Yutong na Scania

unachobisha nini sasa au unataka na ushuhuda wa picha iyo majinja yako inavogonga matako ya wenzie ikipitwa?
J̤̈ä̤m̤̈ä̤ä̤ ä̤n̤̈ä̤b̤̈ï̤s̤̈ḧ̤ï̤ä̤ ṳ̈z̈ë̤ë̤f̤̈ṳ̈ n̤̈ä̤ s̤̈ï̤ö̤ ṳ̈z̤̈ö̤ë̤f̤̈ṳ̈
 
We vipi?mbona sikusomi?Kwani marcopolo ni nissan?Marcopolo ni haina mojawapo ya scania buses!
Marcopolo ni kampuni ya brazil inayojihusisha na utengenezezaji wa body za magari ya abiria, kwa TZ ni kama Dar coach, Quality Body etc, hamuoni marcopolo za tata tena hizi ndogo tuu za watu 30-40!!?,
Irzar,tirino,paradise etc ni version za marcopolo zilizoboreshwa, mfano samsung galaxy then s1.... S7
 
Kuna ile Scania ya Majinjah Dar-Sumbawanga ile ni noma aisee,nadhani njia nzima ya Mbeya hana mpinzani kwa mwendo. Unatoka Dar saa12 asubuhi unafika Sumbawanga saa6 usiku.
Ile bas hapan nmewah panda njia nzima unasali sio mwendo ule
 
Mkuu Dar Mwanza au Dar Kahama kwa mbio zinatisha Kisbo na Cityboy ambazo ni scania. Wakuu, scania ni namba nyingine ikishachanganya hakuna basi inayogusa. Uliza kuna happynation zilikuwa scania za mbeya hakuna basi ilikuwa inagusa. Scania busses zipo vzuri sana kwa mbio na uimara. Udhaifu pekee wa scania busses zilizokuwa zinakuja tz zilikuwa hazina AC. Ila hapa juzi kati nilipanda scania bus yenye ac ilikuwa matata sana.

Tukija kwa Youtong zinachakaa haraka sana; ukiangalia scania za abood hadi leo zipo fresh na zina kama miaka kama kumi hivi lkn yutong za BM zina miaka kama sita hivi lkn zmechoka mbaya.
Now abood ana yutong kama 4 hvi za moro dar naona kaanza kuhama scania
 
we CHAZA hzo hesabu ulizopiga ni za wap ? huez kuwa na average ya 120km kwa saa ukiwa na bus ata vitz haiwezekani average spd huwa ni ndogo sana kuliko unavydhan .......average kubwa niliowah iona kwa 330km from arusha tu singida, bus lilikuwa ni mghamba ambapo lilitumia masaa matatu na dk 55 sawa na average ya 86km/hr ... afu ww unaongelea average ya 120 haiwezekan hata kidogo
Amezungumzia masaa 6 kutoka Dar hadi Moshi. Ili ufike kwa muda huo, kwa wakati ule tochi zilikua hamna, nikasema kama basi likitunia Speed ya 120km/h ambayo kwa zamani ilikua ni speed za kawaida kwa Mabasi kama Ngorika nk kwa wakati ule. Sasa ukiongeza nusu saa za kudelay mizani Kibaha(kwa zamani),kuchinba dawa au Chakula Korogwe, basi masaa sita ni kawaida. Kwa kilometa 562 za Dar hadi Moshi kufika saa6 ni sahihi tu, kwa mwendo nilioutaja huku ikiongezeka na kupungua kwenye matuta, miiunuko na kwenye msururu wa malori yanayoongozana.
 
Yutong ni gari nzuri ya kibiashara na mbona zina mudu hata safari ndefu mf Dar to Bukoba n.k nimesafiri nazo sana ziko poa sana.
 
Ahsante mleta uzi...Kuna vitu nimejifunza leo tena vingi tu japo sijapenda kuishindanisha SCANIA na YouTong
Kama umeizalilisha hivi...anyway ahsante nimejifunza vingi leo
 
Now abood ana yutong kama 4 hvi za moro dar naona kaanza kuhama scania
Yutong ni bei rahisi kuliko Scania, kwaajili ya kushindania soko lazima anunue yutong nyingi kwa hela ndogo. Kumbuka hela ya Scania moja marcopolo unaweza pata Yutong nne. Ili kuzidi kuliteka soko la moro dar ni lazima afanye hivyo. Hata hivvyo in the long run Scania inalipa vzuri kuliko Yutong. Kumbuka Yutong inavorudisha hela yako nayo inakuwa imechoka wakati Scania inavokuwa imemaliza kurudisha hela yako inakuwa bado ipo bomba sana.
 
Katika udadidi tu wa kawaida pale UBT, nilikaa na mdau mmoja ofisi ya moja ya kampuni kubwa yenye mabasi mengi ya Yutong. Aliniambia matajiri wenye Yutong mpya nyingi hupata faida kubwa tu.
Wanachofanya, akiagiza gari kama 30 huzitumia kwa miaka miwili au mitatu. Akadai kwa muda huo hela zake za kununulia basi zinakua zimerudi. Baada ya hapo huuza kwa wafanyabiashara wa kipato cha kati. Kumbuka basi linakua bado liko na hali nzuri. Atauza kila basi kati ya 100-120m/-! Na hapo ndipo anapopata faida. Alinitajia mabasi mawili(sitaki kuyaweka hapa majina). Hayo yana namba za usajili toleo C, yaani bado liko katika hali nzuri.
Nikagundua, ukiwa na hela, utapata hela tu.
 
Hayo yote yanawezekana mkuu, biashara ni kucheza na faida ya muda mrefu na faida ya muda mfupi.
 
Kutokana na ushindani Wa kibiashara ya kusafirisha abiria imebainika scania wameibuka washindi hasa kwa mwendo na durability hasa kwa safari za mbali,km dsm to mby,dsm to Mt.tulichangie wadau.
Yutong huwezi kulinganisha na Scania.Nia ya Wachina haikuwa kuunda gari ambalo ni bora kuliko Scania,nia ilikuwa kuunda gari ambalo ni cheap,and therefore not as durable as Scania,but which can enable a business person to break even by having a big profit margin.Na hii ndio phylosofy ya biashara ya Mchina,ndio maana wameiteka dunia kibiashara.Sio muda mrefu SCANIA ZITAKOSA SOKO!
 
Yutong ni bei rahisi kuliko Scania, kwaajili ya kushindania soko lazima anunue yutong nyingi kwa hela ndogo. Kumbuka hela ya Scania moja marcopolo unaweza pata Yutong nne. Ili kuzidi kuliteka soko la moro dar ni lazima afanye hivyo. Hata hivvyo in the long run Scania inalipa vzuri kuliko Yutong. Kumbuka Yutong inavorudisha hela yako nayo inakuwa imechoka wakati Scania inavokuwa imemaliza kurudisha hela yako inakuwa bado ipo bomba sana.
Je unajua zile marcopolo za abood zimedumu kwa miaka mingapi hadi sasa na bado zipo vizuri sana kana kwamba zinamwaka mmoja kumbe zinazaidi ya miaka mitatu. Scania ni durable but ni ghari sana kulinganisha na yutong & zhongtong
 
Teh teh teh,Mkuu tukianza kutoa real mifano ya kazi nzito za Scania hawa Team Yutong watakimbia hapa. Kuna Scania moja ya kampuni ya Ngorika ilikuwa inaitwa Macedonia safari ya Dar-Arusha ile kitu ni moto wa kuotea mbali ilikuwa inatoka Dar saa12 asubuhi ipo Arusha saa7 mchana. Kuna kipindi cha Xmas ilikuwa inatoka Dar saa12 asubuhi saa6 kamili ipo Moshi Mjini then inageuza kurudi tena Dar ili kuja kubeba Abiria wa kesho yake asubuhi. Kama una roho nyepesi ulikuwa huwezi kupanda ile Gari na haijawahi kupata ajali hata mara moja mpaka inastaafu kwa utumishi wake uliotukuka.
teh teh teh teh umenikumbusha mbali mkuu Frank Wanjiru MACEDONIA,MACEDONIA ilikuwa moto wa kuotea mbali,kuna nyingine ilikuwa inaenda mbeya inaitwa HAPPY NATION a.k.a SAUTI YA MANKA ilikuwa balaa ndege ya ardhini yaan hapo yutong anakaa kiulaini.
But ata hizi yutong za super feo na new force zimefungwa engine za scania
 
Na Scania Kama zingekuwa hazilipi nadhani Mremi wa Dar Express angekuwa ameshafunga biashara siku nyingi sana,maana yeye tangu aanze biashara ya usafirishaji Mabasi yake ni Scania tuu hana huo uchafu wa Kichina hata mmoja.
haha mkuu umekurupuka,angalia now Dar express kaleta zhongtong na higher kibao,au haupo dunia hii
 
Back
Top Bottom