Yutong Vs scania Vs ud

Ijapokuwa tokea mwaka wa 2000 scania zinazoingia Afrika mashariki ubora wake ni duni, mabovu na kibaya zaidi scania tz wala hawaweki vipuli na wakileta ni vipuli vya kutoka china ambayo bei inastahili iwe nafuu lakini scania tz wanawararua wa bongo.

Tunazisikia na kuzijua mbinu hizi. Na ndio maana wananaonunua mabasi ya scania kwa mikopo wanashindwa hata kulipa mikopo hiyo kwa sababu ya ughali wa magari, gharama kubwa ya uendeshaji na ubovu usiohimili.

Kwa hali hiyo tuweni wa kweli kwa kusema Yutong ni mabasi mazuri na yakiundwa China kwa technologia ya Europe na yanatumia Engine za Cummins ambayo ni technologia ya kimarekani iliofaulu, na pamoja na hayo bei ya Yutong ni nafuu mno na ni sawa na ni asilimia 30% TU ya bei ya scania, na isitoshe vipuri vipo kwa wingi tu na vya asilia pia ambavyo hutengenezwa na Yutong wenyewe kutoka China, na ulaji wa mafuta ni pungufu kuliko scania na bodi zake Yutong zimeundwa kwa kuzingatia viwango vya usalama duniani na kuzingatia hali ya barabara ya Tz na Afrika mashariki na kwa hivyo BODY zake za Yutong zina usalama kuliko scania marcoplo na irizar.

Kwa hivyo kama kuna watu wanaponda Yutong, basi hao ama wanadanganywa na wauzaji wa scania na ud kwa kufikiria kuwa kila cha china ni kibovu JAMBO AMBALO NI UZUSHI maana hata hao scania na ud hutengeneza vipuli vyao huko huko china. Na kama mtu atafatilia maintenance za Yutong vizuri na kutumia vipuli asilia UTAKUTA NA KUTHIBITISHA KUWA YUTONG NI bora na ndio suluhisho kwa usafiri na uchumi wa Tz. Wa Tz tuzinduke, si kila kitu cha ulaya ndicho kizuri, HAPANA, wakati umebadilika,

scania ishapitwa na wakati, scania hawatujali u Tz wetu wala uchumi wetu, bali wanachojali wao ni mishahara yao na maslahi yao binafsi tu. Ikiwa wanajali, iweje scania wako tz takriban miaka 40 lakini hata vipuli vya kutosha hawana, ukienda pale kwenye karakana yao utakuta vipuli vingi hawana, na ama hawana wanakuagizia kutoka aduka ya mjini ambayo ni mali ya taiwan iio na uboira na hata hizo vipuli walio navo utavikuta ni vya china huko huko au vya brazil na vya brazil ni vya uhafifu mno. Sasa iweje tukubali kudanganya kuwa scania ni bora kuliko Yutong kwa kisingizio kuwa yuong imeundwa China ili hali scania ni jina tu maana vipuli vyote ni huko huko China na afadhaliYuyong inaundwa China na Yutong wenyewe na hutoa Guarantee sembuse scania wanatengeneza china kwa kisiri na kwa hivyo huwezi hata kupata Guarantee.

wa tz tuamkeni na tuangalie maslahi yetu Kiuchumi, ikiwa ni wasafirishaji ni vema tununue Yutong ambayo ni asilimia 30% ya bei ya scania, na vipuli vyake tutumie genuine ambayo ni vipo vingi tu Tz na yenye bei nafuu na yana usalama kwa abiria wetu na ikiwa tunataka kuhakiki basi tuzitumie miaka 5 na tuuze tununue mpya maana muda huo fedha yetu tumerudisha, Lakini scania utanunua ghali sana sawa na mara 3 bey ya Yutong, inakula nafuta mengi, gharama yake ya uendeshaji ni mkubwa, na utatengeneza kila siku, na hata ikitembea miaka 3 mpaka 5, wakati bado hukurudisha fedha yako maana umenunua ghali abiria anaona basi lako kuukuu na hapandi tena, maana utamaduni wa abiria wetu kila miaka 3 wanataka bus mpya kwa hivyo utakuta scania wapende wasipende hawana nafasi.

