Mongoiwe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 524
- 263
Asalaam Aleikhum.. kupo nipo nipo ila haya mambo ya kijijini ya kutumia mtandao kwa simu kwa kweli sijayazoea. Nitarudi mjini muda si mrefu tumekuja kusalimia wakwe kidogo. Ukiondoa cellphones zilizozagaa.. kijijini hakujabadilika, duka la mzee Mswahili bado lipo pale pale, ile nyumba kwenye kona kwenda shuleni iko vile vile kama inataka kudondoka.. ila huko mjini utadhani niko Detroit!
MKUU;
Bora umejitokeza maana watu walikuwa wakifikiri umenunuliwa na mafisadi. Pole inaonekana ulilowea mjini, sisi tulishazoea sana maisdha ya Bush, kwani hiyo ndiyo Bongo yetu.
Uasipime maisha ya Mjini ni tofauti kwa asilimia 900 na yale ya kijijini Utadhani ni nchi mbili tofauti, kumbe moja.
Najua hujabahatika kunywa chai toka umefika kijijini, kama umekunywa basi ni kwa visenti vyako ulivyotunza kwa ajili ya kuwasaidia wazazi huko kijijini, au kutokana na hali ilivyo umesingizia swaumu.
Hali hii yote inatokana na kile tunachokipingania kila siku, tunachokilalamikia kila kukicha, tunachokazania kukiondoa hapa nchini. UFISADI