Yule shabiki wenu aliyemkumbatia Kaka - yataka moyo!.

Kijana hana kosa.
Katika jambo kubwa kama lile la Brasil vs Tanzania ilikuwa ni lazima jambo kama lile kutokana, na hii siyo kwa bongo tuu wazee, hata huko ughaibuni nako tunashuhudia hayo kila leo, na sometime yanakuwa makubwa zaidi ya hayo.

Tatizo ni jinsi sisi wabongo tunavyo yashughulikia matatizo yetu. Inasikitisha kuona Polisi walivyompa tafrani yule kijana, aisee...!! Nahisi tunahitaji kubadilika wandugu, tunahitaji pia kujiboresha, tuahitaji hasa kuwa serious japo kidogo waungwana. Hebu jiulize kidogo haya maswali...

  • Hivi vyombo vya usalama havikutegemea kukutanana na jambo kama hili?

  • Je, kama walitegemea walijiandaa vip kulikabili?

  • Hivi kipigo, matumizi ya nguvu, ubabe na uvunjaji wa sheria ndio muhimili wa jeshi letu la polisi?

  • Hivi zipo kweli juhusi za makusudi za kuifanya Tanzania ifanane na nchi nyingine zilizoendelea?

Hongera kijana, maana kwa watu wenye akili wangetumia kile alichokifanya ili kuiboresha kesho yetu na si kumuadhibu kwa marungu na ngumi. Japo na amini ililazimu kufanya kitu fulani ili kuepuka jambo kama hili kujitokeza tena huko mbeleni, lakini lazima iwe adhabu yenye kujenga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom