ZANZIBAR HAINA FISADI hata mmoja

Ninadhani Mwinyi mihogo anavyojua yeye ufisadi ni wizi tu tena wa mabilioni - na kwa hilo yuko sawa kwani Zanzibar hakuna yaho mabilioni ya serikali kueza kuyafisadi, lakini ukiangalia upande mwengine wa maana ya ufisadi Zanzibar umejaa na unachefua moyo lakini wa kuutangaza hadharani hajatokea tu.

Mfano mdogo ni kugawana kwa shamba la Selemu kwa vongozi wa juu wa serikali kila mmoja akapewa kipande chake na kuuza. Shamba la ng'ombe Mtoni nani anajua lilivyotolewa.

Katibu Mkuu wa kilimo katika kipindi chaMradi wa MANSEP kajenga nyumba ngapi za kifahari ziisizopungua milioni mia sita kwa kila moja ( kwa Zanzibar ni fedha nyingi hizo kuchotwa kutoka serikalini).

Huyo huyo Mwinyihaji muulzeni alipataje kiwanja chake cha Mbweni kama si kuwageuka walalahoi - Wakati akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, baadhi ya wafanyakazi wakati vinapimwa viwanja vya Mbweni waliomba wapatiwe viwanja katika sehemu ilokuwa inafugwa kuku ( Shamba la serikali) Mwinyihaji aliwaahidi wapeleke maombi na yakpitia kwake atayabariki - wapi baada ya muda walishtukizia sehemu inapimwa na viwanja kugawiwa kinaMwinyihaji Makame na kina Brigadia mstaafu Mwakanjuki wakati huo akiwa Waziri wa Kilimo - Jee huo ni nini?
 
Back
Top Bottom