Zaidi ya bilioni 25 zatafunwa; Watendaji waanza kuwajibishwa!

Kilichobaki tuandamane tudai pesa yetu. Nadhani tuanzie na majumbani mwao halafu tunamalizia wizarani kitaeleweka. Hawa wanatufanya sisi mbumbumbu mzungu wa reli. Mimi nasema wote mliolifilisi taifa hili na bado mnaendelea kulifilisi basi mwisho umefika kwani dalili sasa zinaanza kuonekana. Tukose wote. shwain!
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo hili ni sugu huko wilayani kwa miaka kadhaa na serikali pamoja na kuendelea kuongeza pesa za ruzuku kwa wakulima lakini wanaofaidika ni wafanyabiashara wa katikati pamoja na viongozi wa siasa na watendaji wengine wa serikali.

Kwa uchunguzi wangu mimi kwenye wilaya moja ninaona tatizo kubwa ni uongozi wa mikoa na wilaya ambao unashindwa kuwaandaa wakulima ili wajue haki zao katika hizo ruzuku na pia wanashindwa kufuatilia kujua hiyo ruzuku kama imetumika ipasavyo.

Hili halina tofauti na yale mabilioni ya Kikwete, ni mtindo ule ule wa nia njema ya serikali kutekwa na wajanja katikati kwa faida yao.

Waheshimiwa wabunge wangelikuwa wanawajibika kwenye majimbo yao, wana uwezo mkubwa kwa kushirikiana na viongozi wengine kama wakuu wa mikoa, wilaya, kata na vijiji kuhakikisha hii ruzuku inafika kwa mlengwa.

Hayo mnayosema ni sehemu ndogo tu ya ufisadi ambao unafanywa kwenye ngazi ya wilaya mpaka vijijini. Ukiingia kwenye pesa za kuendeleza elimu, kuendeleza afya, pesa wanazopewa NGO kwa ajili ya matatizo mbalimbali nk. Utagundua zaidi ya asilimia 50 inachotwa na wajanja.

Sioni dawa ya haraka zaidi ya wana harakati mbalimbali ambao wanaamini katika maadili na utumishi bora kujihusisha moja kwa moja na shughuli hizi. Kwa mfano suala la ruzuku, kikundi chochote kilichotimiza masharti kinaweza kuisimamia na kusaidia kuwaelemisha wananchi badala ya kuwaachia matapeli.

Ndio ni vizuri tukiyaweka wazi haya matatizo mbalimbali ili labda serikali ichukue hatua, lakini kama una uzoefu wowote wa mambo yanavyofanywa kule wilayani, basi hii vita nayo huenda itatushinda.

Ushauri wangu njia pekee bora ni kushiriki kule kwenye grassroot kuhakikisha hiyo ruzuku au pesa zingine zote zinaenda kwa walengwa, vinginevyo kila mwaka tutakuwa tunaongelea jambo hilo hilo.

Mimi ningetegemea wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi walisimamie hili jambo kwa faida ya wakulima na wao wenyewe pia. Bahati mbaya wengi wao hata hawajui nini kinaendelea kule vijijini.

Binafsi nilikuwa very dissapointed na jinsi viongozi wa wilaya na mikoa walivyoshindwa kusimamia yale mabilioni ya JK na hizo pesa zikaishia kwa walanguzi na kuwatajirisha watu wa bank na wanasiasa. Wabunge walijua hizo pesa zipo, kwanini walishindwa kuwaelemisha na kuwaandaa watu?

Matatizo ya Tanzania ni makubwa mno kuliko tunavyoweza kuongea hapa, uongozi bora haupo, utendaji mbovu umetawala kila sehemu, jamii nzima ni kama imegeuka kuwa ya wezi na wasanii. Bila kubadili hii culture mbovu, tutaendelea kupoteza mabilioni ya pesa kila siku.

This topic is a shocking story than any topic I ever red(read). I do not imagine such a nation how can it exist!! kweli hata mwili unasisimka! For me is like the end of my world!! I lost hope.
 
Petition ya kumtaka mkuu wa mkoa ajiuzulu iko wapi?
we kwani ujaisoma hiyo post yote, hii tena si ngoma ya rukwa tu kumbe na mikoa mingine chungu mtele sio billioni saba tena sasa ni 25.

sasa kama ni petition ni ya Mh.Raisi watu wanaanza kupoteza total confidence nae na bora ungei anzisha tu hiyo petition ya raisi ku-resign mi naona kama vile hawa jamaa wanachelewa.
 
Petition ya kumtaka mkuu wa mkoa ajiuzulu iko wapi?
GT when you see such things happen is only because we have weak presidents. strong and accountable presidents will want to know the outcome of their efforts by making followups.

He recognized that ambulance he was giving was to a wrong person, how can't he recognize that such big amount of funds are just stolen?
 
hakuna cha ajabu hapo,kama wanashindwa just to manage pesa za jengo moja kama la BOT au kununua generator za richmond wataweza vipi hii project ya nchi nzima....bila kujenga strong institutions za kusimamia pesa zetu na sheria zilizopo tutakuwa tunapoteza billions na kulaumiana kila siku.
 
Tatizo la Tanzania ni tatizo la kimfumo, mtanisema ama kunichukia lakini tatizo la Tanzania ni Wazee.

Wazee wanahitajika kuondoka kwa wakati mmoja, vinginevyo Tanzania haitatibika miaka nenda miaka rudi. Labda aje atokee kiongozi dikteta mustaarabu kitu ambacho si rahisi kumpata kiongozi wa namna hiyo kwa hali iliyopo sasa.

Tatizo wazee wamegubikwa na mentality ya kikoministi ndani ya ubepari, hivyo kasi yenyewe ya kibepari ina wa control badala ya kui-control kasi ya kibepari.

Mtasema vijana waliopo wamefanya nini? ni kweli hawawezi fanya kitu wakiwa wamezungukwa na wazee wakumunisti wenye miendo kasi ya kibepari.
 
Kama kuna jambo ambalo sitaki kusahahu wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ni ku profile na kufanya analysis ya thinking pattern ya mafisadi ili kuweza ku predict next moves zao.

Nakumbuka siasa za kupakana kinyesi zilishamiri kipindi kile kashfa zimepamba moto na ikapelekea kurupushani kubwa sana tu zilizoenda kuanzia kwa mtikila na hadi kanisani kwenye kwaya nk....Move niliyoiona ikilenga kupakaziana ili kuneutralize.

Kimsingi ninachojaribu kusema hapa ni kwamba inawezekana kabisa mind set ile ile bado inafanya kazi,na hivyo harufu ya kinyesi/Ufisadi,imetapakazwa....Sidhani kama ni kwa bahati mbaya.

Kuna mawili hapa;kwanza ni uwezekano wa kuneutralize kashfa za ufisadi kwani sasa si kwamba flani na flani tu ndo mafisadi,sasa ni wengi. Na kwa mwananchi wa kawaida,watu wa karibu watakaowalaumu ni wenyeviti wao wa vijiji madiwani nk....Tena hata kama ni mwananchi mmoja vs Diwani ama Mwenyekiti wa Kijiji,mwananchi anamwangushia lawama mmoja collectivelly kwa ku refer hayo mabilioni,yani mwananchi anaweza kumlaumu Diwani mmoja kwa kula mabilioni,wananchi hawana uwezo wa kutenganisha hayo,hilo linapelekea pointi yangu ya pili kwamba sasa serikali inakuwa imepata nafasi ya kujisafisha kwani wigo wa kuwashughulikia dagaa wadogo ni mkubwa na hivyo serikali kuonekana kuwa inafanya kazi dhidi ya ufisadi kuelekea uchaguzi mkuu baadae mwaka huu.

Ni kweli kuwa jamii yetu iko corrupted lakini sidhani kama hili ni bahati mbaya kwasababu manufaa yake kisiasa ni makubwa zaidi kwa wale mafisadi papa....Sijui tofauti kati ya fisadi papa na nyangumi ila nazungumzia mafisadi wale waliokuwa kwenye fikra za wananchi wengi kutokana na kashfa zilizoweza kujulikana miaka ya hivi karibuni.
Ngoma nahisi imetokaa juu,mark ma words guys.
 
Tatizo la Tanzania ni tatizo la kimfumo, mtanisema ama kunichukia lakini tatizo la Tanzania ni Wazee.

Wazee wanahitajika kuondoka kwa wakati mmoja, vinginevyo Tanzania haitatibika miaka nenda miaka rudi. Labda aje atokee kiongozi dikteta mustaarabu kitu ambacho si rahisi kumpata kiongozi wa namna hiyo kwa hali iliyopo sasa.

Tatizo wazee wamegubikwa na mentality ya kikoministi ndani ya ubepari, hivyo kasi yenyewe ya kibepari ina wa control badala ya kui-control kasi ya kibepari.

Mtasema vijana waliopo wamefanya nini? ni kweli hawawezi fanya kitu wakiwa wamezungukwa na wazee wakumunisti wenye miendo kasi ya kibepari.

....yule mlevi waziri wa mambo ndani ni kijana lakini albino wanakufa na ujambazi ni order of the day,mbona Mrema mambo ya ndani aliiweza yeye vipi na ukijana wake....sio factor hiyo mkuu!
 
