Yutong Vs scania Vs ud

jana nilipanda scania ya ottawa horse power ni f 330 tulikuwa tunatoka songea kuja dar, tulizikuta yutong za super feo kabla hata ya njombe wakati zenyewe zinatangulia kutoka. Sema scania zimetofautiana uwezo
 
Binafsi sina vigezo vya kiutaalamu sana, ila nilisha(ga) panda yutong za Greenstar, Happynation, Muro na Luckystar, zote hizo haziwezi kulingana na Scania hata siku 1.. Scania iko poa n very strong..! Nakumbuka 2011 niliwahi kutoka mwanza saa 12:00 na kufika mbezi saa 19:15 na Scania ya Ally's,. So binafsi Yutong sijazikubali kwa kazi ila kwa starehe ziko poa sana.
 
kulinganisha SCANIA na YUtong au Zonda ni kujisumbua tu ni sawa na NOkia na tecno.kabla hatujaelezea ki undani(technical specs)kwanza mleta mada anatakiwa ajuwe umri wa uwepo wa yutong na scania kuwepo sokoni.au alinganishe hata bei ya scania na bei ya yutong.
kuhusu speed na mambo mengine kuna factors nyingi za kuangalia mambo hayo ikiwa ni pamoja na ukubwa wa injini,gear box,differential(difu),fuel pump inayojumuisha fuel governors,nozzles,fuel reduction,fuel turbo nk.
 
<br />
Zitakusumbua kwa sababu ya hali ya hewa kwani engine mbele ni kwa ajili ya upepo system ipoe vizuri, achana na hiyo kiti.[/QUOTE]
Mkuu ni. Kweli zitamsumbua ila si kwa sababu uliyosema! Basi zenye injini nyuma ndiyo standard ulimwenguni kwa sasa. Ndio maana mwaka 2010 fifa world cup walipotoa tenda ya mabasi kwa wageni waalikwa na wachezaji, manufacturer waliobid kwa basi za injini mbele walishindwa vibaya.Cooling system zimeimarishwa sana na kuna baadhi ya model zina double radiator. Kwa wanaotaka kuleta na kutumia basi ,zenye injini nyuma wanakabiliwa na changamoto zifuatazo
1:kwa sababu ya comfort basi za injini nyuma zinakuja na injini kubwa sana. Marcopolo paradiso kwa mfano ingine zina range 420 to 500 hp, idea ni kufanya iwe inatembea kwa mwendo wa wastani at very low engine rpm. mostly huwa 100km/h at 1000rpm,na hivyo quiet cabin. Hapo ndio suala la dereva linaingia. ukimpata dereva anayependa ligi ,utaumia sana kwenye mafuta na biashara litakushinda.
2: Kwa sababu injini kuwa nyuma .mara nyingi madereva hawaisikii hali halisi ya injini so inakuwa ngumu kufahamu ni wakati gani engine inataka change down ,hivyo wanaya overload bila kujua (magari mengi huwa yanaeleza kila kitu kwenye dash board ni bahati mbaya madereva wengi hawafatilii).matokeo yake ni kuharibu clutch plate ,bell housing ,gearbox ,axle n.k ( hili ndio linalomsumbua sumry kwenye luxury basi zake za malasia.) Hapa sasa Automatic transmition inakuwa ni best option.
3: Idea ya mashine kubwa ni kufanya kazi ya kawaida kirahisi na sio kufanya kazi ngumu kuwa ya kawaida , So routes ambazo ni power demanding kama songea ,tunduma n.k.Japokuwa basi litaweza kwenda lakini zitakugharimu mafuta na matairi(tyre friction to road increases as engine horse power increases)
Ushauri tu kama unataka kufanya biashara. Na mabasi ya mashine nyuma nunua automatic, halafu tafuta dereva mzuri litakaa miaka mia! Na utafanya biashara sana ,anayezijua raha za mabasi hayo atapanda basi mashine mbele kwa shida sana.
 
scania zinatoka sweden moja kwa moja, ila south africa ni assembling plants za magari ya marcopolo, irizar au iris. marcopolo zinatengenezwa brazil.
yutong zinauzwa mil 200 - 250, marcopolo zinauzwa mil 700 - 800, marcedes benz zinauzwa mil 800 - 900.
ukinunua bus ni sawa na unavyonunua suzuki yako, wanaipakia kwenye meli had dar na proces zote zinaendelea hapo.

