Zanzibar Hatarini zaidi

B ila shaka kitambulisho cha Utanzania hakija kubalika zanzibar kwa kuwa Zanziabr pia wana vitambulisho vyao vya Uzanzibari. Kama ni nchi moja kwanini kuwe na vitzmbulishio karibu sabini?. Iko tatizo hapa hapa. Wazanzibari wana vitambulisho vyao na watanganyika wawe na vyao. Sisi wazanzibari tunajitambulisha kote ulimwenguni kama wazanzibari kwanza baadae n dio tanzania kwa shinikizo wala sio hiari.
Wazanzibari wanataka nchi yao huru. Tatizo ni ukoloni. Tunaweza kudumisha uhusiano wetu tukiwa mbalimbali kuliko hali ilivo sasa hivi.

Unaongelea duniani wapi huko unapojitambulisha kwa kitambulisho cha Uzanzibar??
 
Matatizo yapo kwenu wabara. Ndugu zetu nyinyi mumaktaa kuwafahamu wazanzibari. Huu ukaidi wenu ndio unawasukuma wazanzibari kudai nchi yao. Hamuna lugha ya upole. Mawaziri wenu, ambassadors wenu, viongozi wenu na hata walalahoi wanawadharau sana wazanzibari. Wazanzibari wamechoshwa na udanganyifu na kuburuzwa na serikali ya Tanganyika kwa jina la muungano. Basi wakati umefika. Muungano kuvunjika ni kama kufa. Kila mtu atakufa na muungano pia unakufa. Sasa hivi muungano upo ICU(coma).

Kumbe problem ni kubwa kuliko nilivyofikiri. Poleni sana, mkishamaliza kulalama mvunje muungano.

Maneno maneno tu ya chokochoko......na ubinafsi umewajaa.
 
Sidhani kama itakubalika huko Zanzibar.

Kwani waZnz ni watu makini sana , pamoja na tafauti zao lakin ukija kwenye maslahi a nchi yao siku zote wanakuwa wamoja na kutetea kwa nguvu zao zote.

Tuvute subra tuone ukweli na usahihi wa maneno haya.
 
B ila shaka kitambulisho cha Utanzania hakija kubalika zanzibar kwa kuwa Zanziabr pia wana vitambulisho vyao vya Uzanzibari. Kama ni nchi moja kwanini kuwe na vitzmbulishio karibu sabini?. Iko tatizo hapa hapa. Wazanzibari wana vitambulisho vyao na watanganyika wawe na vyao. Sisi wazanzibari tunajitambulisha kote ulimwenguni kama wazanzibari kwanza baadae n dio tanzania kwa shinikizo wala sio hiari.
Wazanzibari wanataka nchi yao huru. Tatizo ni ukoloni. Tunaweza kudumisha uhusiano wetu tukiwa mbalimbali kuliko hali ilivo sasa hivi.
Vitambulisho vya Wazanzibari vinafaa na vinatumika kwa masheha kuwakataa na kuwabana wapinzani. Sheha huyo huyo aliyekuuzia kiwanja, au mume wa mwanawe ikiwa huyu atakuwa mpinzani, siku ya kudai kitambulisho anadai huishi mtaani kwake na mkwewe hamtambui. Hivi hutumika zaidi wakati wa uchaguzi wa wawakilishi.

Vitambulisho vya Watanzania vitatumika kwa kuwachagua wabunge na Raisi wa JMT na haki ya kuishi popote Tanzania.
 
wa zanzibar ni wabinafsi, zanzibar hakuna rasilimali yeyote ya maana zaid ya karafuu, lakini wamekuwa na gubu ilhali wao ndio wamewekeza zaid huku bara

wa zanzibari wamepewa fursa kubwa kisiasa na ki uchumi, kisiasa wanaweza kupata nafasi yeyote bara lakini mtu wa bara hawezi kupata hata ujumbe wa mtaa

ki uchumi na kijamii ni rahisi mzanzibari kupata eneo na hata kufanya biashara huku bara kuliko m bara kwa zanzibar

lakini ukipita mitaani zanzibar ni kila siku maneno hayaishi unakuta stika zinasema 'zanzibar tuachwe tupumue' 'usiseme muungano ni mkataba tuuu' kwenye maskani ni uchochezi kila uchao

mimi naona wazi wakati umefika, kura ya maoni ipigwe kwa uhuru na haki then ikionekana haja ya kuvunja muungano na uvunjwe ili mpinduane pinduane kama madagaska, leo ustadh juma kawa rais kesho maalim hussein keshokutwa tunawakatia umeme na mlivyo na kiburi mtauzwa mchana kweupe
mtarudishwa enzi za usultani

shauri zenu na fikra zenu!

Hah ah haaa...Enzi za Usultani Zanzibar haikuwa fukara...Enzi hizi za watanganyika na Muungano ndio Zanzibar imekuwa fukara...
 
Mtabe,

..sasa kama nyinyi mko huku Tanganyika, kwanini mnatuzuia tusije Zanzibar??

..sisi hatuna tatizo ikiwa mtapenda kuvunja muungano, tatizo ni haya mambo yanayoleta chuki miongoni mwa wananchi.

JokaKuu,

Hakuna mtanganyka anaezuiliwa kwenda na kuishi Zanzibar. Mimi nilisoma na watanganyika ambao wengi wao walikua wanakuja kusoma Zanzibar baada ya kufeli darasa la saba Tanganyika.

Sisi kilio chetu ni mamlaka( maamuzi) ya nchi yetu . Hapa Zanzibar wapo hata wakenya na raia wa nchi nyengine. Mazingira ya chuki mnayatengeneza nyinyi wenyewe. Huwezi kuniambia Zanzibar sio nchi ,halafu utegemee mapenzi kutoka kwangu. Kwanza mnatakiwa mufute zile fikra za kidikteta kwamba nyinyi ndio waamuzi wa mustakbali wa Zanzibar.
 
ukweli Zanzibar si nchi nje ya mipaka ya muungano so sidhani kama mzanzibari (wanavyojiita) anaweza kutumia kitambulisho chake kwenda nchi jirani bila kujitambulisha kama mtanzania
Huo utabaki kuwa ukweli japo mchungu
 
Dharau na majivuno, kejeni na majigambo, ubinafsi na choyo chenu ndo unawafanya wazanzibari kudai zanzibar yao. Dharau imezidi mno, hakuna majibu kwa maswali magumu yanayoulizwa na wazanzibar bali manachojua ninyi ki dharau na kejeli tu. Yaani mzanzibari hata kama ni msomi wa daraja gani kwenu ninyi ni onyo tu ni mbumbumbu n.k. Kuweni wastaarabu, kwa kujibu hoja badala ya kuzidi kujalizana chuki na kuleta kejeli zidi ya wazanzibari. Nakumbuka waziri wa Ushirikiano wa Afrika mashariki mwaka juzi 2010, akijibu swali bungeni la kwanini wazanzibari hawapatiwi fursa sawa za kufanya kazi katika office yake alitoa majibu ya ufasaha sana, nilifurahi binafsi maana si kawaida kwa wabara kuwathamini wazanzibari. Yeye alikiri kwamba ni kweli kuna wazanzibari wachache katika office yake lakini tatizo ni wazanzibari wenyewe hawataki kuja kufanyakazi bara! alitoa mifano akisema, nafasi hutangazwa ila wanzanzibari hawaombi, wachache wanoomba hufanya vizuri sana kwenye interview ila tatizo ni kwamba wanapopewa fursa hawataki kuja bara. alitoa mafano mwengine akisema karibuni walifanya interview na mzanzibari pekee alieomba alikua ni best candidate lakini alipopewa offer hakutaka kuja kufanya kazai bara. Huyu waziri alikua muungwana sana maana alijibu kwa upole mno na alionyesha ustaarabu wa hali ya juu. kwa wengine husema wazanzibari hawana uwezo. hivi ilishatokea kwa TRA and BoT, wakiulizwa kwa nini wazenj hawapewi fursa ispokua za uangalizi wa office ete wanasema wazenj hawana uwezo! shame upon you!
 
wewe jamaa mjinga sana hivi hujui kua hata mtakatifu nyerere kua alisoma makerere uganda? Je nae alikua mganda?