Umeniacha hoi kabisa, i think i have to have a rest! Rais nafikiri ana umri wa miaka 58 au 59 kwa sasa. wastani wa mawaziri wake na advisors ni 50 years old (meaning anao wale tangu 39 hadi 60). please give me a break, age has got nothing to do with thie. mindset. We are Africans!! Mr. Zuma has got 5 wives and still went on his friends daughter having a kid with her. how do such presidents get time to work for the people, at the sametime they are trying to manage their wives at home and concubines outside marriage?

African mindset! we call it culture at the same time the sufferer is ourselves.
 
....yule mlevi waziri wa mambo ndani ni kijana lakini albino wanakufa na ujambazi ni order of the day,mbona Mrema mambo ya ndani aliiweza yeye vipi na ukijana wake....sio factor hiyo mkuu!

Ni factor kubwa sana.
Soma vizuri habari ,ni ngumu kubadirisha system kijana mmoja kati ya wazee. ukitaka kupima kasi ya vijana na mabadiriko ya kweli nafasi ya vijana iwe sawa na wazee waliopo saizi na wazee wawepo kama ilivyo saizi kwa vijana.
 
Umeniacha hoi kabisa, i think i have to have a rest! Rais nafikiri ana umri wa miaka 58 au 59 kwa sasa. wastani wa mawaziri wake na advisors ni 50 years old (meaning anao wale tangu 39 hadi 60). please give me a break, age has got nothing to do with thie. mindset. We are Africans!! Mr. Zuma has got 5 wives and still went on his friends daughter having a kid with her. how do such presidents get time to work for the people, at the sametime they are trying to manage their wives at home and concubines outside marriage?

African mindset! we call it culture at the same time the sufferer is ourselves.

no no no no
angalia vizuri wote hao uliowataja ni makomunisti ktk siasa za Tanzania.

Ninaposema makomunisti nina maana hii. Nenda kakae barabara ya bagamoyo uone hawa makomunisti wanavyoelekea kwa babu.

In other word nchi unapompa mzee kuongoza unakuwa umemkabidhi babu fulani ambaye hajaenda hata darasa moja kuongoza nchi. Mind you nchi inaoongozwa na waganga wa kienyeji ambao hata hawajaenda darasa moja.

Viongozi hawa wazee kabla hawajafanya maamuzi kuhusu mustakbali wa nchi wana wa consult waganga wa jadi(vibabu ambavyo hata chekechea havijaenda) na hivi vijiganga ndo vinawapa viongozi ushauri namna na jinsi ya kufanya.
Justification. Angalia maamuzi yanayotolewa utaona kabisa ni maamuzi ya mtu ambaye hajaenda shule.
Na kama unabisha basi jitahidi kupoteza mda wako ufuatilie viongozi wawili tu wajuu um-monite vizuri umufuatilie kila kona mwisho wa mwisho utamkuta mwambani bwagamoyo kwa babu.

wazee wanahitaji kuondoka hata wakibaki wabaki wachache sana.

Unamuongelea Zuma ,the same type. Wanafanya walichokiona kwa mababu zao ndio maana utawakuta bado wanakimbizana kwa vijibabu kwa sababu zilezile.

Rais akiapointi vijana wawili, watatu nothing will happen. Bwana hapo ameongelea Mrema, mrema kweli alijitahidi lakini hakufanikiwa na hakuna kipindi kilicjokuwa kina rushwa kama wakati wa Mwinyi na Mrema.
 
no no no no
angalia vizuri wote hao uliowataja ni makomunisti ktk siasa za Tanzania.

Ninaposema makomunisti nina maana hii. Nenda kakae barabara ya bagamoyo uone hawa makomunisti wanavyoelekea kwa babu.

In other word nchi unapompa mzee kuongoza unakuwa umemkabidhi babu fulani ambaye hajaenda hata darasa moja kuongoza nchi. Mind you nchi inaoongozwa na waganga wa kienyeji ambao hata hawajaenda darasa moja.

Viongozi hawa wazee kabla hawajafanya maamuzi kuhusu mustakbali wa nchi wana wa consult waganga wa jadi(vibabu ambavyo hata chekechea havijaenda) na hivi vijiganga ndo vinawapa viongozi ushauri namna na jinsi ya kufanya.
Justification. Angalia maamuzi yanayotolewa utaona kabisa ni maamuzi ya mtu ambaye hajaenda shule.
Na kama unabisha basi jitahidi kupoteza mda wako ufuatilie viongozi wawili tu wajuu um-monite vizuri umufuatilie kila kona mwisho wa mwisho utamkuta mwambani bwagamoyo kwa babu.

