Yule mwanamke muuaji wa sumu: hitimisho lake limekamilika jioni hii!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Kwa mnaokumbuka kile kisa cha mwanamke alotaka kumuua mumewe kwa kumuwekea sumu ktk chakula leoo familia imeyamaliza ktk kikao kilichomalizika robo saa iliyopita.

Kifupi ilikubaliwa na mwanamke mwenyewe alikubali kuchukua nyumba moja. Yeye ndiye atakuwa 'mmiliki' wa hiyo nyumba kwa kuchukua kodi na kuitumia kwa mahitaji yake. Hata hivyo kwa kuwa nyumba hiyo iliandikishwa kwa jina la mtoto, ndugu walishauri asipewe hati ya nyumba wakichelea kwamba anaweza akaiuza, kutokana na uwaruwaru wake. Na leo ndo wametangana rasmi masikini. Jamani haya mapenzi, yanatia uchungu sana unapowaona wahusika wanaachana, inatia huzuni kweli!

Majadiliano yalikuwa makali kwani mke alitaka apewe gari pia. Alipokumbushwa kuwa hiyo ya kuachiwa kodi ya nyumba ni hisani tu ya mume, na kwamba alipaswa awe kolokoloni muda huu, alikubali kwa shingo upande. Hata hivyo ndugu wa mke walishukuru sana kwa jambo hili kumalizwa kifamilia zaidi badala ya kwenda mahakamani.

Niwaache wanjf, maana nadhani nilipaswa kuwapa final rulling ya hili jambo nililowaletea mwezi jana.

(LIVERPOOL POLENI SANA KWA YALIYOWAKUTA LEO KWENYE SHAMBA LA BIBI, OLD TRAFFORD)
 
Kwa mnaokumbuka kile kisa cha mwanamke alotaka kumuua mumewe kwa kumuwekea sumu ktk chakula leoo familia imeyamaliza ktk kikao kilichomalizika robo saa iliyopita.

Kifupi ilikubaliwa na mwanamke mwenyewe alikubali kuchukua nyumba moja. Yeye ndiye atakuwa 'mmiliki' wa hiyo nyumba kwa kuchukua kodi na kuitumia kwa mahitaji yake. Hata hivyo kwa kuwa nyumba hiyo iliandikishwa kwa jina la mtoto, ndugu walishauri asipewe hati ya nyumba wakichelea kwamba anaweza akaiuza, kutokana na uwaruwaru wake. Na leo ndo wametangana rasmi masikini. Jamani haya mapenzi, yanatia uchungu sana unapowaona wahusika wanaachana, inatia huzuni kweli!

Majadiliano yalikuwa makali kwani mke alitaka apewe gari pia. Alipokumbushwa kuwa hiyo ya kuachiwa kodi ya nyumba ni hisani tu ya mume, na kwamba alipaswa awe kolokoloni muda huu, alikubali kwa shingo upande. Hata hivyo ndugu wa mke walishukuru sana kwa jambo hili kumalizwa kifamilia zaidi badala ya kwenda mahakamani.

Niwaache wanjf, maana nadhani nilipaswa kuwapa final rulling ya hili jambo nililowaletea mwezi jana

(LIVERPOOL POLENI SANA KWA YALIYOWAKUTA LEO KWENYE SHAMBA LA BIBI, OLD TRAFFORD)

Thank you for the update ndokyo! Iam still puzzled mwanamke alikuwa anawaza nini huyu! Kazi kwelikweli!
 
stori nzuri.

Ila umekuwa kama u.m.e.j.a.m.b.a high table
baada ya kuingiza kibwagizo cha mpira hapa
nna mood swing sasa hivi.
 
Sikujua kama natupa mawe ikulu, nisamehe sometime furaha huondoa hupelekea busara kwenda likizo kidogo!
 
Back
Top Bottom