Yuda Iskariote.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Siku moja YESU alipokuwa akijiaandaa kupanda mlimani kwenda kusali,aliwaambia mitume wake wabebe jiwe moja moja.Mitume wote walibeba mawe yenye ukubwa wa wastani isipokuwa Yuda Iskariote,yeye kwa ujanja na uvivu wake alibeba kajiwe kadogo kama kidonge cha Asprin.Walipofika mlimani baada ya sala,YESU aliyaombea yale mawe akayageuza kuwa mikate na kila mtume alikula mkate wenye ukubwa sawa sawa na ukubwa wa jiwe alilobeba.
 
Siku ya pili,YESU kama kawaida aliwaambia wabebe jiwe moja moja.Yuda kwa hasira na usongo aliokuwa nao alibeba bonge la jiwe ili likiwa mkate ale kipande cha kushiba na kitakachobaki akauze apate hela.Walipofika juu mlimani baada ya sala kwisha,YESU aliwaambia mitume wake watupe chini yale mawe waliyobeba kwa sababu alishawaandalia maandazi na soda!
 
Moral of the story;ujanja ukiuzidisha si muda mrefu utaitwa mshamba!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom