Zamani na sasa

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
549
185
WANA JAMVI, NIMEIPATA HII KUTOKA FB, NIMEIPENDA, TUIJADILITangaza Mazuri ya Nchi, Onea Aibu Udhaifu!

Kuna semi nyingi za Kiswahili ambazo kimsingi zinasisitiza umuhimu wa jamiikutimiza wajibu wao kwa kufanya yaliyo sahihi, yaliyo mema na kuiacha jamiiiwahukumu kwa matendo yao.

Semi nyingi zinatusisitiza tuwe wanyenyekevu kwajamii na tusiwe na majivuno ama kujisifu tunapotenda mema. Semi hizo ni kamavile; “chema chajiuza kibaya chajitembeza, tenda wema wende zako usingojeshukurani, sifa wakusifu ukijisifu wajikashifu, n.k. Sina imani sana kama semihizi zina nafasi ileile katika dunia yetu ya leo kama ilivyokuwa hapo zamaniama jamii inahitaji kufanya masahihisho ili kufanya semi hizo ziendane namahitaji ya dunia ya leo.


Nimechagua semi hizi chache kwa sababu zote zina maudhui ambayo kiasifulani yanashabihiana na mada ambayo nakusudia kuitolea maoni yangu na kushauriwatanzania wenzangu kutafakari tabia zetu ama matendo yetu sasa na mustakabarigani tunakusudia kuufikia, kwa mtu mmoja mmoja na kama taifa kwa pamoja.

Tofauti na siku za nyuma, dunia yetu ya sasa ina mabadiliko makubwa hasakatika tabia za watu kufanya maamzi. Leo hii hakuna nafasi kubwa saana ya watukufanya maamzi kwa majaribio. Yaani kujaribu kwamba nifanye jambo fulani kamanitakuwa nimekosea basi nitasahihisha hivi au vile. Maamzi ya aina hii yanaghalama kubwa sana ndio maana nafasi yake ni ndogo kwa watu kufanya majaribio.

Gharama ambayo inaweza tokana na maamzi mabaya ni kubwa ila ina mbadala.Mbadala wake ni kutafuta taarifa sahihi na hivyo kupunguza makosa katika maamzi.


Katika misingi hii basi maamzi ya watu leo hii yanategemea sana kuwepo nataarifa sahihi ambazo zinawezesha watu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kufanyamaamzi sahihi na kwa wakati sahihi. Hapa ndipo ulipo msingi wa hoja yangu...tofauti na ilivyokuwa zamani, sasahivi kuna umuhimu mkubwa ama tuseme ulazimawa sisi, kama mtu mmoja mmoja na kama jamii kwa pamoja, kwa upande mmoja, kutafuta taarifa sahihiwakati tunataka kufanya maamzi, ili tuzitumie kufanya maamzi sahihi na yenyemanufaa kwetu.

Kwa upande mwingine tunalazimika kujenga uwezo, umahiri na ueredi wa kutoataarifa sahihi na shawishi zinazotuhusu ili kufanya wengine wafanye maamzisahihi lakini yenye manufaa kwao na kwetu. Sasa ambalo limenisukuma kuliandikaleo ni hili la pili, yaani la kutoa taarifa sahihi na shawishi zinazotuhusu...kwa kifupi, kujitangaza.

Hoja yangu ni kwamba, badala ya kusema chema chajiuza kibaya chajitembeza,dunia yetu ya leo inatutaka tukitangaze chetu hata kama ni chema. Kuna vingivyema na kuna vingi vibaya ambavyo pia vinafananishwa na vyema. Tusipokitangazachetu hata kama ni chema, watu hawatakijua badala yake watachagua kibaya kwasababu wenyenacho wamekipamba na kukiita chema. Tusijiamini tu kwa sababu tunakitu cha thamani tukaamini kuwa watu watajua thamani yake na kukinunuabila ya kuwatangazia kuwa chetu kinaubora huu na ule na kuna faida hii na ile kununua chetu. Hili ndio badiliko lililopo katika jamii ya leo na jamii iliyokuwapo zamani.

Msingi wa hoja yangu unalenga kuwasisitizia watanzania wenzangu kuwa tunadhima kubwa kuyatangaza mazuri yetu miongoni mwetu wenyewe kwa wenyewe na njeya mipaka ya nchi yetu. Hili lina umuhimu sawa kwa ngazi ya jamii, lakini piakwa mtu mmojammoja. Ni muhimu kuyaandika, kuyatangaza, kuyasifu na kuyapambayaliyo yetu. Hata kama ni mazuri kiasi gani, tusipoyatangaza sisi wenyewe,kuyaandika na kuyapamba kwa ufundi na weredi, hakuna atayefanya kwa niaba yetu,zaidi sanasana, wengine watayatekanyara na kuyafanya yao. Kutangaza mazuri aukwa maneno mengine kutangaza mafanikio yetu ni njia moja ya kutangaza jinaletu, hivyo kujenga kuaminika, kujulikana na kuheshimika.

Naandika haya kwa sababu ninachokiona sasa kwa kiasi kikubwa nchini kwetutuna tabia ya kuona na pengine kuamini kuwa jambo zuri linapofanywa na mmojawetu basi huo ni wajibu wa mja kufanya mema, hatuliongei wala kusifu. Ilaikitokea mmoja wetu amekosea basi ni nongwa, atasemwa, kusakamwa na kulaaniwakwa njia zote za mawasiliano na kupewa majina yote mabaya!!!!!!!!