Maamuzi ya Mtu aliyeenda shule na ambaye hajaenda ni yapi hayo??sioni kwa siasa za TZ hili lina mantiki hata kidogo, Mfumo ndo unaliangamiza taifa, Kulindana, Hata mtu awe msomi vipi maamuzi hayawezi kwenda kinyume hata kidogo na mfumo wa kulindana uliopo, Dr Hosea taasisi yake ilikosea mbona mfumo unamlinda??? hata uwe msafi vipi lazima utende kazi kwa mujibu wa mfumo uliopo
 
Ni moja ya kipengele ninachokiongelea kwa lugha tofauti.

Huwezi mlaumu tuseme Masha eti kashindwa kazi wakati kuna kundi la wazee walioko juu yako mfano wanakundi la majambazi wanakulazimisha ulilinde kundi hilo.

Tatizo ni Tree ya wazee waliopo na ili kubadirisha hilo lazima uingize vijana wengi kwa asilimia 90%, maana hawa ni wapya hawatakuwa na mtu wa kumlinda badala ya kuchapa kazi. Hapo una ouita mfumo utabadirika outomatically.

Maamuzi ya mtu aliyenda shule ni tofauti na maamuzi yanayotolewa na waganga wa kienyeji ya kuwaambia viongozi walioenda shule namna ya kufanya badala ya kutumia elimu kufanya maamuzi makini.

ndio maana nikasema kama hiyo haiwezekani basi aje Kiongozi dikteta mustaarabu, zaidi ya hapo kelele zitapigwa miaka nenda miaka rudi bila mafanikio.
 
Ni moja ya kipengele ninachokiongelea kwa lugha tofauti.

Huwezi mlaumu tuseme Masha eti kashindwa kazi wakati kuna kundi la wazee walioko juu yako mfano wanakundi la majambazi wanakulazimisha ulilinde kundi hilo.

Mfumo uliopo wa ni kabisa tatizo na Tree ya wazee waliopo na ili kubadirisha hilo lazima uingize vijana wengi kwa asilimia 90%, maana hawa ni wapya hawatakuwa na mtu wa kumlinda badala ya kuchapa kazi. Hapo unaouita mfumo utabadirika outomatically.

Maamuzi ya mtu aliyenda shule ni tofauti na maamuzi yanayotolewa na waganga wa kienyeji kuwaambia viongozi walioenda shule namna ya kufanya badala ya kutumia elimu kufanya maamuzi makini.

ndio nakasema kama hiyo haiwezekani basi aje Kiongozi dikteta mustaarabu, zaidi ya hapo kelele zitapigwa miaka nenda miaka rudi bila mafanikio.

What are you talkin about?Hao asilimia yako 90 ya kufikirika nao si watakuwa wameingizwa na mfumo?Itakuwa ni diferrent ish the same shovel.....Vijana wapya mfumo ule ule,sasa sijui hiyo kusema "Utabadirika outomatically" umeitoa wapi mkuu.
 
Kwani mfumo ni nini?
kama nimekosea nirekebishe.
mfumonielewavyo mimi ni Tree diagram, mfano alikuwepo mwanzirishi wa chadema ,huyo mwazirishi kamuachia mkwe, mkwe kumuachia rafiki yake ,huyo rafiki kamuachia mtoto wa mwanzirishi wa chadema huyo mtoto kamwachia mkwe wa mkwe wa mwanzirishi.

hiyo tree diagram mimi nafikiri ndo mfumo/system yani ya kwamba ikija kunguduruka yule mkwe alifuja fedha za chadema lazima huyu aliyopo sasa lazima amkingigie kifua maana hiyo tree diagram ina uhusiano wa moja kwa moja.

Ukileta vijana wapya ,i mie nafikiri ni mfumo tofauti ,ulio na mtazamo tofauti, ni tofauti na ule wa kwanza.

Nani atawaleta hawa vijana ni Rais ambaye ameshindwa namna ya kuushughurikia diagram tree iliyopo.

mfumo ni tofauti na sera, ukiangalia vizuri kuna uwezekano mkubwa sana sera ya ccm ni best kulinganisha chama chochote.Sasa ukiingiza vijana ama tree diagram mpya ambayo imenuia kusimamia sera nafikiri tutasonga kwa kasi.
 
Kila siku tunapiga kelele za ufisadi mkuu. Hivi sasa ufisadi umefika hadi ngazi za chini kabisa kiutendaji. Binafsi nimeshuhudia ufisadi huo ktk moja ya mikoa iliyotajwa hadi kufikia hatua ya PM kuamuru mkuu wa mkoa kuunda tume kufuatilia ufisadi huo hivi karibuni. Tatizo baadhi ya wajumbe katika kamati hiyo nao wamejichotea pesa za kutosha kwenye vocha hizo,je tutafika kwa utaratibu huo?
 
