Yuko wapi Wilfred Lwakatare?

nafikiri sana anajuta sna. Walimdanganya sana CHADEMA. na kwa jinsi ninavyoijua Bukoba mjini sijui kama atashika nafasi ya nne katika UBUNGE.

naomba hii muiNOTE kisha mniulize baada ya uchaguzi.

Watu hawana inami naye ni ndumilakuwili tu.

Uko sawa kabisa mkuu,jamaa alidhani akihama cuf atahama na wanachama wake.hali imekuwa tofauti.juzi nilikuwa bk wakati wa uchaguzi wa selikari za mitaa.niligundua cuf bado wako juu bk mjini na km mwakani watapata mgombea makini,rwakatre atakuwa amefulia mazima.
 
sasa tuone kama Yeye Rwekatare atakuwa hata mshindi wa nne katika Uchaguzi wa ubunge wa Bukoba mjini.

naweza kukuthibitishi kuwa baada ya CHADEMA kujulikana kama chama cha KIDINI na UKABILA sijui kama watashinda kule Bukoba na Kigoma.

Kujulikana kwa nani? Halafu anayetoa uthibitisho wa shutuma hizi ni CUF! Iko kazi. Kweli nyani haoni.......

Uwe unaona aibu siku nyingine. Si kila kitu lazima kiangaliwe kwa msingi wa dini kama unavyofanya wewe. Tuachie Tanzania yetu wewe bakia na huko uliko.

Amandla........
 
Kumbe wewe umeuliza swali hili kwa lengo la kutaka kumdhalilisha Lwakatare? Huyu bwana amefanyakazi kubwa sana kule Bukoba katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Chadema kimeshinda viti vingi kuliko hata hiyo CUF. Tusubiri tuone uchaguzi ukifika..
 
Siwaamini sana mijitu inayohama hama vyama hata siku moja...? if there is problem you solve it siyo kuhama/kukimbia chama well labda anaweza kuwa useful kwa chadema time will tell!
Lakini usisahau wafuatao waliokimbia vyama vyao..
tambwe (hopeless man), kabouro (hopeless man), masumbuko (hopeless man) lyatonga (ametuchosha wanamageuzi) ..the list goes on...
All the best lwakatare..however, you will never never get a trust from me...

Naghadhibika maradufu endapo uhamaji huo umetokana baada kuvuliwa madaraka kwa tafsiri yoyote ile!!!
 
Re: Yuko wapi Wilfred Lwakatare? Kumbe wewe umeuliza swali hili kwa lengo la kutaka kumdhalilisha Lwakatare? Huyu bwana amefanyakazi kubwa sana kule Bukoba katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Chadema kimeshinda viti vingi kuliko hata hiyo CUF. Tusubiri tuone uchaguzi ukifika..

Wahenga walisema "aulizaye ataka kujua"
 
Tumuombee mema na matokeo mema ya baadae kwa kumpa mikakati mizuri ya kulikabiri jimbo la Bukoba mjini.

Bukoba na mkoa mzima wa kagera ukiondoa wilaya ya Ngara una siasa chafu za kidini na kikabira au kiukoo. Lwakatare analijua vizuri jimbo lake la Bukoba mjini lakini anatakiwa awe na maono mapya na mbinu mpya za kulirejesha jimbo hilo mikononi mwa Chadema.
Ana kazii kubwa ya kufanya ila tumpe mchangowetu wa mawazo ili afanikishe malengo ya chama cha Chadema kuliko kumkatisha tamaa.

Tuijenge Tanzania kwa michango yetu mizuri ya mawazo ili tuwafukuze mafisadi wa CCM.
 
Lwakatare: Sikuhamia Chadema kutafuta cheo

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananci (CUF), Wilfred Lwakatare, amesema hakuhamia Chadema kusaka cheo, bali amegundua kuwa chama hicho kunawapambanaji wa kweli dhidi ya ufisadi.

Aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya Tangamano wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Operesheni Sangara inayoendeshwa na Chadema.

Lwakatare alisema Chadema kuna watu makini ambao wana uchungu wa kweli na rasilimali za nchi. “Nilimwambia hata Mbowe, mimi sikuja kufuata cheo maana kama kusoma nina elimu ya kutosha kufanya kazi popote, isipokuwa nataka kuendeleza mapambano dhidi ya wezi wa mali za umma. Septemba 2007 pale Mwembeyanga mlitangaza majina ya mafisadi waziwazi bila woga pale ndipo nilipobaini kuwa huku kuna wanaume wa shoka,” alisema Lwakatare.

Alisema baadhi ya vyama vya upinzani vinafanya siasa za kujitafutia umaarufu binafsi, badala ya kutafutia wananchi ukombozi.

Alisema baadhi ya vyama hivyo vinaendeshwa kama asasi zisizo za serikali. Lwakatare alisema kazi ya kuiondoa CCM madarakani sio lelemama kama watu wanavyoweza kudhani, ni ngumu inayohitaji kukomaa.

Naye Joseph Selasini, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi NCCR Mageuzi, alisema kuna vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikiibuka wakati wa uchaguzi.

Selasini alisema vyama hivyo viliandikishwa tangu kuingia mfumo wa vyama vingi, lakini vina hali mbaya kutokana na kuendeshwa kihuni.

“Wakazi wa Tanga tuungane tutengeneze ngumi ya nguvu tuitandike CCM, mageuzi ni muhimu maana tuna tatizo la uongozi, nchi inaongozwa kisanii na CCM imefulia kisera,” alisema.

Aliongeza kuwa badala ya kuwaletea wanachi maisha bora, CCM imekuwa wakati wa uchaguzi ikiwaletea wananchi fulana tena za bei rahisi ambazo huchanika muda mfupi.
 
Acha uzushi, dalili ya mvua ni Mawingu; chini ya Mwenyekiti Lwakatare CHADEMA imeshinda mitaa na vijiji kuliko chama chochote cha upinzani majimbo yote ya mkoa wa Kagera ikiwemo jimbo lake la Bukoba Mjini

Asha
Mheshimiwa kwa vijembe?utafikiri uko kwenye rusha roho? by the way sijawahi kukuona kwenye mambo kama hayo au wewe ni jinsia nyingine?
 
Kujulikana kwa nani? Halafu anayetoa uthibitisho wa shutuma hizi ni CUF! Iko kazi. Kweli nyani haoni.......

Uwe unaona aibu siku nyingine. Si kila kitu lazima kiangaliwe kwa msingi wa dini kama unavyofanya wewe. Tuachie Tanzania yetu wewe bakia na huko uliko.

Amandla........
Lwakatare hakuwa muislamu ndo maana walimfukuza, CUF ni ya waislam(bisha au usibishe, huo ndio ukweli)!.
Unamfahamu Tambwe Iza? muulize kilichompata mpaka akahamia CCM.
 
Ulikuwa unaaminika lkn kwa Hili la kusema CUF ndio linatoa shutuma za UDINI na UKABILA wa Chadema ni kufulia kwa Hali ya JUU...Kwa kanuni za Logic....Chadema ndio inatoa shutuma za UDINI kwa CUF kweli?..kwa utaratibu huu CCM itaendelea kushinda Daima!!!

...Hio IKO wazi unaipata wapi? Are u trusting JF members kwa emotions zao za Vyama?Una hakika member fulani ni mwanachama wa CUF/Chadema/CCM thru contribution zao?
 
Lwakatare hakuwa muislamu ndo maana walimfukuza, CUF ni ya waislam(bisha au usibishe, huo ndio ukweli)!.
Unamfahamu Tambwe Iza? muulize kilichompata mpaka akahamia CCM.

Very low contribution...!!!
 
Uko sawa kabisa mkuu,jamaa alidhani akihama cuf atahama na wanachama wake.hali imekuwa tofauti.juzi nilikuwa bk wakati wa uchaguzi wa selikari za mitaa.niligundua cuf bado wako juu bk mjini na km mwakani watapata mgombea makini,rwakatre atakuwa amefulia mazima.
Chadema walipata viti vingapi na kafu walipata viti vingapi?
Ondoa uzushi hapa jf
 
Ulikuwa unaaminika lkn kwa Hili la kusema CUF ndio linatoa shutuma za UDINI na UKABILA wa Chadema ni kufulia kwa Hali ya JUU...Kwa kanuni za Logic....Chadema ndio inatoa shutuma za UDINI kwa CUF kweli?..kwa utaratibu huu CCM itaendelea kushinda Daima!!!

...Hio IKO wazi unaipata wapi? Are u trusting JF members kwa emotions zao za Vyama?Una hakika member fulani ni mwanachama wa CUF/Chadema/CCM thru contribution zao?
Ndio nina hakika.
Watanzania tuchoke kukaa kwa kujificha jificha.
Tuinue sauti zetu tuseme nini ni mapenzi yetu.
 
Uko sawa kabisa mkuu,jamaa alidhani akihama cuf atahama na wanachama wake.hali imekuwa tofauti.juzi nilikuwa bk wakati wa uchaguzi wa selikari za mitaa.niligundua cuf bado wako juu bk mjini na km mwakani watapata mgombea makini,rwakatre atakuwa amefulia mazima.
Mkuu siasa za bk mjini zimetawaliwa na udini Rwakatale alipendwa enzi za CUF kwa kuwa chama kilikuwa na mtizamo wa kiislam aliweza kushinda lkn alipopambanishwa na muislam mwenzie (Kagasheki) ukristo wake ukaonekana akaukosa ubunge,tuliokuwa Bukoba tuliviona vipeperushi vilivyokuwa vikisambazwa na vijana wa kiislam,cpendi kuamishia mjadala kwenye udini lkn ndo ukweli.
 
afisa ulinzi na usalama CDM HQ, ni mzuri sana wa political intelgency and security
 
This guy he knows politics sana na chuki yake na CCM si yakubahatisha .Akienda CCM kweli nitashangaa sana .Wacha tuone hayo yakiyosemwa.Chadema atakuwa wanamwangalia tu kama kweli ana harakati hizo .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom