Elections 2010 Yule Asha Mtwangi aliyemhoji Rais ni mtumishi wa Ikulu?

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,534
8,619
....Hivi mbona jana JK hakuhojiwa na Rose MWAKITWANGE kama ilivyokuwa imepangwa ....maana yule dada ASHA MTWANGI aliyemuhoji ni moja ya waajiriwa wa IKULU chini ya kurugenzi ya habari ........inayoongozwa na SALVA RWEYEMAMU...na kuna wengine pale wakiwamo waandishi wasaidizi waandamizi ie Primi Kabanga...na wengine waandishi ambapo mmoja wao ni Huyu ASHA MTWANGI....

SO tuseme mahojiano ya jana yaliandaliwa na kuendeshwa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais.....
 
Mimi sikuona mwanzoni, kwani wakati anaanza kumhoji Rais hakujitambulisha nafasi yake ili awe amedeclare interests? Au hawakuona a major conflict of interests kwa mwajiriwa kumhoji mwajiri wake hasa mwajiri huyo akiwa ndiye Rais? I hope its not true aisee maana vikashfa vingine haviingii hata akilini..
 
Kwani we hukuona hata maswali aliyokuwa anaulizwa? We utaulizaje eti "Mgombea kama ukipata ridhaa unatuahidi nini kwenye elimu?" au "Kwa kipindi cha miaka mitano ulifanya nini katika elimu?"

Hivi hapa unategemea mtu akose jibu kweli?

Angalia swali kama la Kibonde la 2025 millenium goal lilivyomtoa nishai. Kwanza sidhani kama anazijua hizo goals za 2025!! ah, anaboa tu.
 
kuna watu hawaitakii mema tanzania......wanapanga ujinga kila siku....watakufa na dhambi nyingi
 
kweli,walau Ephraim alikunja swali kidogo..majibu yangekua fikirishi kwa wanaoomba kuingia ikulu kwa mara ya kwanza ila sikuona sababu ya jk kua mwepesi kiasi hiki ikiwa ana experience kwenye mambo ya uongozi..
 
Hata swali la Kibonde tayari alikuwa ameshaandaliwa majibu ila inaonyesha jamaa hakuwa makini kudesa...

Nilichojionea na kujifunza jana ni kuwa Congressional Corruption Movement (CCM) ni chama cha wazee ambao mbaka wafe ndipo Tanzania itakuwa na mafuriko ya maendeleo tunayoyatamania...

Wanachakachua kila kitu wakisaidiwa na mataifa makubwa ya dunia hii...
 
Asha Mtwangi siyo mtumishi wa Ikulu tena.. alikuwa enzi za kipindi cha awamu ya tatu.

Sasa hivi anafanya kazi kwenye International NGO moja ya kimarekani
 
jamaa alikuwa kama yupo kijiweni anapiga story, wala sikuona la maana aliloliongea
 
....Hivi mbona jana JK hakuhojiwa na Rose MWAKITWANGE kama ilivyokuwa imepangwa ....maana yule dada ASHA MTWANGI aliyemuhoji ni moja ya waajiriwa wa IKULU chini ya kurugenzi ya habari ........inayoongozwa na SALVA RWEYEMAMU...na kuna wengine pale wakiwamo waandishi wasaidizi waandamizi ie Primi Kabanga...na wengine waandishi ambapo mmoja wao ni Huyu ASHA MTWANGI....

SO tuseme mahojiano ya jana yaliandaliwa na kuendeshwa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais.....
 
Mtangazaji mmoja wa redio amekiri yale maswali walimpelekea ayaandalie majibu. JK sasa amekua kituko tanzania, ni mtu mbaya anang'ang'ania madaraka - tumwogope
 
Asha Mtwangi siyo mtumishi wa Ikulu tena.. alikuwa enzi za kipindi cha awamu ya tatu.

Sasa hivi anafanya kazi kwenye International NGO moja ya kimarekani

lakini amewahi kufanya kazi na timu hiyo hiyo na chini ya bosi huyo huyo au alikuwa Ikulu wakati wa Mkapa?
 
kwa jinsi nchi inavyoendeshwa, sishangai, kwani nani anajua kama rose hakua na interest na chadema??? in short ni kwamba kila kitu kimechakachuliwa tukapewa mafamba... A GOOD MIALOGUE INAHITAJI NEUTRAL PERSON NA AHOJI WOTE PAPO KWA HAPO SIO HIZI BREAKFAST FORUMS AT NIGHT
 
Asha Mtwangi siyo mtumishi wa Ikulu tena.. alikuwa enzi za kipindi cha awamu ya tatu.

Sasa hivi anafanya kazi kwenye International NGO moja ya kimarekani

ukishakuwa mtumishi wa ikulu ....umekuwa na utakuwa ...muda wowote utakaohitajika ku serve you must oblige...ndio maana jana Asha [a seasoned journalist]...alikuwa prefered to Rose Mwakitangwe....[experienced journalist and panelist too]...its the devil you know!!!.....

Pamoja na hayo kuna muda uzalendo ulimshinda Asha akampasha JK kuwa anachukua muda sana kuzunguka maswali ....na akamtahadharisha kuwa itafanya maswali mengine yashindwe kuulizwa pale muda utakapoisha!!!...pamoja na dessa ...jk alikuwa anayajuwa maswali ...alitumia muda mwingi kujibu maswali ili baadhi yasiulizwe....who knows labda swali la baba mama watoto lilikuwapo!!!....kuna muda aliulizwa na mungy kuhusu matibabu ya viongozi aliuzunguka wee hadi suzy akanuna kweli...nadhani alijutia nafsi yake kuwa kwenye ile panel ya kumlamba JK viatu ukizingatia naye ni mwandishi mwandamizi ....na alikuwa na Asha miaka hiyo ..wakabaki wanaangaliana na Asha!!
 
Hivi kwanini hawakumuuliza kama akishindwa atakubali matokeo? that is the only question I wanted to hear his response to.
 
Mimi sikuona mwanzoni, kwani wakati anaanza kumhoji Rais hakujitambulisha nafasi yake ili awe amedeclare interests? Au hawakuona a major conflict of interests kwa mwajiriwa kumhoji mwajiri wake hasa mwajiri huyo akiwa ndiye Rais? I hope its not true aisee maana vikashfa vingine haviingii hata akilini..

Usijifanye hujui!
 
Hivi kwanini hawakumuuliza kama akishindwa atakubali matokeo? that is the only question I wanted to hear his response to.
angeanguka aisee... kuna maswali yanaweza kukupa presha... yeye ameomba wengine wakubali matokeo tu, hayo ya yeye kukubakli ni issue nyingine
 
lakini amewahi kufanya kazi na timu hiyo hiyo na chini ya bosi huyo huyo au alikuwa Ikulu wakati wa Mkapa?

Wakati JK anaingia Ikulu Asha alikuwa katika kitengo cha mawasiliano nadhani wakati huo kilikuwa chini ya Peter kalaghe. baada ya muda kitengo hicho kikashikwa na Salva ambaye punde alimtimua Asha kwa madai kwamba kulikuwa hakuna budget katika nafasi hiyo.

Lakini hii si kweli -- ukweli ni kwamba Salva hakuwa anamuafiki baba yake Mtwangi -- Khaliud Mtwangi ambaye ni mwandishi maarufu wa makala za kupinga establishment.
 
Wabongo tunabishana nini jamani ?? Mlitaka amweke nani ?? Salva rweyemamu ?? Hiyo haiwezekani
asha mtwangi ndio anayefaa ili kuwaficha watu jamani. Cha msingi kwangu mimi na wewe kuelewa
ni ile connection yake aliyokuwa nayo na ikulu. Nyie wabongo mnajua kwamba kupata kazi mahala
siyo lazima umjue bosi bali ukimpata mtu anayefahamiana na wahusika kule ndani hiyo pekee inatosha.
Ikulu ilikuwa inatafuta mtu wa nje lakini wanamfahamu ili awatengenezee igizo lao na asha mtwangi
was the right person.
 
Back
Top Bottom