na kingine kuhusu haya mabasi ni kwamba marcopolo zinadumu sana kwa mazingira magumu ya africa mfano dar ex press ana marcopolo toka mwaka 2002 nipo mzigoni hadi leo naziona zinapiga mzigo (T ... AJR) ila life span ya yutong kwa mazingira ya africa ni maximum of 3 - 4 years inategemea na service yako na jinsi unavo-imaintain. Na wafanya biashara wamegundua kutumia yutong kwasababu ni cheap na wanayatumia kutengenezea faida ya haraka likichakaa wanatupa na kununua mengine.
 
Nimefuta kauli baada ya kufanya simple research,scania ni zaidi ya yutong
kwa speed,durability etc.
 
Scania zinakuwa nzito sana hasa kwenye kupandisha milima/milimani....lakini kwenye flat road...dah usipime!! Yutong ni laini mno na zinapepea kama karatasi, it is good by then!!

Scania inapandisha mlima kama inashuka vile na kumbuka zinatengenezwa kwenye nchi za Milima, Yotong inakimbia kidogo kwenye Tambalare lakini mlimani hamna kitu hata mtembea kwa miguu anaipita.
 
Huyutong co gari kwa mwenye akili timamu!

Tunaziona kila cku zinakufa gia box watu wanalala porini! UD na scania ndo mpango mzima! Mifano mizur ni basi za abood hood taqwa na falcon! ukipanda hizo safari ni huhakika kwa asilimia 95! Ila ukitaka kulala porini panda huyutong zisizo pewa service kama green star!
 
wadau kuna kaubishi kapo hapa kijiweni kwetu kuhusu efficiency ya haya magari especially mabasi. Ubishi ume-base sana kwenye
1) speed ya mabasi, wengi wanaSema yutong ni funiko kuliko scania na ud.
2) ubovu- wamerate kuwa ubovu mchina anaongoza na relate kipindi yalipoingia Yalilaza watu njian nikiwemo na mimi. Ud wanatolea mfano sumry anavoPotea kwenye ushindan.
3)oil consumption. Mchina consumption yake iko chini kuliko wote. je ni kweli
NaOmba wadau na wajuzi wanisaisidie kwasabab nahitaJi kujua ubora wa haya Magar na hata wadau wengine ambao wanaweza kutaKa kuinvest kwenye biashaRa ya magari itawasaidia

Bado hakuna kampuni ya kuishinda Scania. Na labda huko ambapo Yutong zinasumbua wana Scania model za zamani. Sasa hivi kuna Scania F330 ambako kwa Mwanza wanazo kampuni ya Ally's, kwa Mbeya kuna Nganga, Budget, Moshi na Arusha kuna Dar-Express na mengineyo. Bado hakuna Yutong ya kukimbizana na hizo gari. Ina Scania Euro6 engine 9.0L Turbo Intercooler plus Turbo Compound inayogenerate 330HP na 1600 Nm of Torque and a top speed of 130kph (Scania Euro 6 buses and coaches) ulinganishe na Yutong yenye engine ya Cummins 300HP Turbo and the max speed of 110kph(ZK6116D-YUTONG). Nissan Diesel haziwezi kupambana na hao wawili kwa kuwa hazinaga Turbo ila zina sifa ambayo hayo yote hapo juu hayana nayo ni uwezo wa kwenda safari ndefu mno. Ukitaka kuhakiki angalia kampuni zenye mabasi yanayokwena nje ya nchi..
 
Huyutong co gari kwa mwenye akili timamu!

Tunaziona kila cku zinakufa gia box watu wanalala porini! UD na scania ndo mpango mzima! Mifano mizur ni basi za abood hood taqwa na falcon! ukipanda hizo safari ni huhakika kwa asilimia 95! Ila ukitaka kulala porini panda huyutong zisizo pewa service kama green star!

Abood na Hood wote wanatumia Scania, Taqwa na Falcon wanatumia Nissan Diesel UD ambayo yana uwezo wa kuvumilia safari ndefu mno. Kama utakumbuka kombe la dunia lilifanyika South Africa mabasi yaliyotoka hapa kupeleka watu huko yalikuwa ni ya kampuni ya Kampala Coach ambayo yote ni UD...
 
Wandugu yutng engine zake ni madhubuti asikudanganye mtu. ni za kimarekani toka magari ya MAN. MBIO NDO NYUMBANI KWAKE HAKUNA CHA MARCOPOLO WALA UD.

unaijua marcopolo au unaongea tu..marcopolo ni body type,af nani kakudanganya kwamba utong ina engine ya MAN
 
Scania ni noma; Mbeya-Dar kuna Happy Nation (Sauti Ya Manka), Arusha-Dar kuna Chakito(Ndama Jeuri au Masogange) Ngorika(Nazareth au Macedonia), Mwanza-Day Kuna Ally's Sport Bus. Hayo mabasi niliyataja hapo hakuna Yutong ishawahi kuyaona hata yalipopita...
 
Binafsi sina vigezo vya kiutaalamu sana, ila nilisha(ga) panda yutong za Greenstar, Happynation, Muro na Luckystar, zote hizo haziwezi kulingana na Scania hata siku 1.. Scania iko poa n very strong..! Nakumbuka 2011 niliwahi kutoka mwanza saa 12:00 na kufika mbezi saa 19:15 na Scania ya Ally's,. So binafsi Yutong sijazikubali kwa kazi ila kwa starehe ziko poa sana.

Hizo Allys achana nazo ni Mashine nyingine labda ufananishe na Arusha Express au Mghamba za arusha mwanza.

Hao jamaa nasikia huwa wanabadilisha Difu wanafunga kitu cha High Speed hapo ni mwendo wa kukimbia tu.

Ila kumbuka Allys walikuwa wandispline sana na kusimama njiani kwani piga hesabu kutoka Dar mpaka mwanza kuna vituo vingapi na kila kituo ukisimama Dakika 5 hiyo ni zaidi ya Lisaa lizima.
 
wadau kuna kaubishi kapo hapa kijiweni kwetu kuhusu efficiency ya haya magari especially mabasi. Ubishi ume-base sana kwenye
1) speed ya mabasi, wengi wanaSema yutong ni funiko kuliko scania na ud.
2) ubovu- wamerate kuwa ubovu mchina anaongoza na relate kipindi yalipoingia Yalilaza watu njian nikiwemo na mimi. Ud wanatolea mfano sumry anavoPotea kwenye ushindan.
3)oil consumption. Mchina consumption yake iko chini kuliko wote. je ni kweli
NaOmba wadau na wajuzi wanisaisidie kwasabab nahitaJi kujua ubora wa haya Magar na hata wadau wengine ambao wanaweza kutaKa kuinvest kwenye biashaRa ya magari itawasaidia

Nachangia kwa utaalam as mechanical engineer, Youtong technlojia na design iliyotumika kulitoa basi hilo kwa matumizi inaruhusu gari hilo kulala kwa nyuzi 52 (fitytwo degrees) wakati mabasi mengine including scania ni 32 degrees that means ikitokea kuyumba na tairi zikanyanyuka upande mmoja kwa mlalo nilioutaja, Youtong iko vizuri kurejea barabarani bila madhara tofauti na scania
Kwenye sifaza chuma kigumu na majina hiyo ni kwa miaka tuliyopita ni kweli tulihitaji mabasi yanayodumu kwa muda wa miaka mingi lakini sasa tunahitaji teknolojia ya kukuwezesha kufika kwa muda mfupi, comfortably na luxurier mambo ya unaisikia scania inavyolalamika mlimani htutaki!!!
 
Kwa speed, nadhani sometimes uzito wa gari unachangia kuhisi kama gari inakimbia zaidi. namaanisha same speed lakini kama gari ni nyepesi unaweza ona kama inakimbia zaidi kuliko nyingine nzito. So, at 80 km/h unaweza ona Yutong inakimbia kuliko scania ambayo ni nzito zaidi. hata kwa gari ndogo, jaribu endesha 4x4 cruiser na gari ndogo kama vitz at 100 km/h, vitz unaweza dhani unapaa wakati land cruiser unaona kawaida tu.
 
Shda c gearbox hata yutong ikiekewa 10 speed ya scania 113M bado hawez pambana na scania yeyote inayoanza na 91 kuendelea mpaka 124
 
Back
Top Bottom