Zaama la Talaka laingia kwa wachungaji - Benny Hinn Apigwa Talaka na Mkewe

count shetwani out of this mess please...
mbona unamtetea shetani??? amekutuma au umeamua tu kumtetea??? Of course kuachana ni kazi za shetani - yeye kazi yake ni kuchinja, kuharibu, kuua - Hata hivyo naamini mtumishi huyu wa Mungu (Benny Hin) atasimama imara katika jaribu hili bila kumkosea Mungu na bila kutetereka kuifanya kazi ya Mungu aliyoitiwa. Katika kila jaribu Mungu ameweka mlango wa kutokea - let all believers pray for him - amen!!

simtetei shetwani. lakini lazima tujenge imani kuwa mapenzi ni kama kiumbe hai. huwa yanazaliwa kwa kuanza kufahamiana na baadae mapenzi yanadhihirika na haja ya kuishi pamoja mkiwa katika hali ya mapenzi inajitokeza na ndio ndoa huzaliwa hapo... lakini lazima pia tukubali kuwa kila chenye uhai na kinachozaliwa hakina budi kufa. mapenzi pia yana uhai usipoyalisha yananyauka, au yakipata magonjwa ya magomvi utengano n.k. yanaweza hata kufa.. na hayo ya mama huyyo yameisha. Tubadili mtazamo na viapo vyetu hii habari ya tutaishi pamoja hadi kifo kitutenganishe ni tatizo hapa, ingekuwa ni mpaka hapo mapenzi yetu yatakapokufa basi kusingekuwa na kushangaa wakati wa talaka. msisahau wachungaji ni binadamu pia wanamapungufu yao
 
Back
Top Bottom