mbali mbali pamoja na upotoshwaji uliofanywa dhidi ya Waarabu!

Mpemba Mbishi,

..kweli kuna maeneo historia imepotoshwa.

..sasa kuna wanaotumia upenyo huo kupotosha zaidi.
 
Waarabu hawa hawa au wengine unaowaongelea? Maana wale walikuwa wafanya biashara ya binadamu wenzao! Mtu mweusi alikuwa takataka na walichokiacha nyuma pamoja na ukweli kuwa wao ndo walianza kufika sehemu nyingi za nchi yetu ni urithi usiorithika. Fanya tafiti vizuri uone! Tuongee mambo kwa kubalance sio kusema tu kwa sababu tuna key boards au midomo!

Mkuu hemu nisaidie hivi wale Waarabu walipokua wakifanya biashasa ya kununua watu weusi walikua wanawapeleka wapi? Mbona kule Uarabuni hakuna idadi kubwa (kama sikusema hakuna kabisa) hao watu weusi Isijekua Wazungu ndio walikua wanaifanya hii biashara na badala yake 'Zigo' hili wakatwishwa Waarabu! Naona baadhi ya nchi za Wazungu yapo hadi baadhi ya majimbo yana wale watu ambao wana maji ya kiafrika (Wazungu weusi).
 
..kabla ya mzungu kuingia, Mwarabu ndiyo alikuwa akitamba ktk eneo hili.

..pia wapo Waafrika walioshiriki biashara ya utumwa pamoja na Waarabu.

..popote pale utakapoona urafiki kati ya Muarabu na Mtemi/mtawala wa Kiafrika/Kitanganyika ujue ushirika huo ulihusisha biashara ya utumwa.

..the fact kwamba hakuna watu weusi Uarabuni haimaanishi kwamba Mwarabu hakushiriki biashara hiyo, bali inamaanisha kwamba watumwa hawakuhitajika kwa ajili ya nguvu kazi huko Uarabuni.

..Wareno nao walikuwa wameshika eneo la kusini mwa Afrika kuanzia Mozambique mpaka Angola na wao walishiriki sana ktk kukamata watumwa.

..ukweli mwingine ni kwamba dini mbili kuu za Ukristo na Uislamu zilishiriki na kuhalalisha biashara ya watumwa wa Kiafrika.
 
Back
Top Bottom