Heb njoo utembee zanzibar utoe ushamba mana naona uko mbali sana kwenye vijiji vya mkoa wa dodoma huko ambako watu hata gari kwao ni ajabu.

Ujue tu kuna wageni kibao wanaosoma udom ambao si watanzania je nao waondoke?

Istoshe udom imejengwa kwa fedha ya jamhuri ya muungano ya tanzania hivyo basi wazanzibari wana haki kufaidi nguvu zao.
mimi na wewe nani mshamba muungano mnasema hamuutaki lakini fursa zote za muungano mnazita muuvunje mapema mkichelewa tutauvunja sisi tutawatimua halafu mjue kama muungano ndio uliwafanya nyinyi kuitwa watanzania
 
Hii mipango ccm wangesitisha kwanza maana hawajui kesho itakuwaje na nani atashika Dola. Ingekuwa ni sera ya Taifa ningewashauri waendelee
 
B ila shaka kitambulisho cha Utanzania hakija kubalika zanzibar kwa kuwa Zanziabr pia wana vitambulisho vyao vya Uzanzibari. Kama ni nchi moja kwanini kuwe na vitzmbulishio karibu sabini?. Iko tatizo hapa hapa. Wazanzibari wana vitambulisho vyao na watanganyika wawe na vyao. Sisi wazanzibari tunajitambulisha kote ulimwenguni kama wazanzibari kwanza baadae n dio tanzania kwa shinikizo wala sio hiari.
Wazanzibari wanataka nchi yao huru. Tatizo ni ukoloni. Tunaweza kudumisha uhusiano wetu tukiwa mbalimbali kuliko hali ilivo sasa hivi.

Samahani mkuu, hapo kwenye RED, we unaandika ukiwa bara au visiwani? na umesema mkiwa popote huwa mnajitambulisha kama Wazanzibari na sio Watanzania, hivi huwa Passport zenu zimeandikwaje kweli? NI Zanzibar au Tanzania?

Halafu ushauri tu mkuu, ukiwa mchoyo usiwe mroho! Kama hupendi kulisha wengine na wewe usipende kula kwa watu! Anyway, ni ushauri tu!
 
Unajua wazanzibar wanapenda na wanashupalia sana kuuvunja muungano ila ukizungumzia kuhusu wazanzibar waliopo bara watatakiwa warudi kwao wakaijenge nchi yao na walipo kazini waache warudi kuajiriwa kwao zanzibar hili kwao mbona linaleta kigugumizi kwao hawakubali kuzungumzia?? nini siri hapa? sijapata majibu ina maana zanzibar hakuna nafasi za kufanya biashara na kuajiriwa???
 
Chao chao chetu chao! Afadhali iwe serikali moja ili chetu kiwe chao na chao chetu.

Serikali moja bado ni balaa kwa Zanzibar. Serikali tatu ndio suluhisho la kuungana na nchi kama Zanzibar. Natamani niishi na nione muungano wa serikali tatu ikiitwa Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (SMTZ)au The United Republic of Tanganyika and Zanzibar(URTZ). Ee mwenye enzi Mungu sikia maombi yangu.
 
Kwa aman ya pande zote mbili n bora Zanzibar na Tanganyika zibaki kuwa nchi huru. Kama ni jumuiya ya muungano kama africa mashariki sawa!!! Huku tuendako na huu muungano mambo yanaweza kuwa s shwari tena!!
 
Back
Top Bottom