Zaidi ya bilioni 25 zatafunwa; Watendaji waanza kuwajibishwa!

Kama hatutafuti jinsi ya kurekebisha/kubadili serikali, tutaendelea kujaza makabati yetu kwa taarifa za ufisadi na ubadhirifu wa serikali kila uchao! Na wao wataendelea kusema hizo ni kelele za mlango tu wala haziwanyimi usingizi! KURA YANGU SIWAPI!!!!
 
Bado najiuliza, hivi mambo kama haya yangefanywa China ingekuwaje? Lazima wahujumu hao wangekiona cha moto. Wanaleta sera zao eti "KILIMO KWANZA" halafu mambo yenyewe ndio haya? wanapiga ma deal mpaka kwenye mbolea? halafu ili mazao yastawi watasema "tusubiri kudra za Mwenyezi Mungu". Pumbavu kabisa.
 
Interested Observer,

Politically you are right, Practically you are not!

Let me put this way... for this ase in hand,

President: is Accountable
Prime minister: is Responsible


Usually you start with that who is responsible b4 that who is Accountable! in other words wait n see whether Pinda will do something, if not then move on to the "mwenye nyumba";

But surely not everthing escallated to president as if there is no administrative structures in this country...

Remember "TAWALA ZA MIKOA" is under Prime Minister Office ...

Thanks
Kasheshe

With due respect nakubaliana na wewe, lakini kwa nchi zetu hizi hilo ni gumu, watendaji wa serikali wameshamsoma mwenye nyumba na kugundua kwamba sio mtu wa kuumiza kichwa kufuatilia kwa ukaribu utendaji wa wasaidizi wake. Kilichobaki.....wote walio chini yake ni business as usual!!

Tone at the top is critical mkuu!!
 
Jamani hii ni issue planned na CCM ukweli ni kwamba pesa hizo za kilimo nyingi hazikupelekwa huko, walipeleka hewa ili ku-justify kwamba pesa za EPA zimerudishwa kumbe hakuna lolote.
 
Kama hatutafuti jinsi ya kurekebisha/kubadili serikali, tutaendelea kujaza makabati yetu kwa taarifa za ufisadi na ubadhirifu wa serikali kila uchao! !!!!

Bora hata hayo makabati wanayotunzia hizo ripoti yangekuwa yametengenezwa Tanzania, tungesema vijana wetu wanapata ajira. Cha kushangaza kila ofisi ya serikali unayoijua, inatumia fenicha za china....kuanzia masofa mpaka meza ya kuwekea chupa za chai!!
 
mi nilishasema kuwa hapa watu wamebuni njia nziri sana ya kula pesa maana hakuna sheria yoyote. viongoz wpo na wao ndo wanakula nao

nimeamini kunazia ngazi ya juu serikarini wapo wapo tu hakuna jipya.
nimesikia et julai anachukua form tena!!!!!!!!!
 
Jamani hii ni issue planned na CCM ukweli ni kwamba pesa hizo za kilimo nyingi hazikupelekwa huko, walipeleka hewa ili ku-justify kwamba pesa za EPA zimerudishwa kumbe hakuna lolote.

.....Magezi,

You very wrong kwenye hoja hii......! Nakuhakikishia, vocha za Ruzuku zilisambaswa mikoani, wajanja wa mikoani(wafanyabiashara + viongozi wa serikali za mitaa), walicollude na kujinufaisha wao wenyewe.....!

Kuna watu wakaribu kabisa ninaowafahamu waliofaidi na vocha hizi....tena for ur info, hili lilikuwa open deal for anyone with good money......soma post ya mtanzania pia on this....then will understand what I am saying!
 
We shall be singing this song everyday and it will get through no-ones brain. I say it's a question of attitude and values. Our values as TZs are twisted. Already most of us have been wired to desire the easy way out. If it involves saving a few cents we will do it e.g illegal connections, buying stolen, fake goods at cheaper prices, conning, bribing the police because we do not want to be responsible for our deeds...DECI, small corruption, medium corruption and of late grand corruption. Its everywhere! When we are involved in stealing, corruption etc we should be SEVERELY punished iwe fundisho kwa wengine kama ambavyo Babu Seya and co. wanakua SEVERELY punished iwe fundisho kwa wengine. Shame...This is sad, sad...hata wakulima vijijini tunawaibia jamanii?
 
kinachouma katika sakata zima la utafunaji ni ule ukatili wakutowaonea huruma wakulima wetu, kweli pesa inatengwa kwaajili ya ununuzi wa mbolea na pembejeo za kilimo anakula mtu fulani kwa njaa na tamaa zake....inakera.
nimebahatika kutembela mikoa yote ya TZ kwa kipindi cha miaka 7 hivi, kwa kweli umasikini wao ni matokeo ya unyanyasaji wa aina hii ambao hufanywa na serikali yao.
Tembelea vijijini wakati wa mavuno ukaone mazao yanavyooza mashambani kisa hakuna usafiri wa kuaminika, ama hakuna soko la kuaminika.
wameanzisha kampeni ya kilimo kwanza kushawishi watu walime wakati wale wanaolima wameshindwa kuwapatia masoko yakueleweka....nani alietuloga ?
KWELI ccm NA UFISADI ni chanda na pete......kuwatenganisha ni mpaka kifo cha mmoja wao.
 
