Zaidi ya Suti: WikiLeaks yafunua mgongano kati ya JK, Kapuya na Gen. Waitara...

Kurugenzi ya Ikulu imefanya bonge ya miscalculations, wikileaks documents mpaka zitakapokuwa released zote sijui watatoa press release ngapi?

Hawatajibu tena, basically tactically wnaweza kusema kwamba Ikulu haiwezi kuhangaika kujibu kila cable kwa sababu kimsingi cable hizi hazna credibility kama yule mdada wa Ki Guinea aliyechakachuliwa na DSK.

Unless Waitara aongee wakijibu watakuwa wanaalia makaa tu.

Hapa anatakiwa kutafutwa Waitara atuambie kwa nini alimtilia ngumu rais wake, kama atataka kuongea kunaweza kuwa na bombshell hapa.
 
Hatuna uhakika kama CDF alitoa sababu za kusisitiza kuwa ni muhimu wakasaini Status of Forces Agreement (SOFA) kabla ya kuanza African Contingency Operations Training and Assistance (ACOTA). Inaonekana wamarekani walikuwa wakisisitiza kuwa sio lazima kusaini SOFA kabla ya kuanza mafunzo kitu ambacho CDF alikuwa hakubaliani nacho. Labda tujiulize kwa nini CDF aliona ni muhimu kuwa na makubaliano ya SOFA kabla ya kuanza utaratibu wa mafunzo wa ACOTA? Na kwa nini wamarekani walikuwa wanataka kuharakisha mafunzo kabla ya kusaini huo mkataba?

Hapo kama kuna uChifu Mangungo fulani Waitara kaukataa vile.

Tatizo letu tunaingia vitu bila kuangalia mikataba vizuri halafu baadaye tunalia ( umeme, madini etc).

Inawezekana kabisa SOFA ikawa si requirement, lakini sie kama a sovereign state tungeweza kuifanya kuwa requirement kama inatulinda, na hiki ndicho kinaonekana kama alichotaka Waitara, Wamarekani mara nyingi hawataki ku deal na mtu mjanja zaidi yao, wanataka domination.

Sasa mimi nikisikia Mtanzania yeyote anagoma kuingia kitu kichwa kichwa bila kuangalia mikataba kwa umakini, hususan wageni wanaposema mikataba si muhimu, nakua naona ni bora kuwa kwenye upande wa skepticism ya Waitara kuliko kuwa katika position ya kuingia kichwa kichwa bila scrutiny halafu kulia baadaye.

Tushaona mifano mingi sana, hatujifunzi tu?

On the other hand

How sincere are the Americans when they assert that attaching reciprocity to SOFA would have elevated it to a treaty level of agreement, requiring congressional approval and possibly jeopardizing speed or the entire training in the usual congressional political muckraking? Are we being overly sensitive here? Kuna ukweli hapo? Au ni gia ya tu ya kukataa reciprocity?
 
kumbe Gen mwamunyange ni kibaraka?. Kapuya said to ambassador, "umefanya vizuri kumshirikisha!". This means ni kibaraka, na hii inatisha kwani hata chief of staff wake shimbo ni walewale! Jeshi letu wanaliweza watu wa Mara, they ar intelligent na wana misimamo, nashangaa hawa wametokea wapi! ..jeshi ni entity inayojitegemea km ilivyo bunge au mahakama..lazima iwe na maamuzi yake bila kuingiliwa! naionea huruma sana nchi yangu!
 
Sishangai hii cable na yaliyomo. Mara nyingi presidential appointees wana mtindo wa kuendeleza utiifu wao kwa aliyewateua hata kama ameshatoka ofisini; Gen. Waitara ni mteule wa Mkapa na wala sishangazwi na jeuri yake kwa Amirijeshi Mkuu mpya. Na hili lilionekana karibu katika kila idara hadi ikafikia maagizo mengi ya JK yalikuwa yanadharauliwa.

@Mwanakijiji et. Al., kama mlifikiri tunaongozwa na Malaika basi; kwa mujubu wa hizi cable, viongozi wetu ni binadamu wa kawaida. Kwa taarifa yenu, zingemwagwa cable zianzoelezea kipindi cha Mzee Ruksa, ilifikia hadi wanajeshi kukataa uteuzi wake wa CDF mpya!
 
Ohhhhh! Si nilisema mwanzoni jamani kuwa hawa Wikileak ni maji marefu hawa, na si mtandao wa kushindana nao hata kidogo; nilisema Magogoni wangekaa kimya na haya mambo, ona sasa ngoma nzito iliyokuja, tena inayohusu masuala ya usalama wa nchi. My take: Nadhani umefika wakati muafaka sasa kwa wahusika kujiengua na kuiacha nchi ichukue mwelekeo mwingine, vinginevyo, hapa tutasoma mpaka rangi za nguo za ndani wanazovaa (Nikiwa na maana kuwa, tutasoma siri ambazo hazikustahili kabisa kuwekwa hadharani, halafu sijui watatuambia nini watanzania.) Kwa jinsi mambo yanavyoenda, ya Shimbo yanakuja.
 
Kutoka kwenye one of the cables: Nadhani si kila kilichopo kwenye wikileaks ni sahihi.Mfano hilo la kuoa cousin wa Juvenal .



Kikwete's Biographical Notes
----------------------------

6. (C) Kikwete represents the "young Turk" segment of
the CCM party. He is popular, politically adroit,
charismatic and very ambitious. In socially
conservative Tanzania, however, Kikwete's relative
youth - he is 55 - has worked against him. So has his
playboy reputation. As the party has increasingly
emphasized experience and education, Kikwete has a
built an impressive resume. Since 1995, Kikwete has
been Foreign Minister and also the MP for Chalinze
Constituency. Previous government positions include
Minister for Finance (1994-95), and Deputy Minister,
then Minister for Energy, Minerals and Water (1990-
94.) For the twenty years before his government
service, Kikwete served in various positions in the
CCM party, and in its predecessor party, TANU.

7. (U) Kikwete comes from the small town of Msogo, on
the coast near Bagamoyo. He has a BA in economics
from the University of Dar es Salaam.

8. (C) An able politician, Kikwete is a somewhat
unenthusiastic administrator. On Embassy row, his
Foreign Ministry has a reputation for being
understaffed and minimally responsive. Kikwete
himself is personable, and conveys the impression that
he will at least consider the views of foreign
diplomats. Kikwete has signaled that he might discuss
signing an Article 98 agreement with the US; the
current President Benjamin Mkapa has firmly closed the
door on any agreement for the remainder of his
Presidency. For years, observers of the Great Lakes
conflicts have considered Kikwete to be virulently
pro-Hutu. Rumors that he was facilitating arms
transfers to Burundian Hutu rebels persisted, but have
never been substantiated. Kikwete's marriage to a
cousin of former Rwandan President Juvenal Habyarimana
may have fueled these rumors, which are now fading as
the Burundi conflict winds down.
 
The Ambassador assured the Minister that we understood the temporary obstacle President Kikwete faced and that we looked forward to
starting ACOTA training in August. END SUMMARY.
Rweyemamu asikurupuke tena kujibu, niliwaambia hawa jamaa wanatujua zaidi ya tunavyojijua sisi, kuna member mmoja ameanzisha thread eti Marekani ituombe radhi kwa suala la suti ni wehu tu huo, hilo kwao ni jambo dogo sana ngoja watoe dili za silaha kwenda DRC ndipo akili itawarudi.
 
Democracy at its best. Mlitaka wakae kama ma zezeta? Kwani ni kampuni binafsi hiyo? Mnanchekesha, hata kampuni zina kuto-kukubaliana.

Halafu hiyo habari ni ya lini? history.

...hata suit huchakaaa na kugeuka matambala, hivyo kuwa history! Lakini kamwe hutosahau kuinunua...!!!
 
ndugu yangu!hii pia kali, hebu ianzishie thread mpya.. kumbe jk alikuwa akisupply silaha BURUNDI? Wajibu na hili. mods iwekeni kwa thread mpya
 
Hivi General (rtd) Waitara yupo wapi wakati huu?

Hivi kuna uwezekano wa kumpata na kutujulisha ni kwanini alikataa mpango wa ACOTA?

Hivi Gen Davies na Lt. Gen Shimbo wanaelewa kwa kina ni nini madhumuni ya mpango ACOTA?
 
'Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianzan kuumbuana kuna atakayepona?' Lowassa. 'Muda ukifika nitatoa tamko' Lowassa. 'Kwani nimefanya nini hadi mnataka kunifukuza CCM kuna kitu gani ambacho nimefanya kisha wewe JeiKei hukijui' Lowassa. Vuta pumzi kaka kama yeye anavyotuhumiwa na yeye sasa kasababisha na wenzie kuumbuliwa, ; swali, nani atamvua gamba mwenzake? Mwingine 'Msekwaa' keshaumbuliwa na matamaa yake sasa yuko kimya pua limemvimba tu kama kitimoto. Vuta pumzi tu kaka mengi utayaona, hawa magamba wana memngi ambayo umma haujui...
Na hii hapa "serikali ina ugonjwa wa kufanya maamuzi, Watanzania wnanjua, dunia inajua"
 
Rweyemamu asikurupuke tena kujibu, niliwaambia hawa jamaa wanatujua zaidi ya tunavyojijua sisi, kuna member mmoja ameanzisha thread eti Marekani ituombe radhi kwa suala la suti ni wehu tu huo, hilo kwao ni jambo dogo sana ngoja watoe dili za silaha kwenda DRC ndipo akili itawarudi.

Mbona Hillary Clinton kashaomba radhi dunia nzima kuhusu hizi cables?

Tujue kutofautisha kwamba haya ni mawasiliano ya ndani ya serikali ya Marekani, na wala Marekani haikuwa na nia ya kuyachapa wazi, ni kwamba wamekuwa violated mawasiliano yao yakachukuliwa bila wao kutaka. Kwa hiyo ukisema "watuombe radhi" unakuwa kama nasema Wamarekani wametoa statement publicly kwamba Kikwete kanunuliwa suti.

Tunahitaji Wikileaks yetu tuone maafisa wetu wanavyochakachua mitandao ya serikali kutumiana pornographic materials. Usalama wa taifa kina Mudhihir Mudhihir ilikuwa ndiyo kazi yao kubwa kwenye computer.
 
Unadhani Julian Asange wa Wikileaks anajua kama tuko kwenye zoezi la kujivua gamba?
na hata kama anajua labda hayuko interested na hoja za magamba na kama ana interest atafumua pale atakapo ona inafaa!!!
 
Tatizo si kushirikiana na Marekani tatizo mikakati na mwenendo mzima wa watu watako deal na Markeani wametayarishwa kukabiliana katika majadiliano nao.Na kuelewa kila kipengele cha makubaliano ya ushirikiano na wadau hao.

manake dunia hii kwa sasa tupende tusipende hatuwezi kukwepa kushirikiana nao,Mwalimu na misimamo yake bado alishirikiana na Wamaerekani.Lakini Je tuko tayari kwa upeo kuwa washirika na wadau wa kimaendeleo na kibiashara na Taifa hili kubwa duniani.

Kwa upande wetu kama watanzania wajibu kwetu ni kuwa na vichwa [Watu Makini] wanaojua na hata kuwacheza shela pindi inapobidi hawa jamaa kwa kuwa wao nao wanania yao binafsi kwenye mashirikiano nasi.Nasi tutumie nia zetu binafsi kufanikisha yetu hata kama ni kwa ghalama za migongo yao.Ndipo hapo pia nasi tunapswa kuthibitisha kuwa tuna maliasili watu think tank yenye upeo unaotengeneza win to win situation.

Nasikia Mwalimu alipatwa kuulizwa swali na wamerkani kuwa juna umbali gani kati ya Tanzania na Dar es salaam,na Mwalimu kabla ya kujibu nae akaulizaa swali kuwa "kuna umbali gani kati ya Washington DC na United state of America".Swali kama hili ukilitizama unaweza kuona ni mdhaha lakini kwa wenzetu ni kipimo kupima uwezo wa mhuiska katika kufikilia.Pata picha jibu la Mwalimu kisha tegemea muda si mlefu ataingia kwenye kikao cha majadiliano [negotiation] na kuweka makubaliano na wadau ya kitaifa tegemea uzao wa majadiliano hayo utazaa nini. Tena wakati wa Mwalimu Majidilaiano [Negotiation] hayakuwa na taaruma ambayo kwa zama hizi ni swala la taaluma dalasani.Hivyo kama Taifa hatuna budi kuwa na Watu makini wanaolelewa na kukuzwa kwa kusomeshwa ili kuja kuwaza na kutoa majibu ya shida na maendeleo kwa niaba ya faida ya UMMA.

Hapo kwenye red: Kwa nini Tanzania ni masikini?
 
Nimeisoma hii topic vizuri sana, mi nipo tofauti kidogo na wachangiaji wengine. Ningependa kujua kwanini Waitara aligoma, na serikali ikaheshimu na kusema inasubiri kwanza astaafu then ndo program ianze. Kama mkuu wa majeshi amegoma, maana yake kuna sababu za msingi na bila shaka alizitoa na serikali ilimuelewa. Kinachonishangaza kama mtu ana sababu za msingi na amezitoa (Kama alifanya hivyo) na serikali kama serilkali akazielewa, kweli dawa yake ni kumsubiri huyo mkuu wa majeshi astaafu????
kwa nini ilikuja kipindi cha hiki cha kikwete na sio walio mtangulia?? ya wezekana pia hii programme waitara aliona kuwa haina tija!!
 
CCM ingekaa pembeni ijipange upya na baada ya miaka kumi irudi bila akina Kingunge, Malechela, Pius Msekwa na wazee wa DSM. Heshima ya nchi inawekwa kwenye mnada namna hii wakati bado watoto wetu wadogo hivi watakuta kitu gani cha kuwafanya wajivunie Tanzania. Je akina Mkwawa, Isike, Sina, Chabruma, Songea wa miaka ijayo watakuwa akina nani wakati wajukuu zetu watakaposoma historia ya nchi yetu miaka 100 ijayo? Je watasoma historia kwa fahari au kwa kulia kama inavyosomwa historia ya Adolph Hiltler,Benito Musolin, Stalin, Karl Peters na waovu wengine?.

Hiki kizazi tunataka kukirithisha nini hasa kwani sisi tunaishi kwa sababu waliotangulia waliamua kutuwekea akiba ya rasilimali tulizo nazo. Je tunataka harakati za uhuru zije kuanza tena miaka 100 ijayo kwa sababu tu tumeshindwa kuwa enzi babu zetu waliopigana na wakoloni kwa kujua hawatutakii mema ila sisi eti leo tumewakumbatia na kuwaona wa maana sana ?
 
Mbona Hillary Clinton kashaomba radhi dunia nzima kuhusu hizi cables?

Tujue kutofautisha kwamba haya ni mawasiliano ya ndani ya serikali ya Marekani, na wala Marekani haikuwa na nia ya kuyachapa wazi, ni kwamba wamekuwa violated mawasiliano yao yakachukuliwa bila wao kutaka. Kwa hiyo ukisema "watuombe radhi" unakuwa kama nasema Wamarekani wametoa statement publicly kwamba Kikwete kanunuliwa suti.

Tunahitaji Wikileaks yetu tuone maafisa wetu wanavyochakachua mitandao ya serikali kutumiana pornographic materials. Usalama wa taifa kina Mudhihir Mudhihir ilikuwa ndiyo kazi yao kubwa kwenye computer.


Usidanganyike mkuu, huu waweza kuwa mpango wao wa kuwachafua au kuwafumua maraisi ili wachukiwe na wananchi wao kwa malengo yao. Hivi kweli M7 ni msafi kuliko JK? Mwai na Raila ni wasafi kuliko JK? No! Hawa watu wanahitaji kutuvuruga tu ili wachukue maliasili zetu kiulaini. Pamoja na tofauti zetu za kisiasa, hawa wamekuwa wapinzani wetu wa tatu ambao wanachonganisha pande mbili za kisiasa (Utawala na Upinzani) ili tuchafuane. Naomba wananchi wote wa TZ, pamoja na tofauti zetu, tutumie jicho la tatu kuwaona hawa watu.
 
Jamani kweli kikwete anaendelea kutuuza kila siku, general waitara alikuwa anatetea maslahi ya inchi yetu kama alivyo apa kuilinda katiba ya inchi yetu. Americans wameshamdump rais zamani na sasa lazma atakuwa anaelewa waitara alikuwa ana manisha nini, general waitara we support you

General Waitara gombea uraisi, wewe ni mzalendo na wala huburuzwi na mataifa makubwa.
 
Democracy at its best. Mlitaka wakae kama ma zezeta? Kwani ni kampuni binafsi hiyo? Mnanchekesha, hata kampuni zina kuto-kukubaliana.

Halafu hiyo habari ni ya lini? history.
hata kama ikiwa ya miaka 50 iliyopita lakini ina impact kwa sasa lazima isomwe na hatua zichukuliwe!!!!! pia nina mashaka na uelewa wako juu ya umuhimu wa historia katika nchi yako.
 
Back
Top Bottom