Nchini kwetu tuna mambo ama vitu vingi vizuri ambavyo vinahitaji sanakutangazwa zaidi na zaidi kwa njia tofauti tofauti ili sio tu yajulikaneduniani, bali pia yatujengee ari sisi wenyewe kuona kwamba ukifanya zuri basijamii italitambua. Nionavyo mimi, watanzania hatufanyi hivyo kwa kiasi kinachotakiwa. Lakini pia, kinyume chake matatizo yetu tunajitahidi sanakuyatangaza na kuyaweka wazi – pengine kwa kutaraji saana hisani ya wafadhilina misaada.

Ni jambo la kawaida kuona kwa mfano waandaaji wa vipindi vya luningawakishindana kuandaa vipindi vya ukimwi na kuonyesha ukubwa wa janga hilonchini mwetu. Yanapotokea mauaji ya kutisha kama ilivyotokea Musoma mwanzonimwa mwaka huu, vyombo vya habari vitatoa taarifa na kuandika makala tena kwakushindana na kufufua historia nyingi za mauaji ya namna hiyo kana kwamba hiyoni asili ya mtanzania kuendesha mauaji ya kutisha na kana kwamba nchi hiihakuna zuri hata moja. Mauaji ya albino yanavyoandikwa na kutangazwa yanafunikamazuri yote yaliyopo na yanayotendeka nchini kwetu kiasi kwamba waliopo nje yanchi wanaona sisi ndio wajinga wa kutisha kabisa duniani na hatufai “kuoka wala kulumagia”.

Kwa mfano kuna hili ambalo mimi naamini ni zuri na linastahili sifa kamasio kulipamba kwa maua ya kila rangi na harufu nzurinzuri... la kujenga chuokikuu cha Dodoma kwa kutumia fedha za ndani... kutoka mifuko ya hifadhi zajamii. Ninaamini hili ni zuri na ni mabadiliko makubwa katika mtazamo wetu wa kujiletea maandeleo yetu na kujitegemea. Lakini inanistaajabisha kusoma katika mitandao lawama na shutuma nyingi kuliko sifa kuhusina na mradi huu. Wengine wanalaumu matumizi ya fedha za wafanyakazi kujenga maghorofa, wengine wanalaumukujenga chuo bila ya kuandaa waalimu wa kutosha... ali mradi shutuma zitolewena hakuna kusifu. Kwa kweli ni vyombo vya habari vya umma tu ndio nimeonawamesifu mradi huu. Vyombo binafsi, matamshi yetu binafsi yanaona hili nijukumu lake serikali, inapaswa kufanya hilo kama wajibu... tusifu ili iwe nini!

Mimi kwa mtazamo wangu hili ni jambo la sifa kwamba sasa tuna uwezo kwamba fedha za ndani zinatumika kujenga miundombinu, tena elimu na tena elimu ya juu. Kwa imani yangu kitendo hiki kilistahili sifa zaidi na zaidi na kutangazwa zaidi na zaidi. Kwanza kinajenga picha nzuri ya nchi yetu nje, lakini hata sisiwenyewe ndani kinatujengea ari na kuwa na mtazamo mpya wa mustakabari wa kutafakari safari yetu kuelekea katika taifa linalojitegemea.

Tanzania inaongoza kuwa na mbuga mbili za kwanza kwa ukubwa Afrika (Ruahana Serengeti) na mlima mkubwa kuliko yate Afrika na maajabu kadhaa ya kufanyatuwe na mengi ya kuieleza dunia lakini cha ajabu jukumu hili lipo kwa bodi yautalii pekeyao, wengine tupo pembeni na hatuhusiki. Hebu tujigambe na tupazesauti zetu watanzania kutangaza mazuri yetu!

Hebu tujenge tabia ya kujengana moyo watanzania! Nina imani tuna uwezo wakufanya vizuri zaidi katika nyanja nyingi lakini tu tunakuwa wavivu na aridhaifu kwa sababu hatujengani moyo.

Mwandishi mmoja wa saikolojia ya watoto dk. James Dobson aliandika nimakosa makubwa kutaja udhaifu wa mtoto wako akikusikia. Utamjengea imani kuwayeye si chochote na hata wewe mzazi wake unafahamu hilo... Kwa maana hiyoutakuwa umeua kabisa ari yake ya kuthubutu na kupambana na changamoto zamaisha.

Kwa bahati mbaya dhambi hii ya kujidharau, kudharauliana na kudharau kilakilicho chetu, tunaifanya tena kwa kiasi kikubwa. Washiriki wetu katikamashindano mbalimbali ya kimataifa ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa dhambihii na haishangazi kuona timu zetu kila mwaka hazifanyi vizuri. Wote tunaaminikuwa sisi hatuwezi hivyo hata wawakilishi wetu wanaenda katika mashindano yakimataifa mioyoni mwao wakiwa wameshashindwa wanabaki kujitetea tu iliwapunguze idadi ya magori.

Huu ni udhaifu ambao kama watanzania tunapaswa kuukemea katika nafsi zetuili tuweze kushika nafasi tunayostahili katika dunia hii ya ushindaji naulaghai.

Tukosoe uoza kwa nguvu zetu zote na tuwazomee wanaofanya uoza ili waoneaibu, lakini pia mazuri yanayotendeka tuyatambue, tuyatangaze na tuyaenzi ilikuwapa moyo wanaofanya mazuri ili waendelee kuyafanya, wawe na ari kufanya zaidi na wengine waige.

Watanzania tujadiri!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom