Yu wapi Cheusimangala?

kashai siyo kaisha, butege siyo matege?
uporotoye maisha, mtoto yake amege
cheusi wako kaisha, pale kapata kidege,
wenzio wasema pisha, fanya hima usitege

kiumbe yako huruma, dunia kwako katili,
japo mapenzi yavuma, cheusi hachi ukali,
uporoto ndo auma, japo u-radhi kwa mali
wenzio wasema pisha, fanya hima usitege

huwa nakukubali sana Judith,
A woman of all weather!!!,
uzuri wako wewe ni kiungo mchezeshaji kama ingekuwa ni soka,
kote kote unafit, na unajua kuunganisha mipira yote!!
hongera sana!!!!
 
Wanaokimbia riadha,wanalipwa wanafarijika,
unakimbia mchakamchaka unachoka,
oooh...cheusi,anakuletea makuzi,labda hayajui mapenzi,utampaje shavu badala alibusu anakupiga kofi?
Usilie sana maana we sio mtoto, usilaumu yeyote ulizaliwa peke yako. Ila jipe moyo maana hata Mungu hajawahi kupuzika tangu amuumbe mwanamke hivyo ndivyo wanaume nao hawajapata kupumua kabisa...ila the nature will provide.
 
Kumbe humu ndani kuna wataalamu wa vina!!

Umeona Katavi,

Yaani nimehisi Mungu kanionea...Kwani walau siku moja ninengemtungia bibi walau ubeti mmoja.....Hapo nimenyoosaha mikono..kama ni mtihani below ni halali yangu!
 
Hivi, kashaijabutege,
kumbe shairi linaweza kukusaidia ukango'a mzigo eeeh?
kazi kwake Uporoto01!!!!!!


Asali imesingiziwa, ushairi kwa utamu,
Mfanowe si maziwa, ilivyo tamu kalamu,
Ushairi maridhawa, watikisa kama bomu,
Upaonapo pagumu, ushairi penyezewa
 
Tunashukuru kashaijabutege na mis judith kwa kuburudisha mioyo yetu
 
kashai siyo kaisha, butege siyo matege?
uporotoye maisha, mtoto yake amege
cheusi wako kaisha, pale kapata kidege,
wenzio wasema pisha, fanya hima usitege

kiumbe yako huruma, dunia kwako katili,
japo mapenzi yavuma, cheusi hachi ukali,
uporoto ndo auma, japo u-radhi kwa mali
wenzio wasema pisha, fanya hima usitege

Butege sio matege, maana yake kidume,
Nala mvinyo si mbege, Kabuteigi mfalme,
Jua JOGOO si ndege, Uporoto ni mahame,
Kwa Cheusi mie ngome, Uporoto asiige.
 
Butege sio matege, maana yake kidume,
Nala mvinyo si mbege, Kabuteigi mfalme,
Jua JOGOO si ndege, Uporoto ni mahame,
Kwa Cheusi mie ngome, Uporoto asiige.

rehema kwako butege, unywapo mchungu mvinyo,
bora ingekuwa rege, ipate tikisa vikonyo,
wako heri ya mbege, cheusi kaasi onyo,
jogoo sasa kidege, cheusi huyo kayea

heri mrudie mola, kuliko kutoka hola,
sijali hiyo ngwala, bora umetunza hela,
sasa geukia sala, upate epa mitala
jogoo sasa kidege, cheusi huyo kayea
 
Tunashukuru kashaijabutege na mis judith kwa kuburudisha mioyo yetu

asante mpenzi mati, thamani hii kunipa,
nilikuwa kama bati, hutuzi wala kutupa,
sasa wanituza pati, kwa skuna bila malapa
nami naikaza buti, tayari mwendo kuchapa
 
huwa nakukubali sana Judith,
A woman of all weather!!!,
uzuri wako wewe ni kiungo mchezeshaji kama ingekuwa ni soka,
kote kote unafit, na unajua kuunganisha mipira yote!!
hongera sana!!!!

asante mpenzi bacha, kwa tele zako pongezi,
hata tungekuwa pacha, nisingekosa kuenzi,
wanena kama kocha, nifunda chezea mwanzi,
pongezizo sitaficha, ntajidunga bila ganzi
 
Back
Top Bottom