Yuda Iskariote(2).

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Siku moja Yesu alimtuma Yuda akanunue kuku saba kwa ajili ya sherehe.Katika kuwaandaa wale kuku,Yuda aliiba mguu mmoja kwa kila kuku.Wakiwa mezani Yesu akahoji;Yuda,hapa kuna miguu 7 ya kuku,miguu mingine 7 iko wapi?Yuda akajibu,"yaani mkuu mpaka leo hujui kwamba kuku hutembea kwa mguu mmoja,kwa hiyo kuku 7 wana miguu 7 na sio 14!".Yesu hakutaka ubishi,wakaendelea kula.Wakiwa nje,Yuda alimwonesha Yesu Jogoo aliyesimama kwa mguu mmoja kama ushahidi kwamba kuku ana mguu mmoja.Yesu akamrushia jiwe yule jogoo na yule jogoo akachomoa mguu wa pili,akakimbia kwa miguu miwili.Yuda akasema,"mimi sishangai,umeshaanza miujiza yako,umemrushia jogoo jiwe kisha ameota mguu wa pili na kukimbia kwa miguu miwili!
 
Jocks nyingine kama hizi sio nzuri so tutafute zenye maadili yesu siowachezea kiivyo
 
Jaguar,
Vitu vingine hata huitaji kwenda darasani. Ni vema ukatumia common sense ktk kuamua vitu vingine. Wewe huo upuuzi umeutoa wapi kwenye maandiko matakatifu? Jaribu kufikiria namna unavyotaka kuwasilisha UPUUZI WAKO na si kutumia jina la YESU katika upuuzi wako. Kichekesho kama hicho ungeweza kutoa mfano wa hata FAMILIA YAKO NA UKAELEWEKA.
 
acheni mbona mnakuwa wakali,ndo mana ikaitwa jokes,wengine mnajifanya mnamjua yesu wakati hata hamfanyi sala
 
Sio kila kitu kimeandikwa katika bibilia.....kuna mambo mengi tu yameachwa kutokana na sababu moja au nyingine, sasa sio mnaanza kuwa wakali kupitiliza kwa maana ya kuwaona nyie ndio wacha mungu sanaaa kumbe inawezekana kwenda church pasaka kwa pasaka, na sidhani kama kuna baya lolote jamaa kaliandika hapo mpaka mmekuja juu hivyo, tafuteni masalio ya biblia ndio mtaona vituko zaidi ya hivyo. Nyie hamjiulizi kwanini hamjaelezewa ukuaji wa Kristo Yesu ulikuaje na maisha yake ya kila siku aliyoishi hapa duniani hadi na ufufuo wake?
 
Jaguar,
Vitu vingine hata huitaji kwenda darasani. Ni vema ukatumia common sense ktk kuamua vitu vingine. Wewe huo upuuzi umeutoa wapi kwenye maandiko matakatifu? Jaribu kufikiria namna unavyotaka kuwasilisha UPUUZI WAKO na si kutumia jina la YESU katika upuuzi wako. Kichekesho kama hicho ungeweza kutoa mfano wa hata FAMILIA YAKO NA UKAELEWEKA.
Duuuuuuuuuuuh!haya bhana.
 
Back
Top Bottom