Yuko wapi Mr Blue?

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Kherry Sameer Rajab, ambaye aliwahi kung'ara kimuziki miaka ya mwanzoni mwa 2000 amepata mtoto wa kiume.

Kherry, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Mr. Blue alipata mtoto huyo wa kiume wiki mbili zilizopita baada ya mchumba wake kujifungua.


Mchumba wake huyo, ambaye Mr. Blue aliwahi kumtambulisha kwa jina la Wahida, alijifungua mtoto huyo mjini Dar es Salaam.


"Nimevuka hatua moja kwenda nyingine,"alisema Mr. Blue alipozungumza na mitandao mbalimbali.
"Kwa sasa mimi si mvulana tena bali ni baba, naitwa Baba Sameer," alisema Mr. Blue huku akitabasamu.


"Nimeamua kumpa mtoto wangu jina hili maana naona linamfaa, kwani ni jina langu la pili, ambalo nimekuwa nikilitumia kwa muda mrefu, pia ni jina la baba yangu," aliongeza.
Mr. Blue alianza kujihusisha na masuala ya muziki mwaka 1999 na kilichosababisha ajitose kwenye fani hiyo ni kaka zake, waliojulikana kwa majina ya The Boy Stain na Obrey.


Kaka zake hao walianza kujitosa kwenye muziki mapema na kusababisha naye avutiwe na fani hiyo na kuamua kuyapa kisogo masomo.
Hata hivyo, Mr. Blue hakuanza kuimba moja kwa moja. Alikuwa akifuatilia ni jinsi gani muziki unatengenezwa na kuanzia mwaka 2001 alikuwa akipenda kuhudhuria sherehe mbalimbali za vikundi vya mitaani.
Mwishoni mwa mwaka 2003, ndipo Mr. Blue alipoanza kuchomoza kimuziki baada ya kuibuka na kibao chake cha kwanza kinachojulikana kwa jina la Mr. Blue, ambacho kilimpatia umaarufu mkubwa.


Baadaye aliibuka na kibao chake cha pili kinachokwenda kwa jina la Mapozi, ambacho kiliendelea kumtangaza vyema katika soko la muziki wa bongo fleva.


Baada ya kutikisa soko la muziki huo kwa kipindi kirefu, ndipo msanii huyo mwenye sura yenye mvuto alipoachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Mr. Blue' na kufuatiwa na albamu ya ‘Yote kheri'


Na sasa baada ya ukimya wa muda mrefu, Mr. Blue ameibuka na video ya wimbo wake mpya wa Loose Control, ambao ameuimba kwa kushirikiana na msanii Majol Power.
Mr. Blue amesema katika video hiyo, amekuja kwa staili tofauti kuanzia katika mavazi, uchezaji pamoja na uimbaji, lengo likiwa ni kuongeza ladha ya muziki wake kwa mashabiki.


Msanii huyo alizaliwa Aprili 14, 1987. Ni mtoto wa tatu kati ya wanne kwa kuzaliwa katika familia ya mzee Sameer Rajab mwenye asili ya Ki-Sudan.
Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya Gerezani, ambako alihitimu darasa la saba mwaka 1999. Hata hivyo, hakuweza kumaliza elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Dar es Salaam, ambako aliishia kidato cha pili mwaka 2004.


Alipoulizwa ni kitu gani kilichosababisha kukatisha masomo yake ya sekondari, alisema: "Muziki ndio ulionifanya nikaacha shule, lakini bado nahitaji kusoma na baada ya muda nategemea kujiendeleza kimasomo nje ya nchi."


Akizungumzia hatua waliyochukua wazazi wake kutokana na kuacha kwake shule kwa sababu ya muziki, anasema hawakumgombeza kwani walijua ni ujana tu unamsumbua huku wakiamini itafikia wakati atatulia


Anawashukuru mama yake mzazi, Halima Rajab na baba yake Sameer Rajab kwa kumruhusu kujikita katika muziki, ambao umemwezesha kupata faida kubwa kimaisha

BLUUU.jpg
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom