Yusuph Manji achukua fomu za kugombea uenyekiti wa Yanga!

mafisadi wanajaribu kuingia kila sehemu....kazi kwelikweli....afu ameingia na majina mengi kweli,mara yaoo mara spika...kumbe mtu yule yule amekuja kujisafisha jf...fisadi papa wewe
Kajiunga pia leo pia kwa jina la Gerrard. Manji bwana!!!!
 
Watanzania walivyo wajinga kama Manji atagombea sina shaka yeyote watamchagua.Sijui kwanini watanzania tunahusudu matajiri uchwara.
Yusuph Manji achukua fomu

04/06/2012


Taarifa rasmi na za uhakika alizozipata Shaffi Dauda kutoka makao makuu ya klabu ya Dar Young Africans almaaruf Yanga Sports Club, zinasema mwanachama maarufu na tajiri wa klabu hiyo, mfanyabiashara Yusuph Mehebob Manji amechukua fomu za kugombea nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo.

Manji ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akiisadia Yanga kiuchumi zaidi, alikwenda kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kuchukua fomu za Uenyekiti bila kuweka wazi kama ni kwa ajili yake au amemchukulia mtu kwa ajili kugombea nafasi hiyo.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na taarifa juu ya Manji kutaka kugombea nafasi hiyo japo mwenyewe bado hajathibitisha, ingawa kitendo chakecha leo kimezidi kuupa nguvu uvumi wa kwamba anataka kugombea nafasi ya kuwa bosi wa Yanga.

Wakati huo huo taarifa nyingine zinasema kuwa aliyekuwa mjumbe Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Binkleb naye muda wowote kutoka sasa atadondoka makao ya Yanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea umakamu mwenyekiti.

Mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo Issac Mazwile naye ameshachukua fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.

Naye Mkuu wa wilaya ya Handeni, bwana Muhingo Rweyemamu amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Julai 15, 2012. Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis, Kaswahili amemwambia Dina Ismail kwamba jana kwamba wanachama hao wanafanya idadi ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafsi mbalimbali za uongozi katika klabu hiyo kufikia 10 (baada ya taarifa hapo juu ya Manji kuchukua fomu, sasa idadi itakuwa 11).

Mbali na hao, wanachama wengine waliochukua fomu ni pamoja na John Jambele anayewania Uenyekiti, huku Ayoub Nyenzi akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, “Waliochukua fomu kuwania ujumbe wa kamati ya Utendaji mbali na Muhingo na Binkleb ni Isaac Chandi, Jumanne Mwamwenye na Salehe Hassan,” alisema.


Source: wavuti - wavuti
 
Kama Manji amechukua form ya kugombea uenyekiti Yanga ujue Yanga inakwisha. Na waelewe atakuja kugundua madudu yote ya yeye kuibiwa pesa na akina Madega na Nchunga na hiyo itapelekea yanga kuwa na hali ngumu siku chache zijazo.
 
watu wanatuvurugia mada kwa sabb ya wivu tu.Wanaona yanga inaelekea kuwa kama man city! Wanaona sasa tunakuwa tunachuana na Azam badala ya simba
siamini kama kwenye timu yangu ya yanga kuna watu viberenge kama wewe, yanga chini ya manji kuwa kama man city? ahahahaha, acha utoto aisee. kuna siku yanga itauzwa, haitakuwa timu ya watz tena, itakuwa timu ya manji, yeye kama anataka kumiliki timu, aanzishe kama wanaume wenzie kina bahkresa wa azam, na dewj, asilete mambo ya kudandia vya watu kama mtoto wa kike, yanga ina historia yake, ufisadi hatuutaki...na wale wazee wachawi na sura zao kama wwanakula watu hatuwataki yanga, vipo pale wakipewa hela ya kunywa kahawa na kashata na manji basi wanajifanya kuita vyombo vya habari, hivi yanga itatawaliwa na wachawi wazee wale hadi lini? vijana wako wapi? .......manji hatukutaki yanga...hatukutakii kabisa.
 
Umaskini wa akili wa wanachama na washabiki wa 5STAR wazee wa 5-0 wa Kuamini Mafisadi Ndo mwarobaini wa shida zao Nikutia Petrol kwenye moto ukidhani ni maji. Wajinga ndo waliwao Siku zote
 
Commercial Break Simba baada yatwaa ubingwa1-5.jpg
 
siamini kama kwenye timu yangu ya yanga kuna watu viberenge kama wewe, yanga chini ya manji kuwa kama man city? ahahahaha, acha utoto aisee. kuna siku yanga itauzwa, haitakuwa timu ya watz tena, itakuwa timu ya manji, yeye kama anataka kumiliki timu, aanzishe kama wanaume wenzie kina bahkresa wa azam, na dewj, asilete mambo ya kudandia vya watu kama mtoto wa kike, yanga ina historia yake, ufisadi hatuutaki...na wale wazee wachawi na sura zao kama wwanakula watu hatuwataki yanga, vipo pale wakipewa hela ya kunywa kahawa na kashata na manji basi wanajifanya kuita vyombo vya habari, hivi yanga itatawaliwa na wachawi wazee wale hadi lini? vijana wako wapi? .......manji hatukutaki yanga...hatukutakii kabisa.

Man city imeuzwa kwa waarabu,Man united na liverpool zimeuzwa kwenda kwa wamarekani,Chelsea imenunuliwa na mrusi,kuna timu zaidi ya 7 za uingereza zinamilikiwa na wageni na wazawa wa uingeleza hawakuwa na wivu na ubaguzi kama wako.Inshort yanga na simba hazibadiliki bcoz of wanachama kama nyie,tangu karume awajengee jengo mlishindwa hata kulipaka rangi kwa zaidi ya miaka 66, hadi manji alipojitolea kulikarabati...
 
sidhani kama una imani..you seem to be a dead man walking to me ...dunderhead
Vyovyote inavyokuwa... You are dead man too...Unashindwa hoja unaanzisha matusi.. Watu wengine wana makororo kwenye mbongo zao. Subiri uchaguzi ufanyike Manji atagombea na ukapige kura ili ashindwe badala ya kuropoka ropoka kwenye mitandao kama mtu aliyekosa uelekeo
 
yap, mahela yake ya ufisadi. no wonder hata tiketi za kuingilia uwanjani alishawahi kuamuru ziandikwe maandishi ya kuran, akifikiri wana yanga wote ni waislam....

Kwasababu button ya "DISLIKE" hamna mimi nitakuwa naangusha DISLIKE ya kuandika kwa "*****" wote wa aina hii
 
umaskini wa akili wa wanachama na washabiki wa 5star wazee wa 5-0 wa kuamini mafisadi ndo mwarobaini wa shida zao nikutia petrol kwenye moto ukidhani ni maji. Wajinga ndo waliwao siku zote

"dislike"
 
Sasa Yanga kwisha. Huyu Manji aliitaka hii timu muda mrefu, kumbukeni lile Sakata lake la kuifanya Yanga kampuni na awe mmiliki wake. Zogo hili liliendelea na wale ambao walimpinga alifanya kila aliloweza wakaondoka. Nina wasiwasi hata huyu kiongozi aliyeondoka ni kuwa alishawahonga wale wazee ambao hawana kitu ni vibaraghashia tu na yeboyebo!! Lazima kuna biashara anataka pale si bure!!! Hivi si mnajua tena mambo yalee ndani ya balls!! Si bure nawaambia, kuna kitu!! Kwa uchungu gani alio nao kwa watanzania? Angekuwa na uchungu nasi asingekuwa miongoni mwa mafisadi. Kwelii nchi hii sijui haina wenye mamlaka au nisemeje? Pewwwwwwwwwwwwwwwww.

Nchi hii imejaa wafikiriao kwa Masaburi kama wewe,ulitaka Yanga iendelee kuendeshwa kimaskini ili mechi inayokuja itukute kwenye mgogoro,wachezaji hawajalipwa mishahara yao na element za kuharibiana za ndani kwa ndani ili mtufunge tena?,PERIOD.
 
Kama Manji amechukua form ya kugombea uenyekiti Yanga ujue Yanga inakwisha. Na waelewe atakuja kugundua madudu yote ya yeye kuibiwa pesa na akina Madega na Nchunga na hiyo itapelekea yanga kuwa na hali ngumu siku chache zijazo.

Aina ya jina kweli hu'reflect hali ya mtu,wewe kweli Mzee wa njaa tena siyo ya chakula tu hata ya mawazo,...kugundua madudu yaliyokuwa yanafanywa na waliokuwa wakipokea ufadhili kutoka kwake ni kuifikisha Yanga kwenye hali ngumu,ndo uelewa uliojengewa kule kwenye shule yako ya kata ulipohitimu?
 
Back
Top Bottom