Yuko Wapi Mzee Mwanakijiji?

Status
Not open for further replies.

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Hii si kawaida, karibia siku 8 zimepita huyu mkuu hajatia mguu hapa ukumbini! Stats zinaonyesha post yake ya mwisho ilikuwa tarehe 24 August.

Members wengine wakikosekana barazani lazima tujiulize, kulikoni? Wiki tumeshudia wapiganaji wetu wamejeruhiwa huku demokrasia ikisiginwa kule 'CHAMA MBADALA' na mafisadi wakifanya tafrija kucherehekea magoli.

Vipi ka-inzi kamekatwa mbawa tulete 'super-glue'?

Nawasilisha!
 
nadhani tayari na yeye ametekwa na mafisadi. si unajua mambo ya mapesa haimtupi mtu
 
kwi kwi kwi .... ulisikiliza clip iliyoitoa kwa mara ya mwisho kabla ya kwenda mafichoni? Labda nikwambie kuwa hakuna mwenye njaa ya mabadiliko ya kisiasa Tanzania kama M.M. Mwanakijiji. Hivyo, haya yanayoendelea CHADEMA kwake ni msiba mkubwa sana.

Pole sana M.M.M, come out man, we need you. Sote tunaumia na kuchanganyikiwa lakini hali ndo hiyo. Weakness kubwa ya vyama vya upinzani ni kwamba wanachama wengi (wenye nguvu za kisiasa) ni wale walioondoka vyama vingine kwasababu walikosa vyeo vizuri. Hivyo wananjaa kubwa ya vyeo. Kilichowakutanisha pamoja ni njaa ya vyeo siyo itikadi wala uzalendo.

Hapa ndo ninapopata shida na kujiuliza nani atatuokoa mikononi mwa CCM?
 
my cuzin mwanakijiji yupo ila ametingwa na mambo mengi tuu na wala hajatekwa ma the so called MAFISADI....yeye ni mpiganaji ahodari sana....atarudi tuu subirini goli atakalo kuja nalo mtabloo mapigo sasa hivi anaanda mada.....
 
Hata mimi najiuliza, yuko wapi? ngau yeye kakaa kimya maana naamini anaumwa tumbo, homa n.k kusikia yanayotokea CHADEMA.
 
Nadhani atakuwepo tu hapa ukumbini, hali ya hewa CHADEMA imechafuka huenda amekuja na aka nyingine! Speculation....
 
yupo kwenye mkutano mkuu wa chadema nilionana nae jana ila ndo kama hivyo alikuwa mnyonge sana kutokana na msigano unaofanywa na wachaga huko chamani.
 
Wacheni personality cult nyie, kwani Mwanakijiji ndio nani? Wacheni unyonge wa akili!
 
yupo kwenye mkutano mkuu wa chadema nilionana nae jana ila ndo kama hivyo alikuwa mnyonge sana kutokana na msigano unaofanywa na wachaga huko chamani.

no thank you.
 
Wacheni personality cult nyie, kwani Mwanakijiji ndio nani? Wacheni unyonge wa akili!

Si unajua wabongo wengine tulivyozoea kuletewa nakutafuniwa , akiondoka mtu kama MMK siku mbili tatu watu wanakosa pipi.

kama ushahamasishwa na MMK fuata nyayo, hivi tutaweza kujenga movement kwa kumuangalia mtu mmoja kweli? Kama unamtafuta M-PM.
 
jama, mbona Mzee mwanakijiji yupo? Jana kachangia hoja fulani na hata leo ofcourse sikuonana nae lakini rafiki yangu kaonana naye. Msihofu mzee yupo ila siku chache hizi yuko na kazi nyingi kwa sababu anaandaa Meremeta - 2.
 
Clue: Post zake za mwisho zilikuwa zinaongelea kushindwa kwetu vita dhidi ya ufisadi...
 
Mwanakijiji yupo kwani ndo alituma final report ya meremeta juzi au hukiuona ndugu yangu? Kuna na Invisible naye hajatokea kwa muda naye sijui vipi. Atujuze kulikoni?
 
Clue: Post zake za mwisho zilikuwa zinaongelea kushindwa kwetu vita dhidi ya ufisadi...
Bado hajarudi! Inaelekea Mzee Mwanakijiji kaisusa JF?
jama, mbona Mzee mwanakijiji yupo? Jana kachangia hoja fulani na hata leo ofcourse sikuonana nae lakini rafiki yangu kaonana naye. ....- 2.
Wana JF mnatakiwa mkumbuke kuwa huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, na nahisi ni swaumu tu inamchosha na kusababisha asishiriki shiriki sana katika kona yetu hii. Nahisi muda mwingi anautumia kumcha Mwenyeezi Mungu na kuomba toba, hapa tutamwona zaidi baada ya mfungo;-)
 
Asalaam Aleikhum.. kupo nipo nipo ila haya mambo ya kijijini ya kutumia mtandao kwa simu kwa kweli sijayazoea. Nitarudi mjini muda si mrefu tumekuja kusalimia wakwe kidogo. Ukiondoa cellphones zilizozagaa.. kijijini hakujabadilika, duka la mzee Mswahili bado lipo pale pale, ile nyumba kwenye kona kwenda shuleni iko vile vile kama inataka kudondoka.. ila huko mjini utadhani niko Detroit!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom