Zantel na Zain wapunguza gharama za internet

Unlimited mbona zipo mjini. Kuna ISPs wengi mjini wanauza unlimited downloads/uploads na huja na Dedicated speeds kulingana na budget yako.

Mfano:
Ninatumia ~2GB/Day. Speed yangu ni dedicated (meaning its not shared with other customers). Youtube, ninaangalia vizuri tuu. Lakini nipo kwenye corporate plan = i.e. More $||TZS zaidi ya > 110,000/month.

Sasa kwasababu sio kila mtu ni malaika. Wengine wakipata unlimited basi wanataka kudownload internet nzima siku hiyo hiyo.. Wengine movies ili wakauze , wenginee...(wacha nikianza sitamaliza)..etc etc. Sasa kama unashare speed na huyo jamaa basi wateja wengine wanaumia. Kwahiyo , its only fair yeye alipe zaidi ili apewe link yake mwenyewe na haki yake (kudownload anavyotaka).

Kwa ufupi ukitaka unlimited utapata....swali ni, What's your budget ?

B.P (2010)

Hapo ndio tatizo , mara corporate plan , mara dedicated line , mara ur budget kwa nini kitu kisiwe clear unaposema Unlimited ? .TTCL wana Unlimited ila speed ni ndogo kuliko ile ya wanao lipia kwa bundles.

Sijakuelewa hapo unapo sema 2GB/Day una maan gani , yani 2GB a day? hizo hainitoshi ,nina vitu vingi zaidi kwnye net naangalia ziadi ya kusoma email na ku chat. Mimi huw an ngalia zaidi videos za News , shows n videos , kwa plan ya 2GB a day hainitoshi kabisa.
 
Wakubwa, hii modem ya Zain inaweza kutumika mtandao wa Zantel na Voda?

Yah mkuu. Ingawa mimi sijawahi sana kufuatilia, ila nina jamaa zangu wanatumia modem za Zain kwenye Voda na Zantel. There is a software tool they use to patch the dongle to remove the lock. Will try to get more details next time.

Personally, I use 4GB a month, and I download a files and watch clips from UTube. It's enough if you are not downloading movies.
 
Yah mkuu. Ingawa mimi sijawahi sana kufuatilia, ila nina jamaa zangu wanatumia modem za Zain kwenye Voda na Zantel.
Ahsante. Ila kuna wakuu wamenambia Zantel internet ni CDMA technology, hivyo huwezi tumia GSM Sim card ya Zain na Voda.

Kuhusu ku unlock, hilo sio tatizo kwa sasa, kwanza kabisa nilitaka kujua technology za mitandao zinaendana?
 
Invisibe mi naomba unifahamishe ni jinsi gani unajiunga na hizo tarrif zao hasa hii ya Zantel maana mi ndio ninayo.
 
Ahsante. Ila kuna wakuu wamenambia Zantel internet ni CDMA technology, hivyo huwezi tumia GSM Sim card ya Zain na Voda.

Kuhusu ku unlock, hilo sio tatizo kwa sasa, kwanza kabisa nilitaka kujua technology za mitandao zinaendana?

Whoever told you about this, doesn't have a good understanding as what is CDMA and GSM. To cut it short, these devices are interchangeable. The only reason you can't swap providers is because of the hardware lock which can easily be circumnavigated with software tools.
 
Sio sawa hii, hardware za GSM na CDMA ni tofauti.
 
Mie hapa natumia 1GB kwa mwezi inatosha kabisa bila dowloading ya mafile makubwa.

Mie nimejaribu hiyo 3GB ya Airtel (Zain) lakini naona sitoweza kumaliza kwa siku saba lakini ikifika muda hujamaliza wanazikata sasa hiyo haina mana wangeweka nitumie mpaka zitakapo isha siyo zikifika siku saba wanakata hata kama nimebakiza 1GB.
 
JAMANI WHAT ABOUT HAWA UHURU ONE VIPI??? WAO NI WIRELESS CONNECTION THE WHOLE DAR AND ITS UNLIMITED AND ITS 40,000 Tsh... Has anyone used their service I saw their website na nataka kurudi dar I was searching on affordable and unlimited internet service provider Uhuru One wakatokea Whats their speed?? Their charges are okay.
 
Whoever told you about this, doesn't have a good understanding as what is CDMA and GSM. To cut it short, these devices are interchangeable. The only reason you can't swap providers is because of the hardware lock which can easily be circumnavigated with software tools.
I wish to differ. As Kang said, GSM and CDMA are different technologies.
 
YA TTCL MNAYAJUA?

Nilisoma makala yako kwenye raia Mwema na kati ya vitu ulivyozungumzia ni ahadi za mtandao na kushuka kwa bei baada ya mkongo kuwasili. Nikuhakikishie kuwa bei zimeshuka mno kwa viwango vilivyokisiwa. Kwenye TTCL Broadband Mwaka jana kipindi kama hiki 500MB ilikuwa ikiuzwa shilingi 30,000. Sasa hivi Kwa fedha hiyo hiyo unanunua 2GB (sawa na 2,048MB) ambayo ni chini ya bei ya zamani kwa asilimia 75. Pamoja na punguzo hilo kasi imeongezwa kutoka 2Mbps kwenda 8Mbps.