Yutong ni suluhisho,

Mbongo mwenye uchungu na tz
 
Na kwa taarifa tu, mabasi ya sumry yanayokufa njiani siku zote ni nissan ud na hino na wala si yutong, maana sumry hana yutong hata moja, na mabasi yanayokufa njiani mengi ni scania na kama kuna yutong utakuta ni chache na hata hayo machache utakuta wakati wa utengenezaji wamiliki au mafundi wao wametumia vipuli fake.

kibaya zaidi wamiliki wa mabsi aina ya scania walio wengi wanashindwa kulipa madeni yao tofauti na wanaotumia Yutong,

Huo ni ushauri wa dhati wenye nia ya kuruzindua wabongo,

Simba
 
Kwangu mimi body za yutong sijazipenda kwa sababu zinarusha kinoma hamna tofauti Na kupanda scania made in tandika. what about ubora wa higer buses. Kuna anaezifahamu
 
Kwangu mimi body za yutong sijazipenda kwa sababu zinarusha kinoma hamna tofauti Na kupanda scania made in tandika. what about ubora wa higer buses. Kuna anaezifahamu

Hiyo ndugu yangu si kweli, inaweza kuwa na katika wafanyakaza wa scania au hufahamu magari kwa sabu mili zifuatazo :

1 ) Body haihusiani na urushaji wa abiria bali suspension system ndio inayohusika, na katika hilo ukweli ni kuwa YUTONG INA RAHA NA WALA HAIRUSHI KABISA. na hata ukiangalia statistics utaona likipata ajali bus aina scania wanapoteza maisha na kujeruhiwa ni wengi mno ukilinganisha na Yutong, na hiyo ni kwa sababu Yutong imundwa kwa kuzingalia usalama wa binadamu maana imefpitia roll over tests, nk, na isitoshe licha ya Yutong kuwa bora na salama pia waundaji wake kutoka kiwandani walikuja Tz wakafanye research na kujua aina gani ya mabasi yatakayohimili na kufaa ndio wakahakiki kuyatengeneza na kuyaleta kupitsha kwa wakala wao alie hapa Mikocheni na ndie wanaotengeneza pia na kuuza vipuli asilia.

2 ) Higer sio mabasi mazuri na yameundwa kwa kujaribu kuiga Yutong na kwa hivyo hayahimili na ndio hazikufaa si Tz tu bali hata Nchi jirani.

Yutong ndie mtengenezaji mabasi duniani mkubwa kwa sasa

Simba
 
Mkuu Sizinga hakuna kitu Yutong inakimbia kwenye tambarale tu kwenye mlima sufuri mkuu ila scania kwenye mlima ni noma maana inafunguka turbo achana nayo!!

Mbona songea kuna Yotung za Superfeo kila siku za kwanza kufika hapa songea tena ziko 4 kwa siku(songea dar then 4 dar songea)na scania za Ottawa zinatimuliwa vumbi wakati zinatoka muda mmoja songea au dar?songea kuna milima sana but still zinatembea?Yutong zinapendwa kwa vile ziko economical na hela inarudi kikubwa ni kufanya maintenance na ikifika muda flani inabidi gari ulipungizie ruti ndefu,scania vifaa vyake ni ghari sana once ikiaariba na kurudisha hela inachukua muda mrefu sana ukilinganisha na yotung
 
nilitaka kuandika kama wewe..ile njia hizi marcopolo na scania mpya huwa tunaziacha mbali sana na yutong za green sema tatizo huwa hazitulii njiani na driver asipokuwa mwangalifu mkipata ajali kwa speed ile na kwa bodi ile ya karatasi hatoki kiumbe anayepumua.

Mkuu yotung walishasema wameweka bodi nyepesi ili kupunguza vifo na vilema vya abiria,wanadai bodi ikiwa nyepesi incase gari ikapata ajari haiwezi kubingirika zaidi ya mara moja tofauti na zile zenye bodi ngumu zinabingirika mara nyingi na abiria hapo ndo wanavyopata vilema na vifo kutokana na kujigonga na kugongwa na mizigo
 
Mbona songea kuna Yotung za Superfeo kila siku za kwanza kufika hapa songea tena ziko 4 kwa siku(songea dar then 4 dar songea)na scania za Ottawa zinatimuliwa vumbi wakati zinatoka muda mmoja songea au dar?songea kuna milima sana but still zinatembea?Yutong zinapendwa kwa vile ziko economical na hela inarudi kikubwa ni kufanya maintenance na ikifika muda flani inabidi gari ulipungizie ruti ndefu,scania vifaa vyake ni ghari sana once ikiaariba na kurudisha hela inachukua muda mrefu sana ukilinganisha na yotung

Nnaungano mkono na mwenzetu alietowa mfano wa Yutong ya super feo route ya Sngea, na ni kweli gharama ya uendeshaji ya Yutong ni ndogo, ulaji wa mafuta ni mdogo na hata bei ya ununuzi wake ni mdogo kwa maana bei ys scania moja unapata Yutong 3, na wakati huo huo Yutong no bora kuliko scania.

Route ya songea ni km 1,000 na suer feo ameanza kutumia Yutong mwaka wa 2009 mwishoni na tangu hapo hataki gari nyingine isipokuwa Yutong.
Wananunua scania ghali waelewe ughali huo si kwa ajii ya umadhubuti wa scania bali matanuzi wa wakurugenzi wa scania wanaojilipa mishahara mikubwa sana na kutembea tembea kwa hivyo gharam hizo ili kufidia wanatengeneza magari mabovu kwa kuwadanganyia watu ni scania kama ya enzi za kle na kuwabandika bei. Wenzao wachina wako serious wameunda Yutong kwa kuzangatia ubora na kuhakiki wakala wao alie Mikocheni anauzamabasi Yutong kwa bei nafuu na anakuwa na vipuli vyote origino na kuwahudumia wateja wao muda wote vizuri tu,

Kwa hivyo Yutong ndio suluhisho kwa usafiri wetu Tz
 
...Mkuu Simba, 'makala' yako ni ndeevu lakini nimeona imekaa kii-'sentimental' zaidi.
Inaelekea una Mapenzi na Yu Tong na una uhasamana na Wafanyakazi wa Scania.

Ni kama vile ulienda pale Ofisini kwao Kibaha na hamkukubaliana kuhusu suala fulani basi umewawekea nongwa.
Maana kama Hoja iliyo mezani ni 'Ubora kati ya Yu Tong na Scania' hili la kwamba wafanyakazi wa Scania hawatujali watanzania na wako pale kula mishahara yao tu la nini??

Umesema kuwa bei ya basi la Scania ni ghali kwa mara Tatu zaidi ya lile la Yu Tong, Ungefanya jambo jema sana kama ungeweza kuweka angalau bei roughly ya mabasi ya kawaida ya makampuni hayo ili na sisi tuhakikishe.

Kukazania tu kuwa Scania ni ghali mara tatu kuliko Yu Tong bila angalau kutoa tu ushahidi wa tarakimu ni kutotutendea haki WanaJF wenziao.
Hujatupa pia takwimu kuonyesha wamiliki wa mabasi ya Scania walioshindwa kulipa mikopo na kufilisika.

Sisi wengine tunapoangalia kampuni kama ABOOD, HOOD, DAR EXPRESS na kadhalika jinsi 'zinavyotesa' na Scania zao tunapata wasiwasi na kauli yako hii.

Nilidhani kwamba Kampuni hizi ndio zingekuwa za kwanza kukimbilia mabasi ya Yu Tong ili kupata unafuu unaosema??

Lakini kubwa ni kuwa ni vyema ukatuwekea hapa bei angalau roughly za mabasi haya ili tuone tofauti yake. Haitoshi tu kudai kuwa bei ya Yu Tong ni rahisi zaidi kwa asilimia 30% kulinganisha na ile ya SCania.
Pia utafanya jambo la maana iwapo utatufahamisha kama Mtu unaponunua basi la Yu Tong kwa mfano, unaunganishiwa hapa hapa Tz ama linaundiwa huko huko China na wewe Unaletewa kwenye Meli??
 
...Mkuu Simba, 'makala' yako ni ndeefu lakini nimeona imekaa kii-'sentimental' zaidi.
Inaelekea una Mapenzi na Yu Tong na una uhasamana na Wafanyakazi wa Scania.

Ni kama vile ulienda pale Ofisini kwao Kibaha na hamkukubaliana kuhusu suala fulani basi umewawekea nongwa.
Maana kama Hoja iliyo mezani ni 'Ubora kati ya Yu Tong na Scania' hili la kwamba wafanyakazi wa Scania hawatujali watanzania na wako pale kula mishahara yao tu la nini??

Hii ni kama vile tatizo ulilo nalo kuhusu Scania ni mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wake na sio Ubora ama udhaifu wa Scania dhidi ya Yu Tong!

Umesema kuwa bei ya basi la Scania ni ghali kwa mara Tatu zaidi ya lile la Yu Tong, Ungefanya jambo jema sana kama ungeweza kuweka angalau bei roughly ya mabasi ya kawaida ya makampuni hayo ili na sisi tuhakikishe.

Kukazania tu kuwa Scania ni ghali mara tatu kuliko Yu Tong bila angalau kutoa tu ushahidi wa tarakimu ni kutotutendea haki WanaJF wenziao.
Hujatupa pia takwimu kuonyesha wamiliki wa mabasi ya Scania walioshindwa kulipa mikopo na kufilisika.

Sisi wengine tunapoangalia kampuni kama ABOOD, HOOD, DAR EXPRESS na kadhalika jinsi 'zinavyotesa' na Scania zao tunapata wasiwasi na kauli yako hii.

Nilidhani kwamba Kampuni hizi ndio zingekuwa za kwanza kukimbilia mabasi ya Yu Tong ili kupata unafuu unaosema??

Lakini kubwa ni kuwa ni vyema ukatuwekea hapa bei angalau roughly za mabasi haya ili tuone tofauti yake. Haitoshi tu kudai kuwa bei ya Yu Tong ni rahisi zaidi kwa asilimia 30% kulinganisha na ile ya SCania.

Pia utafanya jambo la maana iwapo utatufahamisha kama Mtu unaponunua basi la Yu Tong kwa mfano, unaunganishiwa hapa hapa Tz ama linaundiwa huko huko China na wewe Unaletewa kwenye Meli??
 
Hahaha mkuu pole, naona kama umechukia, nilikuwa nakutania kuwataja wafanya wa scania na wala sipajui hapo scania kibaha.

Ila mimi ni researcher ndugu yangu na ninazo statistics na si vema kuzitaja ila hata hao uliowataja nina uhakika watakubaliana nami, maana ni kweli wanazo scania na wanajitahidi tu, lakini nina wasiwasi ikiwa wakiongeza wataongeza kwa kununua scania.

Ningependa nikaishia hapo isije kuonekana nina ugomvi na scania ili hali hata kuwajua siwajui ila ninajua mbinu za ndugu zetu za hizi nchi za uaya wanavopenda kuponda chochote kisichotoka kwao. Wanangangania sifa walizokuwa nazo enzi hizo ambazo hawana. Na tukubali era yao kibiashara ishapita hii ni era ya wachina na ili mradi tuhakiki tunachonunua ni kizuri basi tuende na mfuo kwa kuangalia maslhi yetu na sio ya kuiga,

Smba
 
...MKuu Simba, JF is where We dare to Talk Openly, remember??
Umesema upo kwenye research, sawa. Inapotokea mtu anapohoji ulichoandika kwenye andiko lako ni lazima mtu huyo awe amechukia??
Utafeli.
Tuwekee hapa staistic za research yako.Siamini kwamba kuna mtu zitamuumiza kwa namna yoyote ile.
Hivi hata kutuwekea tu hapa bei ya Yu Tong ambayo ni nafuu kwa asilimia 30% dhidi ya ile ya mabasi ya Scania ni statics ambazo si vema kuzitaja hapa?
Basi naomba ufanye Utafiti mdogo tu kwa kupitia Kurasa hizi tatu za mjadala huu uangalie ni wangapi wameikubali Yu Tong na wangapi wameikubali Scania.
Kwa kuwasaidia members wenzako, waonyeshe hawa walioshabikia Scania How they are Wrong and How you are Right kwa kupitia baadhi ya statics zako angalau kwa hilo suala la Bei tu...!
 
kwa walio kwenye mtandao ikiwa mpaka sasa wengi bado walifikiria scania bora kuiko Yutong kutokana na mdahalo huu, hakumaanishi hata siku moja kuwa itakuwa ndio sahihi au ndio itabadilisha ukweli kuwa Yutong ndio bora zaidi, maana inawezekana wamesema hivyo kwa sababu bado Yutong ni ngeni hapa kwetu.

Tukumbuke gari za Japan zilipoingia Africa hususan Tz, watu waliziponda kwa kupendelea peugeot na morris hivi hivi kama wanavofanya kwa magari ya kichina leo lakini leo mjapan NDIE katawala soko. Na waliofaidika zaidi ni wale waliowahi kuelewa kipi kizuri na kutumia za kijapan.

Kuhusu bei niwe mwazi kuwa SIKUSEMA bei pungufu kwa asilimia 30% BALI nimesema BEI YA YUTONG NI ASILIMIA 30% TU YE BEI YA SCANIA. Kwa maana scania marcopolo ilioundwa Brazil na kukamilishwa Afria kusini inamcost mnunuzi ikiwa barabarani kati ya appr Usd 400,000.00 mpaka Usd 420,000.00 wakati bei ya Yutong iloundwa China Kiwandani kwa Yutong wenyewe mnunuzi anaipata hapa Dar Tz pale Mikocheni kwa bei kati ya appr Usd 135,000.00 na Usd 140,000.00 na hizo comparitively uki compare kwa aina na muundo ya bus lenyewe, ikiwa ni pamoja ukubwa wa bus na mashine, nk. Na ubora wa body ambayo ndio muhimu kwenye bus la abiria body ya Yutong ni ya hali ya juu kabisa iliokuwa na usalama wote na ambayo iliofanyiwa test za usalama zote na kuwa na drive line nzuri na kwa hivyo kuwa na ubora wote unaostahili ama kama scania au kuliko scania lakini bado bei YAKE NI THELUTHI ( 30% ) TU ya bei ya scania, na unapata warranty kama warranty inayotoa scania, sasa Je ndugu yangu bora ipi ???

Leo hata mtu akinunua lorry la zamani kuukuu kutoka ulaya ambayo iliozidi mikaka na akaileta Tz na akaikarabati itamcost bei zaidi kuliko hiyo ya bei ya Yutong anaepata mteja hapa Dar Tz, na bado bus hilo kuukuu litakuwa halina sifa yoyote ya usalama, Nadhani suluhisho la wa Tz ni kupata Bus yenye usalama a hali ya juu, na hadhi ya kimataifa na BEI NAFUU,

Kwa hesabu yeyote ile the best economical purchase ni Yutong, ikiwa tunaiangalia kwa mtazamo wa kibiashara kibiashara kiendelevu na kiusalama, ila kama mtu ana fuata jina tu basi hayo ni mengine,

Natumai haya machache kidogo yatasaidia.
 
kama yutong ni bora kuliko scania, mbona mayutong mengi yaliyo dar wametoa diff iliyokuja nayo na wamefunga ya Scania, umeshapata jibu heehe

Sio za Dar tu, Yutong zote bongo zinatumia diff ya scania which means mziki wa scania ni balaa.
 
Mbona songea kuna Yotung za Superfeo kila siku za kwanza kufika hapa songea tena ziko 4 kwa siku(songea dar then 4 dar songea)na scania za Ottawa zinatimuliwa vumbi wakati zinatoka muda mmoja songea au dar?songea kuna milima sana but still zinatembea?Yutong zinapendwa kwa vile ziko economical na hela inarudi kikubwa ni kufanya maintenance na ikifika muda flani inabidi gari ulipungizie ruti ndefu,scania vifaa vyake ni ghari sana once ikiaariba na kurudisha hela inachukua muda mrefu sana ukilinganisha na yotung

Mzee mziki wa Superfeo mbona ni noma, those guys walinibeba one time kutoka moro-dar nilikubali!
 
Mzee mziki wa Superfeo mbona ni noma, those guys walinibeba one time kutoka moro-dar nilikubali!

Umeoonaa eehhh mkuu hapa tunataka facts kama nyie milioona na kupanda,mbeya kuna mabus ya Green star,Ndenjela na JM yanachelewa sana kutoka dar hadi saa moja na nusu ndo JM lamwisho kuondoka ila cha ajabu yanafika sawa na yaliyoondoka saa 12.kwenye swala la speed,consumption ya mafuta,vipuli,kurudisha pesa ya manunuzi Yutong iko juu zaidi,sikatai scania ni imara ila ghari sana na kurudisha gharama zake ni sawa na kucheza kamali
 
Naona WOTE mnashabikia MBIO.......haya shauri zenu

Belgium.jpg
 
Umeoonaa eehhh mkuu hapa tunataka facts kama nyie milioona na kupanda,mbeya kuna mabus ya Green star,Ndenjela na JM yanachelewa sana kutoka dar hadi saa moja na nusu ndo JM lamwisho kuondoka ila cha ajabu yanafika sawa na yaliyoondoka saa 12.kwenye swala la speed,consumption ya mafuta,vipuli,kurudisha pesa ya manunuzi Yutong iko juu zaidi,sikatai scania ni imara ila ghari sana na kurudisha gharama zake ni sawa na kucheza kamali

Nimesafiri na mabasi mengi sana bongo, yani Superfeo mziki mwingine ndugu, basi ilikuwa inatembea balaa, yani hizo basi nazikubali kinoma, unaona kila mtu siku hizi ana yutong mpaka ngorika. Naskia allys nae alikuwa alete yutong sijui kama zimefika
 
kama unataka kujua yutong inakimbia kuliko scania panda haya mabus ya greenstar dar-mwanza route,utapata jawabu,inshort yutong zinatembea mkuu,dont try kushindanisha scania na yutong
allys_bus__-ok_2.jpg

Mkuu, kabla hajaahirisha kwa muda safari za Dar - Mwanza, hakuna mtu aliyekuwa anagusa huu moto! Sio Yutong, UD, Nissan...walikuwa wanaunga tela...kabla ya tochi na ratiba maalum za muda wa safari, ngoma hii Dar saa 12 na kwenda mwanza saa 1 usiku... SCANIA is another thing boss, yutong, they are trying.
 
Back
Top Bottom