Yuko wapi Nsa Kaisi ?

Huyu mzee ni muadilifu na mtenda haki sana,kwasasa anatenda haki ndani ya sekretarieti ya Ajira,ni mmojawapo wa wajumbe wa bodi ya sekretarieti,watu mnaoomba kazi na kupangiwa kazi serikalini mnapitia kwenye mikono yake.kwa mujibu wa mdau wangu pale huyu Mzee yupo serious sana na kazi na hapendi mtu aonewe wala apendelewe.
 
Duh he was the best friend of my daddy aiseehh!!!! Nyumba yake ina sebule tatu I mean utakaribishwa kutokana na class au hadhi yako nakumbuka mara ya mwisho kwenda kwake ilikuwa 2005 then the following year my fadher dead..duh mmenikumbusha mbali sana..
 
jamaa anapenda kusoma na hakuna mambo ya kubabaisha. hes a private person na kama unataka kumpata nenda kwa mzee beni atakuambaia rafiki yake yupo wapi
 
Serikali yamkomoa
msaidizi wa Mkapa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
Jumanne, Januari 15, 2013 05:20
Kanali mstaafu Nsa Kaisi, ambaye
amekuwa Msaidizi wa Rais
Benjamin Mkapa kwa miaka mingi,
amepokwa shamba lenye ukubwa
wa ekari 14 katika eneo la Pugu
Mwakanga mkoani Dar es Salaam.
Uvamizi huo umefanywa na kundi
la watu mnamo Oktoba 19, 2011.
Pamoja na kuwa na hati zote za
umiliki halali wa eneo hilo, Serikali
pamoja na vyombo vyake, hasa
Jeshi la Polisi mkoani Dar es
Salaam, imegoma kumsaidia.
Kaisi ambaye amewahi kuwa mkuu
wa wilaya na mikoa mbalimbali,
amehangaika kwa muda wote huo
katika ngazi nyingi, lakini
ameshindwa kabisa kupata msaada
wa kumwezesha kupata haki yake.
Kwa mujibu wa Mipango Miji, eneo
hilo limeteuliwa na kutengwa na
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya
huduma za viwanda, na yeye
amekuwa akilipia hati zote tangu
alipomilikishwa eneo hilo .
Kova amtosa, ataka aende
mahakamani
Hata Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Saalam,
Suleiman Kova, amekataa
kumsaidia kuwaondoa wavamizi
hao.
Kaisi analithibitisha hilo kwa
kusema, “Nilipoona sipati jibu kwa
barua yangu ya Januari 10, 2012
nilikwenda kuonana na DCP Kova.
Alinielekeza kwamba siyo kazi ya
polisi kuondoa wavamizi na
akanitaka nionane na DC (Mkuu wa
Wilaya ya Ilala) ili nipewe barua
kwenda mahakamani kupata ‘Court
Order’.
“Nilipokwenda kwa wanasheria
kutaka ufafanuzi zaidi, walishangaa
kwa wasimamizi wa sheria na
kanuni wamenieleza hivyo;
kutokana na kwamba wavamizi wa
eneo langu wameachiwa kuharibu
mali yangu halali kisheria, pamoja
na kwamba wametenda kosa
jingine kufuatana na Penal Code:
Under Section 299, Sub-section (a)
and (b) ambayo inazungumzia
‘Criminal Trespass’.”
Mwanzo wa matatizo yote
Uchunguzi unaonyesha kuwa
Novemba 24, 2011 alimwandikia
barua aliyekuwa Kaimu Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni , Jordan
Rugimbana; Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile;
(kwa wakati huo) na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala, Gabriel
Fuime; akiwaeleza juu ya uvamizi
huo, lakini kote huko hakusaidiwa.
Katika barua hiyo, Kaisi alisema,
“Kwa heshima nakuja mbele yenu
kuomba msaada wa kuwaondoa,
kuwakamata na kuwafikisha mbele
ya sheria kundi la wavamizi ambao
Oktoba 19, 2011, majira ya saa tatu
usiku walivamia na kuingia eneo
langu ninalomiliki kisheria, ambalo
lipo Pugu Mwakanga, Mtaa wa
Kigogo Fresh, Kata ya Pugu.
“Baada ya kutokea uvamizi,
msimamizi wa eneo hilo , Omari
Nyangala, alitoa taarifa kwenye
uongozi wa Serikali ya Mtaa, Kigogo
Fresh. Viongozi hao walichukua
jukumu la kuwaita wawakilishi wa
wavamizi na kuwaeleza kuwa eneo
linamilikiwa na mimi kisheria,
pamoja na kuwaonya kwamba
Serikali ya Mtaa haiwatambui na
inawataka waondoke katika eneo
hilo; wao waliwajibu viongozi wa
Serikali ya Mtaa kwamba, ‘sisi siyo
wavamizi ila tumekuja kuishi baada
ya kukuta kuna shamba pori,
mwenyewe ameshindwa
kuliendeleza kwa muda mrefu kwa
mujibu wa wenyeji walivyosema.
Tulikuwa hatuna mahali pa kukaa,
tumeamua tuishi hapo…Tupo watu
240 na tutaendelea kuwepo, iwapo
kuna mtu amejitokeza anasema
pake atupeleke mahakamani ili
tukasikilizwe maelezo yetu’.”
Imeelezwa kuwa baada ya
mahojiano na wavamizi,
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
aliyetajwa kwa jina moja la Maguno
alipeleka taarifa kwa Kamanda wa
Polisi Wilaya ya Sitakishari,
akiomba msaada wa kuwaondoa
wavamizi.
Kituo cha Polisi Sitakishari
kilifungua jalada STU/
RB/16093/2011/KUINGIA/JINAI.
Novemba 19, 2011 Mkuu wa Kituo
(OCD) hicho, Jumanne Muliro alifika
eneo la tukio na kuwakuta baadhi
ya wavamizi wakiendelea na ujenzi.
“OCD aliwafahamisha kwamba eneo
walilovamia lilikuwa na mmiliki
halali kisheria na kuwaelekeza
kwamba iwapo walihitaji eneo la
kujenga na kuishi inabidi wapeleke
maombi yao kwa viongozi wa
Serikali ya Mtaa.
“Pamoja na ushauri wa OCD,
wavamizi bado wapo wanakalia
eneo langu na kuendelea kuleta
uharibifu mkubwa…tayari
wameshateketeza mali zangu nyingi
na kupora vitu mbalimbali pamoja
na kuvuruga mazingira,” amesema
Kaisi katika barua yake kwenda
kwa Rugimbana.
Kaisi, anawaomba viongozi
wanaohusika katika utatuzi wa
mgogoro huo kwa kusema,
“Ninawasihi viongozi wangu
mchukue hatua zipasazo za haraka
za kushughulikia wavamizi hawa na
kulikomboa eneo langu.
Kitendo chao ni cha jinai, kinavunja
sheria na Katiba ya Tanzania …
binafsi nilionalo baya zaidi, ni kule
kuwepo katika jamii yetu makundi
ya wahalifu ambao wamejiandaa
kufanya na kuendeleza vitendo vya
kijinai with utter impunity na
wakati huo huo wakitishia amani
miongoni mwa jamii.
Kwa upande mwingine, inaashiria
kuwa kikundi cha watu 240
kilichovamia eneo langu ni
mojawapo tu ya vikundi vingine
‘crime active and operating’ katika
Wilaya ya Ilala na Jiji kwa jumla.”
Hata hivyo, ana maswali mengine
anayojiuliza: Je, hivi viko vingapi?
Pamoja na uvamizi wa ardhi,
vinaendeleza uhalifu gani
mwingine? Viongozi wa vikundi hivi
ni nani? Je, upo uwezekano
kwamba vikundi hivi vya wahalifu
vinashirikiana na baadhi ya
viongozi wa Serikali za Mitaa,
watendaji wa Kata, na makatibu
tarafa? Kwanini wanavikundi
wajigambe na kujieleza kuwa wao
ni Wakurya? Ni kweli kwamba
makao makuu ya vikundi hivi ni
maeneo ya Kitunda na Mombasa-
Ukonga?
Kaisi anahitimisha kwa kutoa ombi,
“Viongozi wangu, nikiwa raia
mwema, nina imani na mfumo wetu
wa kulinda watu na mali zao,
pamoja na kudumisha amani katika
nchi yetu kwa kuzingatia na
kuheshimu sheria; yaani kuwepo
kwa utawala wa sheria. Kwa hiyo,
ninaendelea kuwasihi kunipa
msaada wa kushughulikia ipasavyo
wavamizi wa eneo langu, pamoja na
kuwaondoa, kuwakamata na
kuwafikisha mbele ya sheria.”
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
azungumza
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Said Meck,
amezungumza na JAMHURI na
kusema hana taarifa za uvamizi wa
shamba la Kanali Kaisi.
“Kwa kweli sina habari, bahati
mbaya kwa sasa nipo Mwanza,
wasiliana na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala inawezekana yeye akawa na
uelewa wa suala hilo.
“Kila kitu kinakwenda kwa
utaratibu na sheria, tutaangalia
namna alivyovamiwa na tutafikia
mwafaka.
“Nakumbuka tuliagiza operesheni
ifanyike katika wilaya zote za Dar
es Salaam kuondoa waliovamia
ardhi ili irejeshwe kwa wamiliki
halali, Nadhani suala la
Mheshimiwa Kaisi litakuwa kati ya
hayo, wiki ijayo (wiki hii) nitakuwa
ofisini, nakuhakikishia kuwa haki
itatendeka,” amesema Meck.
Kauli ya DC wa Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi, ameiambia JAMHURI kuwa
ana taarifa zote zinazohusu uvamizi
wa mashamba na viwanja vya
wananchi katika maeneo mengi ya
Wilaya ya Ilala, yakiwamo ya Pugu,
Chanika na Msongola.
“Juhudi zinaendelea kufanywa
kukabiliana na hali hii, najua kabisa
uvamizi upo, lakini kusema ukweli
sikujua kama Mzee Kaisi naye yupo
kwenye matatizo haya.
“Inawezekana kweli akawa na
tatizo hilo kwa sababu kuna wakati
alimtumia mtu mmoja kuweka
miadi ya kuonana na mimi.
Nikawapa siku na muda wa
kuonana naye, lakini sikumwona,”
amesema.
Amesema kama mtu anamiliki
ardhi, na akatokea mtu akaingia
kwa jinai, ni wajibu wa polisi
kumwondoa mvamizi au wavamizi.
“ Kama ni civil matter inabidi iingie
mahakamani, Mahakama itoe order.
Sisi Serikali, polisi ni wajibu wetu
kusimamia kumtoa huyo mvamizi.
Kama ni sura ya criminal, yule
aliyeingia kwa jinai akamatwa,
anafunguliwa kesi mahakamani.
Kwa wasio na hati kuna mlolongo
mrefu kwa sababu inabidi
Mahakama isikilize na kutoa
uamuzi; kama Mzee Kaisi ana hati
hilo ni suala la kuwaondoa
wavamizi tu,” amesema.
Hata hivyo, Mushi ametoa rai kwa
vyombo vya habari kuhakikisha
vinawaelimisha wananchi ili wasiwe
kikwazo wakati wa kuwaondoa
wavamizi.
“Watu wanavamia maeneo ya watu
wengine kwa makusudi, tukitumia
nguvu kuwaondoa utasikia mara
ooh haki za binadamu zinavunjwa,
polisi wanatumia nguvu…
Haiwezekani kukawa na watu
ambao kazi yao ni kuvamia tu, na
pale wanapoondolewa ndipo
ionekane haki za binadamu
zinavunjwa.
“Vyombo vya habari vitusaidie
kukabiliana na wahalifu hawa,
amesema Mushi.”
 
DuppyConqueror

Navyojua aliteuliwa kuwa Mw/kiti wa Bodi ya Kuwaenzi waasisi wa taifa hili mwaka jana ama mwaka juzi. Sasa wewe unakuja na hoja hii watu waki-query wewe watukana vipi leta ushahidi
 
Hamna kumbu kumbu yoyote inayoonyesha kwamba huyu mzee alifariki. Ukitafuta sana unakuta mwaka 2013 aliporwa shamba lake la heka 14 pale Pugu, aliteuliwa kuchair Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Nyerere na Karume nk. Najiuliza mbona ngumu kupata taarifa za kifo chake
 
Hamna kumbu kumbu yoyote inayoonyesha kwamba huyu mzee alifariki. Ukitafuta sana unakuta mwaka 2013 aliporwa shamba lake la heka 14 pale Pugu, aliteuliwa kuchair Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Nyerere na Karume nk. Najiuliza mbona ngumu kupata taarifa za kifo chake
Nakumbuka akiwa mkuu wa wilaya Bukoba wahindi walichanga pesa wakampelekea ofisini kama "zawadi" akawaambia mpeni secretary awaandikie risit, asante kuchangia serikali, jamaa walikoma
 
Nakumbuka akiwa mkuu wa wilaya Bukoba wahindi walichanga pesa wakampelekea ofisini kama "zawadi" akawaambia mpeni secretary awaandikie risit, asante kuchangia serikali, jamaa walikoma

aha aha aha aha. Jamaa alikuwa kiboko ile mbaya
 
Hamna kumbu kumbu yoyote inayoonyesha kwamba huyu mzee alifariki. Ukitafuta sana unakuta mwaka 2013 aliporwa shamba lake la heka 14 pale Pugu, aliteuliwa kuchair Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Nyerere na Karume nk. Najiuliza mbona ngumu kupata taarifa za kifo chake

Jamani nani kasema amekufa? Mbona yupo?
 
Kondoa watambuka Kabenga Nsa Kaisi kwa ajili ya Mradi wa Maji wa Ntomoko alipokuwa DDD.
 
Sawa, Mkuu huyu Nsa Kaisi kama ulevi wa madaraka basi alilewa akawa chakali, habari zisizothibitisha huyu jamaa hana mke wala mtoto, mke wake alikuwa madaraka aliyokuwa nayo.

Akiwa ni mkuu wa mkoa wa Mtwara kwa kutumia madaraka yake anamiliki eneo kubwa zaidi ya eka 10 kwa wanaoishi Mtwara eneo hilo liko wazi hadi hivi leo limepakana na VETA na nyumba za kilimo pale Shangani, pia aliacha gari mpya kabisa mpaka sasa inaoza pale yadi za VETA, Pickup fulani hivi.

Eneo hilo la Shangani watu wanalimezea kweli, kumbe ana eneo lingine kama hilo huko Pugu.

Nawaunga mkono wanainchi waliovamia, kuna usemi unaosema kwamba "ukishiba sana usimwonyeshe Mungu tumbo" sasa Nsa Kaisi ameshiba sana anahodhi maeneo hawezi kuyatumia wacha wenye shida watumie.(2012)
 
alikuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara miaka ya nyuma,alafu inasemekana aliwah kuwa mwanajeshi mwenye cheo cha juu na alikuwa na elements za u-dictator

kanali Nsa kaisi jembe hili,miaka ile wakati ni RC mtwara ilikua ikifika jioni una muona mitaani na kibaiskeli chake ana piga misele.alikuaga mtemi balaa.
 
Duh he was the best friend of my daddy aiseehh!!!! Nyumba yake ina sebule tatu I mean utakaribishwa kutokana na class au hadhi yako nakumbuka mara ya mwisho kwenda kwake ilikuwa 2005 then the following year my fadher dead..duh mmenikumbusha mbali sana..
Mulugo anahusika hapa
 
Wewe Kenge nimeongea na Nsa Kaisi leo ( saa moja na nusu usiku huu)ni mzima wa afya! Mimi ni shemeji yake. Huyo aliyefariki pengine ni Nsa Kaisi mwingine unayemjua wewe. Acha kabisa kueneza uvumi ambao hauna msingi!

bora tumempata shemeji yake. Nakumbuka aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Mara miaka kadhaa kabla hajaenda Mtwara. lakini siku zote akiishi peke yake pale pamoja na kuwa na mifugo mingi-has ang'ombe wa kisasa. Niliwahi kusikia kuwa alikuwa ni KOMANDOO na alihasiwa ndio maana. Sasa Shemeji yake nikuulize, je ni kweli, na wanavyosema ana mtoto ni kweli, na ni shemeji yako kivipi. Namkubali jinsi alivyokuwa kiongozi shupavu kwa kweli -Mimi nilimwona akiwashauri akina mama fulani alipokuwa akifungua kikundi chao cha maendeleo. Tusaidie shemeji-sio vibaya kufahamu
 
bora tumempata shemeji yake. Nakumbuka aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Mara miaka kadhaa kabla hajaenda Mtwara. lakini siku zote akiishi peke yake pale pamoja na kuwa na mifugo mingi-has ang'ombe wa kisasa. Niliwahi kusikia kuwa alikuwa ni KOMANDOO na alihasiwa ndio maana. Sasa Shemeji yake nikuulize, je ni kweli, na wanavyosema ana mtoto ni kweli, na ni shemeji yako kivipi. Namkubali jinsi alivyokuwa kiongozi shupavu kwa kweli -Mimi nilimwona akiwashauri akina mama fulani alipokuwa akifungua kikundi chao cha maendeleo. Tusaidie shemeji-sio vibaya kufahamu
Mimi nimekanusha kuhusu kifo chake baada ya kuongea naye. Masuala mengine mimi siyo msemaji wake!
 
Yupo Dar. Umemtafuta ukamkosa? To say he doesnt have a kid, do you know him that well? Trust my words...he is safe and sound!!!!
Huyu bwana pamoja na wenzake wengi kujaa makovu ya rushwa na ubabaishaji, he has remained clean...hata wakati wa mzee wa uwazi na ukweli. He is still a character as todate...
A word of advise....usiende kwake bila appointment,lol!

Huyu ni col hasa wa Jeshi. Hana mzaha hata kidogo. Kwa tuliokuwa Mtwara miaka ile ya 90 tunamjua vizuri sana! Katika kisa kimoja pale Mtwara alizuia meli isichukue chakula ( nadhani yalikuwa mahindi) kwenda kisiwani Zanzibar kwa maelezo kwamba mkoa wenyewe haujitoshelezi, jibu straight hamna bla bla, unapewa facts na makavu live!
 
Siyo kweli na hakwenda vita ya kagera,ana mtoto mmoja.
Aliwahi kufukuzwa bungeni wakati wa nyerere kwa kuvaa jeans na tshirt.

Tena na pensi. Kuna mtu humu kadanganya kuwa mzee Col Nsa hatuko naye, huu ni uongo kabisa.
 
Back
Top Bottom