Zambi awa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

TAARIFA zilizovuja kutoka ndani ya chumba cha kuhesabia kura katika uwanja wa sokoine Jijini Mbeya ambako bado matokeo ya uchaguzi hayajatangazwa, zimesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi zmeshinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya.

Zambi kapata zaidi ya kujra 800 na kufuatiwa na Allan Mwaigaga ambaye amepata kura 400 na kufuatiwa na Reginald Msomba aliyepata kura 47.

Habari kamili kesho...

Mtuhumiwa wa rushwa kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa.

Source: Kafulila

Hongera Dhambi!
 
Mkuu tafadhari toa taarifa kamili, kwa mfano
1/Mshindi anatoka kambi ipi ya wapigania urais?
2/Matukio ya aina gani ya fujo yalitokea?
3/Mtindo upi wa kutoa rushwa ulitumika?
 
Ni bora amekimbilia huko mkoani maana wananchi wa jimbo la Mbozi Mashariki walishampiga ban kufika katika jimbo analorisha baada ya tume ya uchaguzi kurazimisha awe mbunge kinyume cha matakwa yao kwenye sanduku la kura.
 
Yule jama hata akipata atajichanganya tuu, maana kwanza ni mla rushwa, halafu ni mwongo, so anaenda kuanda mazishi ya nyinyiem. in short hana uwezo
 
Zambi atakuwa na kazi 2 mojawapo ambazo aliogombania nao uenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya nathubutu kusema wasingeweza. Kwanza kuvunja makudi ndani ya CCm mkoa wa mbeya - makundi hayo yawe ya kisiasa au yale ya kikabila. Kumchagua mnyaki au msafwa mkongwe bado kungeiweka CCM mahala pabaya. Kazi ya pili ya Zambi ni kulirudisha jimbo la Mbeya mjini mikononi mwa CCM. Jimbo hilo limeenda mikononi mwa CDM kwa sehemu kubwa kutokana na makundi ya kisiasa na ukabila ndani ya CCM pamoja na kwamba wananchi walio wengi wanauchukia ufisadi ambao CDM wamejipambanua nao.

Itabidi Zambi ashawishi jimbo la mjini Mbeya linachukuliwa na mwana CCM ambae si Mnyakyusa au Msafwa ili Mbunge aliepo ambae ni Cosmopolitan achuane nae ipasavyo. Tatizo la makabila haya 2 yana mawazo mgando ya kizamani - mawazo yanayobishana na ukweli kuwa Mbeya City ni mji Cosmopolitan. Mbeya City isingefika hapo ilipo kama si juhudi ya ziada ya aina ya watu "wageni" ambao wana nguvu ya umiliki wa raslimali.

Kila la kheri Zambi katika kazi yako ya uongozi. Umekubalika na wa mkoa wa Mbeya watumikie - utawafadhaisha sana ukileta ngonjera za siasa za chuki, ukabila, ufisadi etc.
 
Zambi HATAGOMBEA UBUNGE jimbo la Mbozi Mashariki mwaka 2015 kwa hiyo kajionea kuna "mlo" kwenye nafasi hiyo ya UENYEKITI-MKOA hasa pesa zitakazokuja mwaka 2014 kwenye mchuano wa kutafuta U-Rais CCM!

Sisi Mbunge wetu Dr Mwakyembe mwaka alisema HATAGOMBEA MWAKA 2015(alituambia hivyo kijijini Kasumulu mwaka 2010) lkn sasa juzi kasema tena kuwa ATATOA MAAMUZI kama atagombea au la mwakani!
 
Itabidi Zambi ashawishi jimbo la mjini Mbeya linachukuliwa na mwana CCM ambae si Mnyakyusa au Msafwa ili Mbunge aliepo ambae ni Cosmopolitan achuane nae ipasavyo

Kama Zambi ni mchapakazi;Kwa nini aanze kulikomboa Jimbo la mbali la Mbeya mjini ili hali Jimbo la karibu yake kabisa la Mbozi Magharibi linaongozwa na kijana Silinde wa CHADEMA?Kwa nn asianze na hili then aende la mbali?

Hapo sijakuelewa kwa kweli!
 
Kuna jambo la kujifunza kwenye hizi chaguzi. kwanza wingi wa wapiga kura: Hapa kuna ujumbe unatumwa kwamba kama CCM iwaweka wagombea watakaochaguliwa na wanachama wao badala ya kutumia vikao vya NEC kuchakachua, basi bila shaka tayari wanao mtaji. CCM ina mtandao wa wanachama wao na ni kujidanganya kusema bila vyama vingine kuunda mtandao kushindana na mtandao huo itashinda.

Sehemu nyingi ambako wabunge wa vyama vingine waliwashinda wale wa CCM ni kwa sababu CCM yenyewe ilipasuka. Taadhari yangu kwa hivi vyama vingine wasitegemee mipasuko ya CCM kushinda bali watengeneze mitandao ya vyama vyao kushinda!!
 
Mkuu tafadhari toa taarifa kamili, kwa mfano
1/Mshindi anatoka kambi ipi ya wapigania urais?
2/Matukio ya aina gani ya fujo yalitokea?
3/Mtindo upi wa kutoa rushwa ulitumika?

ndo akili yako inavo kutuma?
 
Mtuhumiwa wa rushwa kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa.

Source: Kafulila

Hongera Dhambi!

Sasa ndio hivyo, Mwenyekiti wa Mkoa ndio huyo aliyekuwa anaomba rushwa toka kwenye halmashauri; hapo utategemea uongozi wa aina gani? Amesoma alama za nyakati kuwa last time kwenye ubunge alichakachua na kuwa come 2015 hananafasi tena; akaona afadhali aponee huku kwenye chama cha magamba!!
 
Kama Zambi ni mchapakazi;Kwa nini aanze kulikomboa Jimbo la mbali la Mbeya mjini ili hali Jimbo la karibu yake kabisa la Mbozi Magharibi linaongozwa na kijana Silinde wa CHADEMA?Kwa nn asianze na hili then aende la mbali?

Hapo sijakuelewa kwa kweli!

nayo pia ni option
 
Back
Top Bottom