Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Malawi na Zambia yatalega lega,kihistoria Majirani hawa kusini mwa Afrika wana Nasaba,Watu wa Malawi wanaingiliana sana na watu wa Zambia na kuna familia zipo kiasili pande zote za Nchi hizi.Hapa kuna Jambo la kujifunza na haswa suala zima la nguvu za Rais.Rais Mteule wa Zambia Michael Chilufya Sata ni mtu wa visasi na mmtoa maamuzi yote mwenyewe bila kujali sana maamuzi ya washauri wake,Kwa kuwa Watanzania ni wapenda mambo ya haraka na ya mlipuko,Rais huyu (Labda kwa kuwa anatoka upinzani) amekuwa na upenzi mkubwa kutoka kwa Watanzania walio wengi,labda ni kutokana na maamuzi yake makubwa anayoyafanya kwa haraka.
Hapa naandika machache kuonyesha uharaka na utendaji kazi wa Rais Sata,haya ni maoni yangu binafsi nipo wazi kupingwa na kushauriwa kwa sababu tunajifunza kwa njia hii,Kwangu Mimi naona Afrika hatuhitaji Viongozi Wababe kama Sata bali tunahitaji Taasisi kama Bunge,Mahakama na Vyombo vya Ulinzi Imara.Hivi karibuni baada ya kuchaguliwa Rais Sata ameingia ktk mgogoro na Rais Mstaafu,Rupia Banda baada ya Sata kudai kuwa Banda ana asili ya Malawi na kwamba Mama yake Banda bado anaishi Malawi hata baada ya Banda kuwa Rais wa Zambia na sheria mojawapo ya kuwa Rais wa zambia ni lazima uwe mzaliwa wa Zambia na Wazazi wako wote wawili wawe ni Raia wa Zambia.
Rais Sata alifukuzwa (Deportation) Zambia mwaka 2007 baada ya kuonekana kuwa ziara yake hiyo binafsi ilikuwa na nia ya kwenda kusaidia upinzani dhidi ya serikali ya Bingu Wa Mutharika.Mwezi Oktoba 2011 Rais Sata alikataa kuhudhuria Mkutano wa Comesa kwa madai kuwa lazima serikali ya Malawi imuombe msamaha kwa sababu ya kitendo cha kufukuzwa Nchini humo mwaka 2007.Serikali ya Malawi ilikataa kufanya hivyo.
Mara baada ya kuapishwa Rais Sata aliwaomba radhi Angola kwa maelezo kuwa Serikali ya Mzee kaunda ilifanya kosa kubwa kuwasaidia UNITA na Jonas Savimbi,kwa maana hiyo anawaomba Msamaha serikali ya Angola kwa kosa hilo kubwa,alipobanwa na vyombo vya habari vya Nje Sata alidai amefanya uamuzi huo kwa sababu za kiuchumi,ni rahisi kununua mafuta Angola kuliko sehemu yoyote duniani.
Rais Sata mara baada ya kuanza kazi alimfukuza kazi Mkuu wa Ant-corruption Godfrey Kayukwa na nafasi yake kupewa Mwanamama Rosewin Wandi,sababu iliyotolewa ktk kumuondoa Kayukwa ni kwamba Taasisi hiyo ilishindwa kutoa majibu kwanini tenda ya kuchapisha nyaraka za Uchaguzi inapewa kampuni moja bila ushindani/mchakato (National printing group) kwa kipindi cha chaguzi mbili tofauti,hali hiyo ilionyesha kuwepo kwa rushwa ktk skuadi ya Ant-corruption.lakini ukweli wa mambo ni kwamba Ant-Corruption hiyo ilishawahi kumuhoji Sata (Alipokuwa raia wa kawaida) baada ya kumkuta ana jumla ya $ 500,000 ktk moja ya akaunti zake za Bank, Rais Sata pia alishawahi kuzuiwa Uwanja wa Ndege wa Johannesburg/Afrika kusini baada ya kukutwa anasafiri na kiasi kikubwa cha pesa.
Kwa kuonyesha kuwa Sata ni mtu wa visasi,na bado ana kinyongo na Malawi,Mwezi Oktoba ameamuru Redio moja ya Nchini Malawi isirushe Matangazo yake ndani ya Zambia,Redio hiyo inamilikiwa na Atupele Mtoto wa Aliyekuwa Rais wa Malawi,Mzee Bakili Muluzi.
Kwa hiyo maamuzi haya ya kupandisha Pango la Nyumba (Ubalozi) ni moja kati ya njia zake za kuikomesha Malawi,bado tutasikia mengi makubwa katika Utawala huu mpya wa Rais Michael sata.Lakini ni wazi kuwa masuala ya Nje na Diplomasia ya kimataifa kwa ujumla anahitaji ushauri madhubuti,vinginevyo Zambia itapoteza marafiki wengi.Kwani hata Muwekezaji mkubwa wa Zambia ktk Madini na sekta nyingine nyingi China wamekwisha kwaruzana nae,katika moja ya mikutano yake ya kampeni Sata aliwaita Wachina sio wawekezaji bali ni Wakoloni!
Mkuu Mwawado karibu sana tena sana Mkuu na heshima mbele.............Huyu Sata kwa visasi........ananikumbusha Gen Idi Amin......wakakti mwingine matokeo ya Demokrasia ndio kama tunayoyaona Zambia...........ni kweli kabisa anahitaji washauri makini...........na Tanzania tuna nafasi kubwa sana ya ku-influence............. ninachoomba pia asianze kuua wapinzani wake........