Kwenye huduma za TTCL Dedicated service (kwa wateja wakubwa) kwa mfano bei ya 64Kbps imeshuka kutoka shiling 1,200,000 (mwaka jana kipindi kama hiki) hadi shiling 250,000 (bei ya leo). Hapa bei imeshuka kwa asilimia 79.17 au karibia 80%. Huduma zote za dedicated zimeshuka kwa viwango hivyo ambavyo kusema kweli ndo ile asilimia 80% iliyotabiriwa. Sasa unaposema bado mnasubiri, si kweli kwani hali inaonesha kuwa bei imeshashuka tena kwa viwango vya zaidi.

Pengine sijazungumzia bei ya simu za mkononi ambapo sasa hivi ni Sh.1 kwa sekunde na kwa TTCL mobile unakuwa na namba tano ambazo unazipigia bure kabisa baada ya dk. ya kwanza, yaani shilling 60 tu kwa simu nzima bila kuangalia urefu wa simu hiyo.

Kwa hiyo ni vizuri tunapoandika makala kama hizi tuwe tunawasiliana na wahusika ili kupata taarifa sahihi badala ya kuueleza umma habari zisizo na uhakika.

Mkuu,

Mimi Nimeguswa na bei ya dedicated. Kama 64kbps ni 250,000 unaweza kujua bei ya 1 Mbps ? Naona wameondoa bei za dedicated kutoka tovuti yao ..

Asante
 
Soko la internet bado ni changa, isipokuwa kwa mtizamo wangu muhimu zaidi ni download/upload speed kuliko bandwidth limits.

Kwa mfano unaweza kuwa na 8GB bandwidth au tuseme hata unlimited, lakini speed ni 128kbps, itakuwezesha ku-download torrents za movie 20 - lakini ikakuchukua mwezi mzima, ukiwa na 5Mbps, utafanya kazi hiyo hiyo kwa siku moja. Speed, speed and speed.

Kwa hiyo, marketing strategy ya ISPs ingebadilika na kuwa combination ya speed na bandwidth. Ukitaka kujua genuine speed / bandwidth limits ulizia Dedicated Internet Service ndiyo utajua unapata nini.

Mfano 1Mbps ya TTCL inagharimu 1,000,000 kwa mwezi, inawezesha hata mashirika ya utangazaji kurusha matangazo ya quality nzuri kutoka Tanzania. Hata hivyo nadhani mambo yanazidi kubadilika, soon kutakuwa na real broadband connections kwa bei ambayo ni rahisi na itachochea internet based business activities.
 
jamani kuna mwenye kujua bei na vifurushi vya sasatel maana nina modem yao nanuaga vocha naweka kawaida yaani nikifungua hata ukurasa wenye picha nyingi 1000 linaisha hapo hapo
 
jamani kuna mwenye kujua bei na vifurushi vya sasatel maana nina modem yao nanuaga vocha naweka kawaida yaani nikifungua hata ukurasa wenye picha nyingi 1000 linaisha hapo hapo

Hakikisha baada ya kuweka Voucher za kifurushi unawapigia customer care ili wakusaidie kuactivate. Usipofanya hivyo na kuanza kutumia voucher itaishia kwa bei ya rejareja.

Angalia bei za vifurushi vya internet hapa: Our Tariffs - Sasatel homepage

Au unaweza kutumia unlimited kama una simu zao za mezani: 60,000/- per month
 
jamani kuna mwenye kujua bei na vifurushi vya sasatel maana nina modem yao nanuaga vocha naweka kawaida yaani nikifungua hata ukurasa wenye picha nyingi 1000 linaisha hapo hapo
Tupa hiyo modem na kanunue ya Zantel ujiachie kwenye net...
 
Habari njema ni kwamba Zantel wamepunguza zaidi bei ya modem zao za EC168 toka Tsh99,900 hadi 46,000..

Mimi niko Tanga na nimekwenda Zantel shop Modem ya EC168 ni TZS 49,900.

Maelezo niliyopata kwa mwakilishi wa Zantel kuwa wanamategemeo ya kujiunga na ''Fibre Optics'' soon kwa mkoa wa Tanga na ni mategemeo kuwa gharama za internet zitashuka sana zaidi ya bei ya sasa.

Pia amenieleza kuwa Zantel inajikita zaidi katika maswala ya Internet kuliko Voice ie simu. Kwa hiyo tutarajie best rate katika soko kutoka Zantel na Speed yao ni nzuri sana.
 
Hakikisha baada ya kuweka Voucher za kifurushi unawapigia customer care ili wakusaidie kuactivate. Usipofanya hivyo na kuanza kutumia voucher itaishia kwa bei ya rejareja.

Angalia bei za vifurushi vya internet hapa: Our Tariffs - Sasatel homepage

Au unaweza kutumia unlimited kama una simu zao za mezani: 60,000/- per month
Mkuu thanx a lot, nimecheck na nimeelewa sasa,
Tupa hiyo modem na kanunue ya Zantel ujiachie kwenye net...
kweli kabisa kuna haja ya kufanya hivyo baada ya kuona vifurushi vyao
 
Guys, mimi nina ka internet cafe ka mchwara mtaani sehemu za nyuma ya Airport (VITUKA) hapa Dar maeneo ambayo siwezi kupata broadbend service za TTCL kwani hakuna nyaya za simu zao, natumia CATS-NET, unlimited services, USD 150 kwa miezi mitatu kwa 64kbps. Wanacharge USD250 kwa miezi mitatu kwa 128kbps. It's 100% unlimited. Tatizo kidogo wakati fulani inasumbua lkn kutegemeana na maeneo ulipo. Nimezunguka sana sijaona ISP mwingine mwenye good rates kama hawa jamaa. Tumia 24 hours 7 days a week kwao sawa tu.
 
Back
Top Bottom