...
Nchi hii mfumo mzima wa utawala kuanzia ngazi ya juu mpaka chini kabisa kny serikali za mitaa, upo kifisadi fisadi. Utawala wa nchi hii, haupo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi bali kujiletea maendeleo yao binafsi. Nchi hii watu watakuja kuuza mpaka anga, barabara na hata wanachi tutakuja uzwa mambo yakiachwa yaendelee hivi hivi......!

Hapo umetoa jibu kwa thread moja iliyouliza kwa nini CCM hushinda kila uchaguzi kwa kishindo. Ni kwamba wamefanikiwa kuingiza nchi nzima kwenye mfumo wa kifisadi. Hata wasiokuwamo hivi sasa ama wanapozwa kwa makombo ya wanaochota au wanapewa matumaini ya kuja kuwa ndani ya mfumo siku moja (kutesa kwa zamu). Kila mradi, kila sheria (regulation), kila mpango unaopitishwa lazima ugeuzwe kuwa dili la kifisadi.

Hivyo, rushwa, dili, misheni, ufisadi kwa pamoja ndio msingi wa amani, utulivu na mshikamano wetu tuliojengewa na hawa jamaa. Ukiibua uozo kama huu utasikia mara moja wakisema wamestushwa sana na watachukua hatua kali kudhibiti hujuma hiyo inayokwenda kinyume na sera ya Chama ya Kilimo Kwanza - changa la macho hilo.
 
Kweli wizi mtupu. Hatuoni aibu hata kidogo kwamba sasa imetosha. Kila siku ni scandal za wizi tu! Nchi hii imekuwaje? Toka juu kabisa mpaka chini tunapigania madaraka ili tujineemeshe kwa njia zisizo halali? Hii ndo Tanzania tunayotaka kuijenga?
Kweli kikulacho ki nguoni mwako. Tunatengeneza tatizo ambalo litakuja kuturudi bila huruma na hatutakuwa na mtu wa kumlilia isipokuwa ni kujililia wenyewe.
 
duuuh inabidi sasa tuanze kuweka kumbukumbu ya fedha zilizochotwa kwenye ufisadi hili raisi anapomaliza miaka yake mitano tujumlisha fedha zote alafu tuone aliwajibika vipi.

bilioni 25 za mbolea na mbegu watu wameenda kujichotea na hapa pia hakuna atakaye wajibishwa? ama kweli nchi inaongoza na waovu wakubwa.hivi kama mtu msafi unaweza kumuogopa mtu mchafu?
 
watch this... within these few weeks mtasikia serikali inapewa misaada ya mabilioni kutoka kwa the so called "our development partners" a.k.a donors.. they always do this everytime there is a scandal boiling... it is like local anesthetic .. hawataki tusikie maamivu.. mark my words.

Unataka kusema kuwa nao wanafaidika nao au kwa kuwa njia inazidi kuwa nyeupe kwao? Sidhani kama misaada hio inatoka US labda Canada.
 
Matatizo ya Tanzania ni makubwa mno kuliko tunavyoweza kuongea hapa, uongozi bora haupo, utendaji mbovu umetawala kila sehemu, jamii nzima ni kama imegeuka kuwa ya wezi na wasanii. Bila kubadili hii culture mbovu, tutaendelea kupoteza mabilioni ya pesa kila siku.

You step from them?
 
Chakufurahisha serekali ipo mpaka ngazi ya kijiji

Ukijaribu kushuka chini Kuanzaia ngazi ya MKOA,WILAYA kuna TAKUKURU,UWT, Polisi, wawakilishi wa raisi i mean wakuu wa mikoa/wilaya,wawakilishi wa waheshimiwa mawaziri, mafisa kilimo wa mkoa/wilaya, chakujiuliza kama serekali ipo mpaka ngazi hizo nini wanachokifanya???wizi unatokea mkoani, mwakilishi wa raisi/mkuu wa mkoa hajui, mkuu wa UWT hajui, TAKUKURU, hajui, AFISA KILIMO MKUU WA MKOA hajui, tujaribu kutafakari NINI KAZI ZA HAWA WATU??? au ni vikao tu visivyokuwa na tija, naona kinacholiangamiza taifa ni mfumo mzima wa utawala, TUWE NA SEREKALI ZA MAJIMBO, mkuu wa jimbo awe na utawala wake from there majimbo yatakayopenda kuendelea lazima yataendelea, kwani mfumo huu wa sasa umekuwa chanzo cha UFISADI, UVIVU,KUTOWAJIBIKA, NA MBAYA ZAIDI KUTOKUJALI.

 
Back
Top Bottom