Zamani nilikuwa naamini kuwa...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
1.Rais na Serikali yake ni watu makini wanaopigania kila uchao ustawi wa nchi hii
2. Viongozi wa Serikali hawawezi kuiba mali za watu wanaowaoongoza kama ilivyo kwa baba kutoiba mali za familia yake
3.Vyama vya siasa ni vyama vilivyojaa watu wakorofi na wapinga maendeleo
4.Popote wapinzani watakaposhinda uchaguzi patatokea vurugu na maendeleo yatadumaa
5.CCM haitatoka madarakani
6.Vyuo Vikuu vyetu ni chachu ya mandeleo ya sayansi na teknolojia kwa maendeleo ya nchi yetu
7.Wanafunzi wa vyuo vikuu ni mwanzo wa fikra mpya za ukombozi na uongozi
8.Elimu ndio ufunguo wa maisha
9.Kuna mihimili mitatu ya Serikali: Dola,Mahakama na Bunge ambayo kila mmoja unafanya kazi zake kwa kujitegemea na kwa uhuru
10.CCM na Serikali yake yaweza kufanya Mkutano wa hadhara popote Tanzania na kushangiliwa kwa hoja zake za kimaendeleo

Na kadhalika...Kwasasa naamini kinyume chake.Wewe je?
 
Back
Top Bottom