Zanzibar Hiyooo: Mwendo Mdundo!!!!

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Wanabodi,

Recently nimefurahishwa sana na wenzetu wa Zanzibar! Kwa nini? Wemeacha kuongea sana siasa kama walivyokuwa mwanzoni wenzetu wamejifunza kwamba too much politics hazitupeleki popote, sasa wanaongelea maendeleo... Jamaa wakiendelee hivi... wabara tunaachwa.

Angalia mojawapo haya mengi SMZ inayofanya. Narudia kuwaomba vijana kama Zitto, Mnyika, January etc ensure we tranform politics za Tanzania bado tunaongea mambo ya kizamani, lets talk about real development....

HabariLeo | Wakurugenzi wa Mipango watakiwa kuwajibika

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema wakurugenzi wa Mipango na Sera watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu, watalazimika kujiondoa wenyewe kwa
sababu watakuwa wameshindwa kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo wakurugenzi wa Mipango na Sera mjini Unguja ambayo
yamefadhiliwa na Jumuiya ya Madola.

Mzee alisema Serikali malengo yake makubwa ni kuona wakurugenzi hao wanakuwa wabunifu katika maeneo mbalimbali na baadaye mafanikio makubwa yanafikiwa.

Alisema wakurugenzi hao kutokana na majukumu yao makubwa wao ni kiungo kizuri kati ya wizara na taasisi zote zilizomo katika wizara hiyo.

"Wakurugenzi wa Mipango na Sera ndiyo tegemeo kubwa la mafanikio katika wizara zetu za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar...tunawataka wawe wabunifu katika utendaji wa shughuli zao za kazi za kila siku," alisema Waziri huyo.

Aidha, alisema wakurugenzi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao, itakuwa wameshindwa kazi na hivyo watalazimika kukaa pembeni kutoa nafasi kwa watendaji wengine.

Alisema Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameamua kuunda Idara za Mambo ya Utafiti na Sera katika kila Wizara kwa lengo la kubuni uwezo na mambo ya utafiti katika wizara hizo.
 
Kumbe nako wamesema! heri mimi sijasema, kwi kwi kwii kwiiii
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema wakurugenzi wa Mipango na Sera watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu, watalazimika kujiondoa wenyewe kwa
sababu watakuwa wameshindwa kazi.

Sasa Nungunungu, haya yanatofauti gani na ya magamba kuwataka wenye magamba kujipima na kujivua wenyewe? Je, hii inatofauti gani na ile kauli za kina Pinda kuwa wakurungenzi watakaoshindwa waachie ngazi?

Taabu kweli kweli
 
Mbona hizo kauli za serikali ya sisiem kuwataka watumishi wake wajiondoe wenyewe tumezizoea? Cha ajabu hakuna hata mmoja aliewahi kujiondoa mwenyewe. Basi utajiuliza je kila kitu kiko sawa? Jibu ni hapana! Zaidi ya asilimia 75 ya matarajio ya serikali hayatekelezeki. Lakini kwa nini basi kujiondoa hakutekelezwi? Jibu ni kwamba hizo kauli ni usanii unaowawezesha viongozi wakuu kupoteza mda ili walau waendelee kulamba posho. Hiyo ndio Tanzania bana ya wadanganyika!!
.
 
Sasa Nungunungu, haya yanatofauti gani na ya magamba kuwataka wenye magamba kujipima na kujivua wenyewe? Je, hii inatofauti gani na ile kauli za kina Pinda kuwa wakurungenzi watakaoshindwa waachie ngazi?

Taabu kweli kweli

Ndugu,

Tangu lini Kasheshe akawa Nungunungu. Muda wangu ni kidogo kuandika sana humu. Kweli wazanzibari watatuacha kwani sisi ni mabingwa wa kufanya vitu kwa mdomo; tunacheza mpira kwa mdomo, tunafanya kazi kwa mdomo. Mtu kaajiriwa na analipwa mshahara lakini anatumia hadi 4 hours za muda wa kazi humu JF na still anailalamikia serikali kutwa kucha.

Badilikeni, maendeleo hayaletwi kwa kushinda kwenye keyboard na porojo za JF!
 
Mimi nachukia kweli wanaoita tanganyika, tanzania bara na kwanini zanzibar hamuuti hivyo!
 
Back
Top Bottom