Kwani mfumo ni nini?
kama nimekosea nirekebishe.
mfumonielewavyo mimi ni Tree diagram, mfano alikuwepo mwanzirishi wa chadema ,huyo mwazirishi kamuachia mkwe, mkwe kumuachia rafiki yake ,huyo rafiki kamuachia mtoto wa mwanzirishi wa chadema huyo mtoto kamwachia mkwe wa mkwe wa mwanzirishi.

hiyo tree diagram mimi nafikiri ndo mfumo/system yani ya kwamba ikija kunguduruka yule mkwe alifuja fedha za chadema lazima huyu aliyopo sasa lazima amkingigie kifua maana hiyo tree diagram ina uhusiano wa moja kwa moja.

Ukileta vijana wapya ,i mie nafikiri ni mfumo tofauti ,ulio na mtazamo tofauti, ni tofauti na ule wa kwanza.

Nani atawaleta hawa vijana ni Rais ambaye ameshindwa namna ya kuushughurikia diagram tree iliyopo.

mfumo ni tofauti na sera, ukiangalia vizuri kuna uwezekano mkubwa sana sera ya ccm ni best kulinganisha chama chochote.Sasa ukiingiza vijana ama tree diagram mpya ambayo imenuia kusimamia sera nafikiri tutasonga kwa kasi.

Mfumo wa kupata uongozi ni tofauti na uongozi wenyewe,wewe unazungumzia kipi? weka pointi zako vizuri ili ueleweke.....Ninachosisitizia hapa ni kwamba mfumo wa kuwaweka viongozi madarakani ukiwa corrupt haijalishi kama aliyewekwa madarakani ni kijana ama mzee....Lazima na wao watakuwa corrupt..Kwavyovyote vile watataka kulipa fadhila kwa wale waliowafadhili wakati wa kampeni za uchaguzi nk....Na kwahivyo hawawezi kwenda kinyume na mfumo uliowaweka madarakani.
Hilo la kulindana wakati wako madarakani ni mfumo wa uongozi ambao ni corrupt na si mfumo wa mchakato wa kupata kiongozi,elewa utofauti hapo....Pia hakuna mahali nimesema sera ndio mfumo....Na hayo mambo ya chadema sijui ni nini unazungumzia.

Angalizo:pia usisahahu kuwa tuko kwenye mjadala unaohusu corruption,so lets build on that kuliko ku suggest mambo yasiyoeleweka.
 
Labda unieleweshe
Unaongelea muundo ama mfumo?

Kwanza si kweli wabunge wote wanafadhiliwa na mfumo kuupata ubunge, na mara nyingi wanaofadhiliwa ndo hao baadae unawaona ktk nyadhifa maana wanakuwa wameshajipanga tangu mwanzo.

Nauhakika hakuna mfumo uliomweka Magufuri kuupata ubunge wala mfumo uliomweka seleli. Sasa mfumo unaoongea hauko bayana unaongelea nini.? wewe vipi hiyo chadema ni mfano mbona waja juu.teh teh teh teh huo mfano wa chadema ndo mfumo huo.
 
Mimi nadhani hili suala ni kubwa mno sababu pesa nyingi za serikali sasa hivi zinakwenda moja kwa moja wilayani. Sasa kama pesa za mbolea zinaliwa kwa kiasi hiki, si ina maana pesa za elimu, barabara, afya nazo zinaliwa kupita kiasi??

Hapa ingawaje ni jukumu la serikali kuwajibika, lakini twende mbele kidogo na kuuliza, hawa wabunge wa hizi sehemu wanakuwa wapi wananchi wao wakiibiwa pesa kiasi hiki??

Nadhani hapa lazima transparency iwe ya hali ya juu, kwa mbunge kuhitisha vikao majimboni kuwaeleza wananchi serikali imeleta pesa kadhaa wa kadhaa, na tuzifuatilie.

Hapa wanaopigwa bao ni sisi wananchi sababu ya kukosa elimu na ufahamu, sasa wabunge lazima wawe mstari wa mbele sababu wao ndio wanajua hiyo budget ya serikali ilivyo.

Kwa kuanzia tu lazima waziri mkuu na waziri wa Kilimo watueleze hatua gani zinachukuliwa kwa haraka kuaddress hili suala linalogusa wananchi maskini huko vijijini.

May God Bless Tanzania.
 
Back
Top Bottom